Kipimo cha X-rays

kipimo cha x-rays
picha ya X rays

X-rays ni kitu gani?

Kipimo cha X-rays ni kipimo maarufu sana cha kufanya uchunguzi wa afya ya binadamu kupitia picha. Ni kipimo ambacho kimekuwa kikitumika kwa miongo mingi sasa kugundua tatizo kwa kupiga picha eneo la ndani la mwili bila hata kufanya upasuaji.

Kuna aina tofauti za X-rays kulingana na matumizi tofauti. Mfano X-rays kwa ajili ya kupima matiti huitwa mommogram. Kuna hatari kadhaa kutokana na kipimo hichi cha X-ray. Lakini kwa wagonjwa wengi, faida za kipimo huwa ni kubwa zaidi ukilinganisha na madhara watakayopata.

Kwanini ufanyiwe kipimo cha X-rays?

Daktari anaweza kupendekeza ufanyiwe kipimo cha X-rays kwa ajili ya

 • kupima eneo unalojisikia maumivu
 • kufatilia maendeleo ya tatizo linalokusumbua mfano changamoto ya joints kulika (osteoporosis) na
 • kufatilia ufanisi wa dawa ulizopatiwa

Baadhi ya changamoto zinazohitaji ufanyiwe X-rays ni pamoja na

 • saratani ya mifupa
 • uvimbe kwenye matiti
 • moyo kutanuka
 • kuziba kwa mirija ya damu
 • changamoto za mapafu
 • changamoto kwenye mfumo wa chakula
 • kuvunjika mifupa
 • kuoza meno na
 • kufatilia kitu kilichomezwa

Maandalizi kabla ya kufanyiwa X-rays

Kulingana na eneo la mwili ambapo unatakiwa kupimwa, daktari atapendekeza uvae gauni la hospitali. Pia unaweza kushauriwa kuondoa vito vyote ulivyovaa, kama saa, pete ama mkufu. Vito hivi vinaweza kuingiliana na upimaji na kuharibu ubora wa picha.

Hakikisha unamwelezea daktari ama mtaalamu wa mionzi kama una kifaa cha chuma kilichpandikizwa ndani ya mwili, mfano pacemaker au risasi. Vitu hivi vinaweza kuzuia kusafiri kwa mionzi na hivo kupunguza ufanisi wa kipimo.

Kimiminika(dye)

Katika mazingira fulani ya kipimo, daktari anaweza kupendekeza umeze kimiminika (contrast dye) ambacho kitasaidia kuongeza ubora wa picha. Kimiminika hiki kinaweza kuwa cha kunywa, kudungwa sindano ama kuingizwa kupitia njia ya haja kubwa.

Kama unatarajia kufanyiwa X rays kwa ajili ya kucheki mfumo wa chakula, daktari anaweza kukushauri kufunga kula kwa muda fulani kuelekea muda wa kipimo. Utahitajika kutokula chochote kwenye funga yako. Pia katika mazingira fulani daktari anaweza kukupatia dawa ili kusafisha kwanza utumbo.

Jinsi gani kipimo cha x-rays kinafanyika?

Baada ya kuandaliwa vizuri, mtaalamu wa mionzi atakulaza kwa namna ambayo itatoa picha nzuri wakati wa kipimo. Unaweza kujulishwa kulala, kukaa ama kusimama kwa kutegemeana na aina ya upimaji. Mtaalamu atapitisha camera mbele ya eneo linalopimwa, huku nyuma yake kukiwa na kisahani maalamu kinachokamata picha za kiungo.

Ni muhimu kukaa kwa kutulia wakati kipimo kinaendelea ili kutoathiri ubora wa picha.

Je kuna madhara gani ya kipimo cha X-rays

Kipimo cha X-ray hutumia kiwango kidogo cha mionzi ili kuzalisha picha ya kiungo husika cha mwili kinachopimwa. Kiwango cha mionzi kinachotumika kinakuwa salama kwa mtu mzima ila siyo kwa mtoto mchanga. Kama una mimba ama unahisi una mimba, mjulishe daktari kabla ya kipimo. Daktari anaweza kupendekeza kipimo kingine mfano MRI.

Endapo kama unafanya kipimo kucheki mfupa uliovunjika, unaweza kuhisi maumivu wakati mionzi inapenya kwenye mwili. Daktari anaweza kupendekeza umeze dawa ya kupunguza maumivu kabla ya kipimo.

Kama umemeza kimiminika cha kuongeza ubora wa picha, unaweza kupata dalili za

 • muwasho
 • kichefuchefu
 • kichwa kuwa chepesi na
 • kubadilika kwa ladha ya mdomo

Baada ya kipimo cha X-rays

Baada ya kipimo cha x-ray, unaweza kubadili nguo na kuvaa zile za kwako. Kulingana na hali ya afya yako, daktari anaweza kukushauri upumzike ama uendelee tu na shughuli zako kama kawaida.Matokeo ya vipimo utayapata baada ya siku chache.

Mtaalamu wa mionzi atandaadaa ripoti na kumpatia daktari, kisha daktari anaweza kupendekeza vipimo zaidi. Mfano kipimo cha damu ama X ray ingine inaweza kupendekezwa kabla ya kukweleza mpango wa tiba.

Bofya kusoma kuhusu kipimo cha MRI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *