Categories
Afya ya mwanamke na uzazi Hedhi salama

Maumivu ya Tumbo la Chango

tumbo la chango

tumbo la chango

Chango ni kitu gani hasa?

Tumbo la chango au mchango, wengi husema wakimaanisha maumivu makali ya tumbo kipindi cha hedhi. Kitalamu maumivu haya huitwa dysmenorrhea, ikimaanisha maumivu kutokana na kujikaza kwa ukuta wa kizazi ili ubomoke na kutoa damu kipindi upo kwenye hedhi.

Aina za tumbo la chango

Kuna aina kuu mbili za maumivu haya ya hedhi ama mchango, ambayo ni primary dysmenorrhea na secondary dysmenorrhea.

Primary Dysmenorrhea (Tumbo la Chango la kawaida)

Chango hili la uzazi ni yale maumivu ya kawaida yanayokupata kila mwezi kwenye hedhi na hayatokani na ugonjwa wowote. Maumivu haya huanza siku moja ama mbili kabla hujapata hedhi yako. Waweza kuhisi maumivu kwenye nyonga, kiuno na tumbo pia.

Pia chango la namna hii huchukua masaa 12 mpaka 73 yani siku 3 kuisha, na inaambatana na dalili zingine kama kichefuchefu na kutapika na hata kuharisha. Chango la namna hii huwa linapungua kadiri unazozeeka ama pale utakapozaa.

Secondary Dysmenorrhea (Tumbo la Chango lisilo Kawaida)

Chango lako linaposababishwa la ugonjwa fulani kwenye via vya uzazi. Chango hili huanza mapema zaidi kwenye mzunguko hata wiki kabla na inachukua mda mrefu sana kuisha. Mara nyingi chango hili halina dlaili za kuchefuchefu, kutapika kukosa nguvu na kuharisha.

Nini kinapelekea upate maumivu makali sana kwenye hedhi?

Maumivu hutokea pale kemikali inayoitwa prostaglandin inapofanya ukuta wa kizazi kujikaza. Ukuta wa kizazi ambapo mtoto hujishikiza na kukua,umetengenezwa kwa misuli, na unajikaza kwenye hedhi ili kubomoka kutoa damu isiyohitajika.

Ukuta unapojikaza sana, unaleta mgandamizo kwenye mishipa ya karibu ya damu, na hivo kupunguza kiwango na hewa safi ya oksijen kwenda kwenye misuli. Na misuli inapokosa hewa ndipo unapata maumivu makali.

Chango la uzazi kutokana na ugonjwa

Chango hili laweza kutokea kwa kusababishwa na ugonjwa fulani, changamoto hizi ni pamoja na

 1. Endometriosis: Changamoto ambapo kuta za kizazi zinakua na kwenda nje ya kizazi. Tishu hizi nyakati za hedhi zitapelekea maumivu makali na kuvimba.
 2. Adenomysis: Hili ni tatizo ambapo kuta za kizazi zinakua kuelekea kwenue misuli ya kizazi. Tatizo hili kaweza kupelekea kizazi kutanuka na hivo kuletea bleed nyingi yenye maumvu
 3. PID: Haya ni maambukizi ya bakteria kwenye njia ya uzazi. PID yaweza kuleta maumivu makali chini ya kitovu, kwenye tendo na maumivu nyakati za hedhi yani chango.
 4. Fibroids: Hizi ni vimbe ambazo siyo za saratani ndani au nje ya kizazi, zinazopelekea chango kali sana
 5. Cervical stenosis: Hiki ni kitendo cha mlango wa kizazi kusinyaa na hivo kuzuia damu kutoka kwa kasi nzuri hivo kuleta maumivu ya chango kwenye hedhi.

Vipimo: Utajuaje kama Chango lako la kawaida au ni hatarishi?

Kama chango lako linachukua zaidi ya siku 3, hakikisha unaenda hospitali kufanyiwa vipimo. Kumbuka aina zote za chango zinaweza kutibiwa hospital na hata kwa tiba asili. Muhimu kwanza ni kujua nini kipo nyuma ya chango lako.

Kwanza kabisa daktari atakwambia ujieleze dalili zote unazopata kwenye hedhi pamoja na mzunguko wako ukoje. Pili daktari atakufanyia vipimo ndani ya via vya uzazi(pelvic exam) ambapo ataingiza kifaa ukeni kucheki kama kuna hali yoyote isiyo ya kawaida kwenye uke, mlango wa kizazi na kizazi chenyewe.

Daktari anaweza pia kuchukua kiwango cha majimaji kwenye uke na kupeleka maabara kwa ajili ya vipimo zaidi.

Nini kinatokea kama kuna ugonjwa?

Kama daktari atahisi pengine kutokana na dalili zako una chango la ugonjwa, hapo utafanyiwa utrasound. Na ikionekana kuna shida, daktari atajikita zaidi kukutibu tatizo husika.

Nini cha Kufanya ili Kupunguza Maumivu ya Chango kwa Muda

Kuna njia nyingi ambazo husaidia kupunguza maumivu ya hedhi ambazo unaweza kutumia ukiwa nyumbani kwako kabla ya kwenda hospitali. Kama maumivu ni makali sana unaweza:-

 • Kumeza dawa za kukata maumivu kama ibuprofen kwa ahueni ya haraka. Angalizo: dawa za maumivu isiwe ni nia ya kutumika kila mara kwani madhara yake ni makubwa kiafya, dawa hizi zitumike kwa uangalifu.
 • Tumia maji ya uvuguvugu kukandakanda mahali pa tumbo la chini
 • Epuka kuvuta sigara na kunywa pombe kipindi cha hedhi
 • Usitumie vinywaji na vyakula vyenye caffeine mfano majani ya chai na kahawa
 • Fanya masaji kwenye upande wa chini wa mgongo na sehemu ya tumbo la chini.
 • Pata muda mwingi wa kupumzika
 • Weka ratiba ya kufanya mazoezi mara kwa mara: Tafiti zinasema wanawake wanaofanya mazoezi hupunguza maumivu ya hedhi kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na wasiofanya mazoezi.

Lini natakiwa Kumwona Daktari?

Chango linapokuwa kali sana linapelekea baadhi ya wanawake washindwe kufanya kazi zao na kushindwa kwenda darasani. Huhitaji kabisa kuvumilia mateso ya namna hii, unahitaji kuishi vizuri na kufurahia maisha. Kama maumivu hayavumiliki hakikisha unaenda hospital haraka.

Jua mzunguko wako

Ni muhimu sana kujua mzunguko wako, pia ujue maumivu huwa yanaanza siku ngapi kabla ya hedhi. Kama chango linaambatana na dalili zingine mfano maumivu makali ya kichwa, bleed nzito sana na nyingi, nenda hospitali.

Je Tumbo la Chango Linapelekea Ugumba?

Kama tulivoona kwamba chango siyo ugonjwa bali ni dalili za maumivu makali ya tumbo la hedhi. Sasa kama unapata chango la kwanza (primary amenorrhea) hapo hakuna kikwazo cha kushika mimba. Lakini kama chango lako ni ile aina ya pili yani secondary amenorrhea, hapo lazima kuwe na kikwazo kushika mimba mapema.

nini ufanye kama umetafuta mimba mda mrefu bila mafanikio?

Endapo wewe na mme wako mmetafuta mimba kwa zaidi ya mwaka mmoja, nendeni hospitali wote wawili kupimwa kujua chanzo cha tatizo. Mwanamke utapima mirija, kizazi na homoni na mwanaume atapimwa mbegu kuona kama zina hitilafu.

Unahitaji ushauri na tiba? Tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254

One reply on “Maumivu ya Tumbo la Chango”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *