Upasuaji Kuondoa Kizazi(hysterectomy)

upasuaji kuondoa kizazi (hysterectomy)
kizazi

Nini maana ya kuondoa kizazi (hysterectomy)?

Kun’goa ama kuondoa kizazi kitaalamu hysterectomy ni upasuaji unaofanyika kuondoa sehemu zinazounda kizazi kwa mwanamke. Upasuaji huu unaweza kugawanyika katika makundi matatu

Partial hysterectomy-ambapo tumbo la uzazi linaondolewa huku mirija ya uzazi na mifuko ya mayai ikibaki
Standard hysterectomy– ambapo tumbo la uzazi na mlango wa kizazi vinaondolewa na
Total hysterectomy– ambapo viungo vyote vya uzazi yani mlango wa kizazi, tumbo la uzazi, mirija ya uzazi na mifuko ya mayai vinaondolewa vyote.

Upasuaji kuondoa kizazi unaweza kufanya kupitia kwenye uke ama kupitia eneo la tumbo. Njia yoyote ambayo daktari ataamua kuitumia inachangia pakubwa katika matokeo yatakayojitokeza baada ya upasuaji.
Soma hapa chini kujua zaidi kuhusu madhara ya kuondoa kizazi

Madhara ya muda mfupi ya kuondoa kizazi

Madhara kwenye viungo vya mwili(physical effects)
Bada ya upasuaji kutoa kizazi utatakiwa kukaa hospitali kwa siku mpaka mbili. Wakati upo hospitali utapatiwa dawa mbalimbali kupunguza maumivu kadiri mwili unavopoa.

Kadiri unavozidi kupona mshono wako utapata bleed nyepesi kwa siku kadhaa baada ya upasuaji. Hii ni kawaida kabisa, unaweza kuvaa pedi wakati huu kuvyonza damu na kuwa mkavu.

Inachukua muda gani kupona kabisa?

Iategemea na aina ya upasuaji uliofanyiwa na afya ya mwili wako kiujumla. Wanawake wengi wanaweza kurejea katika hali ya kawaida baada ya wiki sita baada ya upasuaji kuondoa kizazi.

Kama upasuaji wako ulifanyika kupitia njia ya uke utapona mapema zaidi ndani ya wiki tatu baada ya upasuaji. Salili hizi utaziona wiki chache baada ya kufanyiwa upasuaji

 • maumivu kwenye mshono
 • kuvimba na kuwa na wekundu kwenye mshono
 • hali ya kuungua na kuwasha kwenye mshono
 • kupata ganzi eneo la miguuni

Fahamu kwamba kama ulifanyiwa upasuaji wa kuondoa kizazi chote, utaanza menopause ndani ya muda mfupi. Yaani utakoma hedhi kabisa, na utaanza kuona dalili hizi

Madhara ya kihisia baada ya Kundoa Kizazi

Kizazi ni kiungo muhimu sana katika kushika mimba na kuzaa. Kuondolewa kizazi maana yake hutaweza tena kushika mimba wala kuzaa katika maisha yako. Huu ni wakati mgumu sana kwa wanawake waliopitia hali hii, ni ngumu kuzoea inachukua muda sana kuikubali hali hii.

Kwa baadhi ya wanawake kupata hedhi na kushika mimba ni kashiria kikubwa cha uanawake wao. Kuvikosa hivi vitu maana yake ni kama kupoteza utu wao. Msongo wa mawazo unaokuja baada ya hapo ni mkubwa.

Ni yapi Madhara ya muda mrefu Kuondoa Kizazi?

Baada ya upasuaji maana yake hutaweza tena kupata hedhi. Pia hutaweza kushika tena mimba. Haya ndio matokeo ya muda mrefu ya upasuaji kuondoa kizazi chote.

Kuhama kwa viungo vya mwili ni madhara mengine yanayoweza kujitokeza, kwa mfano,uke unaweza kushuka chini sana kwasababu haujaunganishwa tena na tumbo la uzazi.

Viungo vingine kama kibofu cha mkojo na utumbo vinaweza kushuka chini mpaka kwenye eneo kizazi kilipokuwa na kusukuma uke zaidi.

Wanawake wengi hawapatwi na dalili hizi za kushuka kwa viungo baada ya upasuaji. Ili kujizuia viungo kushuka kabla ya kufanyiwa upasuaji hakikisha unaanza mazoezi ya nyonga kuimarisha misuli. Mazoezi kama ya kegel yanaweza kufanywa popote.

Je kuna hatari yoyote kwenye afya yako baada ya kuondoa kizazi?

Kuondoa kizazi ni upasuaji mkubwa. Kama ilivo kwa upasuaji mwingine mkubwa unaweza kuleta hatari kama

 • kupoteza damu nyingi
 • majeraha kwenye viungo vya karibu kama kibofu, neva na mishipa ya damu
 • kugada kwa damu
 • kuziba kwa njia ya choo na
 • kupata maambukizi

Matatzo haya makubwa yanaweza kumpata mgonjwa yoyote wakati wa upasuaji mkubwa na wala siyo tu kwa habari ya kutolewa kizazi. Daktari atakweleza kila kitu kabla ya upasuaji na atakushauri njia gani ni sahihi kwa upande wako ili kupunguza kujitokeza kwa haya matatizo .

Nini cha Kumuuliza Daktari Kabla ya kuondolewa kizazi?

Daktari mzuri atatenga muda kukusikiliza maswali na dukuduku lako kuhusu upasuaji wa kuondoa kizazi. Haya ni maswali ya muhimu unayotakiwa kumuuliza daktari kabla ya kufanyiwa upasuaji

 1. Je kuna tiba yoyote bila upasuaji inayoweza kuwa mbadala wa upasuaji?
 2. Unapendekeza aina gani ya upasuaji na kwanini?
 3. Kuna hatari gani itakayojitokeza endapo nikiamua kutofanyiwa upasuaji?
 4. Je mnatumia njia za kisasa kufanya upasuaji?
 5. Je kuna utafiti wowote mpya uliofanyika juu ya tatizo langu?
 6. Dawa gani unapendekeza niendelee kutumia baada ya upasuaji huu?
 7. Je ni lazima kuchomwa nusu kaputi kabla ya kupasualiwa?
 8. Baada ya upasuaji nitabaki na makaovu eneo gani la mwili?
 9. Ni muda gani nitahitaji kukaa hospitali kabla ya kuruhusiwa?
 10. Itachukua muda gani kupona na kuendelea na kazi zangu?

Mwisho kabisa, zungumza na daktari wako kabla ya upasuaji, kwa maana lazima kuna madhara yatajitokeza. Unahitaji kujua madhara haya kabla uya upasuaji ili ujiandae kuyakubali.

Kama umependezwa na huduma yetu na unahitaji kutuchangia chochote ili tuendelee kutoa zaidi elimu hii, Wasiliana nasi kupitia whatsapp namba 0678626254.

Bofya kusoma makala inayofuata kuhusu Kuvimba mlango wa kizazi