Faida za beetroot kwa mjamzito

faida za beetroot kwa mjamzito
beetroot

Beetroot kama jina lake lilivyo ni chakula kilichopo kwenye kundi la mizizi, kama ilivyo kwa viazi na mihogo. Beetroot ni chakula na wakati mwingine yaweza kuwa matunda, kulingana tu na namna unavotengeneza na kutumia. Hapa chini ni maelezo ya faida lukuki za beetroot kwa mjamzito

1.Kuimarisha usagaji wa chakula

Wakati wa ujauzito kutokana na ongezeko la homoni za estrogen na progesterone, inaweza kupelekea kukosa choo na kupta choo kigumu. Beetroot itakusaidia kurekebisha tumbo la chakula uanze kupata choo vizuri kwasababu ni matunda yenye fibers/kambakamba kwa wingi.

2.Beetroot zitakusaidia kuzuia changamoto za uumbaji kwa mtoto(neural tube defects)

Beetroot ni chanzo kizuri cha folate au folic acid. Kwa mujibu wa shirika la afya duniani mjamzito anatakiwa kupata kiwango cha folic acid kisichopungua microgram 400 kila siku.

Kama una historia ya mimba kuharibika unahitaji kupata kiwango zaidi ya folate. Ni vigumu kupata kiwango chote cha folate kwenye vyakula. Kwahivo pamoja na kula beetroot, hakikisha unatumia na vidonge vya folic acid ulivyopewa hospitali.

3.Beetroot zinaweza kusaidia kuimarisha ukuaji wa mtoto.

Changamoto za mtoto kushindwa kuendelea kukua tumboni, husababishwa hasa na matatizo kwenye kondo la nyuma(placenta) Mzunguko wa damu kwenye kondo la nyuma unaweza kuimarishwa kwa madini ya nitrate yaliyopo kwenye beetroot.

4.Beetroot zinapunguza hatari ya kifafa cha mimba(preeclampsia)

Kifafa cha mimba hutokana na kuongezeka kwa shinikizo la damu kupita kaisi kwa mjamzito. Tafiti zinasema kwamba kula beetroot kunasaidia kurekebisha shinikizo la damu na kumlinda mjamzito dhidi ya kifafa cha mimba.

5.Kurekebisha uzito

Beetroot zina vitamin C kwa wingi, madini ya potasium, folate, manganese na madini chuma, pamoja na fibers/kambakamba. Unapokula au kunywa juisi ya beetroot, inakufanya uwe umeshiba muda mwingi na hivo kuzuia kula kila mara hadi kunenepa kupita kias.

Jinsi ya kuandaa beetroot

Baada ya kunua beetroot sokoni au kwenye genge la karibu yako, zioshe kwa maji ya kawiada kuondoa tope. Kisha osha tena kwa maji yenye apple vinegar kuua bakteria wabaya.

Kurosti: Unaweza kusrosti beetroot kwa kuzifunga kwenye foil, kisha ziweke kwenye oven kwa dakika 40. Badaa ya hapo ipua na umenye taratibu kuondoa maganda, tayari kwa kuliwa. Unaweza pia kuweka kwenye microwave kwa dakika 15.

Juisi: Kama una juicer au blender nyumbani kwako, unaweza kusaga na kunywa jusi ya beetroot. Osha na umenye beetroot kisha zikate vipate vidogo.
Chukua chungwa likate, kamua maji yake na uchanganye kwenye blender. Kisha saga kwa sipidi. Baada ya hapo unaweza kuchuja na kunywa. Badala ya chungwa unaweza kutumia apple ili kuleta ladha nzuri.

Bofya kusoma kuhusu: Dalili mbaya kwa mjamzito ambazo hutakiwi kupuuza