Chanzo Cha Moyo Kutanuka Na Tiba Yake

moyo kutanuka
afya ya moyo

Nini maana ya moyo kutanuka?

Moyo kutanuka kwa kitaalamu cardiomegally, maana yake moyo wako umekuwa mkubwa kupita kiwango cha kawaida. Moyo unatanuka pale misuli yake inapofanya kazi kupita kiasi mapaka inapanuka na kufanya chemba za moyo nazo kutanuka.

Kumbuka tu na ufahamu hili, kwamba moyo kutanuka siyo ugonjwa. Ni dalili ya ugonjwa fulani wa moyo unaopelekea mpaka moyo ufanye kazi kupita kiasi ya kupump damu. Magonjwa haya yanweza kuwa kupanda kwa presha ya damu na pia matatizo ya valve za kwenye moyo.

Moyo uliotanuka hauwezi kusambaza damu vizuri kwenye maeneo mbalimbali ya mwili ukilinganisha na moyo mzima. Kitendo hichi kinakuweka kwenye hatari ya kupata kiharusi na hata moyo kufeli.

Ni kipi chanzo cha moyo kutanuka?

Chanzo kikubwa cha moyo kupump damu kwa nguvu na hatimaye kutanuka ni kuziba kwa mishipa ya damu. Mishipa ya damu inaziba kwa kujikusanya kwa mafuta mabaya. Kuziba huku kwa mishipa kunapelekea misuli ya moyo itumie nguvu nguvu kusukuma damu, na hatimaye shinikizo la damu kupanda. Kuna vihatarishi vingine kama

  • maambukizi ya virusi kwenye moyo
  • ukuaji wa valve za moyo usio wa kawaida
  • mimba, hasa wakati wa kujifungua
  • magonjwa ya figo
  • matumizi makubwa ya pombe na dawa za kulevya
  • maambukizi ya virusi vya Ukimwi
  • matatizo ya kurithi
  • matatizo ya tezi ya shingoni (thyroid)

Shambulizi la moyo

Wakati wa shambulizi la moyo, sehemu kadhaa za moyo hazipati hewa ya kutosha ya oxygen na hivo kuathiri misuli ya moyo.

Mabadiliko ya mapigo ya moyo mara kwa mara na kupelekea damu kurudi kwenye moyo na kuathiri misuli

Upungufu wa damu

Ni zipi dalili za moyo kutanuka?

Wakati mwingine tatizo la moyo kutanuka linaweza lioneshe dalili zozote linakutafuna taratibu bila hata ya wewe kujua. Dalili zikianza kujionyesha ni hizi hapa

  • kushindwa kupumua vizuri
  • mabadaliko ya mapigo ya moyo
  • kuvimba kwa miguu na vifungo vya miguu kutokana na kujaa maji
  • mwili kukosa nguvu na kizunguzungu
  • maumivu ya kifua
  • maumivu kwenye mikono, mgongo au shingo na kupoteza fahamu

Ukipata dalili hizi hakikisha unaenda hospitali mapema kupata vipimo ili uanze tiba.

Mazingira hatarishi zaidi yanayopelekea moyo kutanuka

Upo kwenye hatari zaidi ya kupatwa na shida ya moyo kutanuka endapo.

  • una shinikizo kubwa la damu
  • uzito mkubwa na kitambi
  • unaishi bila kufanya mazoezi ya viungo
  • familia yako iliwahi kuugua
  • una magonjwa ye tezi ya thyroid
  • unatumia madawa ya kulevya na pombe kupita kiasi na
  • kama uliwahi kupatwa na shambulizi la moyo

Vipimo kugundua moyo uliotanuka

Daktari ataanza kwa kuuliza maswali kadhaa kuhusu dalili unazopata. Pia anaweza kupendekeza ufanyiwe X-ray ya moyo kuona kama moyo umetanuka. Vipimo vingine vitafanyika kujua chanzo cha moyo wako kutanuka. Vipimo hivi ni kama

  • Echocadiogram (ECHO)- kipimo kinatumia mawimbi ya sauti kucheki tatizo lolote kwenye chemba za moyo
  • Electrocadiogram(ECG)- kipimo kinachofatilia umeme wa kwenye moyo ili kuona mabadiliko ya mapigo ya moyo.
  • Kipimo cha damu-kuona kama kuna tatizo la homoni
  • CT-Scan– kipimo kinatumia mionzi ya X-rays kupata picha nyingi zaidi kuhusu moyo wako
  • MRI– kipimo kinatumia nguvu ya usumaku kutoa picha za ndani ya moyo.

Tiba ya moyo kutanuka

Daktari atapendekeza tiba kulingana na chanzo cha tatizo lako. Tiba hizi zinaweza kujumuisha

  • dawa za kupunguza presha
  • pacemaker ama kifaa kingine cha kupandikizwa kuratibu mapigo ya moyo na
  • dawa za kumeza kwa ajili ya moyo uliofeli

Ushauri kuhusu mabadiliko ya mtindo wa maisha kuepuka tatizo

  1. Jiwekee ratiba ya kufanya mazoezi wala mara 4 kwa wiki
  2. Acha kuvuta sigara na upunguze unywaji wa pombe
  3. Anza kupunguza uzito kwa kufuata mpango wa lishe
  4. Punguza kula baadhi ya vyakula kama vyakula vya sukari na wanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *