Kuvimba Mlango wa Kizazi au Shingo ya Kizazi

mlango wa kizazi
kizazi

Shingo ya ya mlango wa kizazi ni kitu gani?

Shingo ya kizazi au mlango wa kizazi ni eneo la chini kabisa kwenye kizazi chako. Hapa ndipo damu ya hedhi hutokea baada ya ukuta wa kizazi kubomoka. Wakati wa leba shingo ya kizazi hufunguka ili kupisha mtoto azaliwe kwa njia ya uke. Shida ya kuvimba mlango wa kizazi inawatokea wanawake wengi.

Kama ilivyo kwa tishu zingine za mwili, tishu za shingo ya kizazi zinaweza kututumka na kuvimba pia kutokana na sababu mbalimbali. Kitaalamu kuvimba kwa shingo ya kizazi huitwa cervicitis.

Zipi ni dalili za kuvimba mlango wa kizazi?

  • kuvuja damu kusiko baada ya tendo au wakati mwingine
  • maumivu ukeni
  • kutokwa a uchafu wa kijivu na mweupe wenye harufu mbaya kwa muda mrefu
  • maumivu ya mgongo
  • kuhisi kama mgandamizo kwenye nyonga na kiuno kuwa kizito
  • maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Nini kinasababisha kuvimba mlango wa kizazi?

Sababu kubwa inayopelekea kizazi chako kuvimba ni maambukizi. Maambukizi haya yanaweza kupatikana hasa kutokana na tendo la ndoa.

Kuvimba huku kwa kizazi tunaweza kuweka katika makundi mawili,
Acute cervicitis– ambapo dalili hujionesha haraka na kupotea na
Chronic cervicitis– ambapo dalili huchukua miezi mingi bila kupotea.

Kuvimba shingo ya kizazi husababishwa hasa na magonjwa ya zinaa kama

Kuvimba kwa shingo ya kizazi pia kunaweza kusababishwa na maambukizi kutokana na sababu mbalimbali kama

  • aleji ya kondomu
  • kitanzi
  • matumizi ya pedi au tampon
  • maambukizi ta mara kwa mara ya bakteria

Vipimo kugundua uvimbe kwenye shingo ya kizazi

Kama una dalili za kuvimba kwa shingo ya kizazi, muhimu umuone daktari kwa ajili ya uchungizi zaidi. Kumbuka dalili hizi za kizazi kuvimba zinaweza kushiria tatizo kubwa zaidi la kiafya.

Daktari pia anaweza kugundua kuvimba kwa shingo ya kizazi chako kama huwa unafanya vipimo hospitali mara kwa mara. Zifuatazo ni njia anazotumia daktari kufanya uchunguzi wa shingo ya kizazi kuvimba.

Bimanual pelvic Exam

Kwenye kipimo hiki, daktari ataingiza kidole chake ukeni chenye glove, kisha mkono mwingine atabinya tumbo kwa nguvu. Hii itamsaidia daktari kugundua uvimbe wowote usio wa kawaida kwenye shingo ya kizazi .

Pap test

Kwenye kipimo hiki, daktari aatachukua sampuli ya ute ute au uchafu wa ukeni, kisha atapeleka maabara kuufanyia vipimo kuona kama kuna shida.

Cervical biopsy

Daktari anaweza kupendekeza kipimo hichi endapo kipimo cha pap test kimeonesha kuwepo kwa seli zenye tatizo. Wakati wa kipimo hichi daktari huingiza kifaa kinachoitwa speculum kwenye njia ya uke.

Kwa kutumia kifaa kingine kinachoitwa colposcope daktari atachunguza eneo a shingo ya kizazi, kisha atakata sampuli ndogo ya nyama kwenye eneo lililovimba na kupeleka maabara kwa vipimo.

Cervical discharge culture

Kipimo hichi ni cha kuotesha kuona kama una maambukizi ya fangasi aina ya candida. Daktari atachukua sampuli ya uteute wa ukeni kisha ataotesha kwa siku kadhaa na kuupima.

Tiba kwa tatizo la kuvimba mlango wa kizazi

Hakuna tiba ya moja kwa moja ya kuvimba shingo ya kizazi. Daktari wako atakushauri tiba sahihi kulingana na chanzo cha tatizo lako, hali ya afya yako, historia ya tatizo, ukubwa wa tatizo na dalili zote unazopata.

Tiba kuu ni kupitia antibiotics kwa ajili ya kutibu maambukizi. Kama shingo ya kizazi imevimba kutokana na kutumia pedi, tampon au kitu chochote cha kuingiza ukeni basi suluhisho itakuwa ni kuacha kutumia kitu hicho.

Kama shingo ya kizazi imevimba kutokana na saratani, daktari anaweza kupendekeza unazishiwe tiba ya mionzi ili kuua seli za saratani.

Bila kupata matibabu ya uhakika tatizo lako la kuvimba kwa shingo ya kizazi onaweza kuwa kubwa zaidi na kuleta maumivu makali zaidi wakati wa tendo.

Yapi Madhara Makubwa ya Kuvimba Shingo ya Kizazi?

Kuvimba kwa shingo ya kizazi kutokana na magonjwa ya zinaa hupelekea kusogea kwa ukuta wa kizazi na mirija ya uzazi na kusababisha maambukizi kwenye kizazi-PID. PID huongeza zaidi maumivu ya nyonga, kutoka uchafu mwingi na homa. PID isipotibiwa mapema husababisha ugumba.

Jinsi gani naweza kujizuia changamoto ya kizazi kuvimba?
Kuna njia kadhaa zitakazokusaidia kupunguza hatari ya kuvimba kwa shingo ya kizazi. Tumia kondomu kila mara unapofanya tendo na mtu usiyemwamini kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa.

Usitumie bidhaa zenye kemikali, kama tampons za kunukia li kupunguza aleji. Kama unatumia kitu chochote cha kuingiza ukeni mfano tampon, hakikisha unafuata maelekezo sahihi muda gani wa kukitoa na kujisafisha.

Bofya kusoma makala inayofuata kuhusu: Kina cha uke wako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *