Kwanini Unalia baada ya tendo la ndoa

kulia baada ya tendo la ndoa
kulia baada ya tendo

Kama umewahi kujikuta unalia baada ya tendo la ndoa, fahamu kwamba ni jambo la kawaida na haupo peke yako. Inaweza kuwa ni machozi ya furaha, au machozi ya aibu pengine au maumivu. Kulia machozi siyo lazima iwe umefika kileleni pengine inaweza kutokea kwa mtu wa jinsia yoyote pia.

Hizi ndizo sababu 10 kwanini unalia baada ya tendo la ndoa

Furaha ya tendo la ndoa

Hisia mbalimbali wakati wa tendo naa baada zinaweza kukufanya utoe machozi na wala si jambo baya hata kidogo. Nadhani umeshaona watu wengi wakitoa machozi wakati wa kuoa au kuolewa au mama kutoa chozi baada ya kujifungua.

Furaha hiyo ndio ile ile inayokufanya nawe utoe machozi baada ya tendo la ndoa. Kama hujafanya tendo muda mrefu hisia za kulia wakati ukifanya tendo zitakuwa kali sana.

Kuzidiwa au Kufunikwa na Tendo husika

Pengine kuna jambo ulitegemea kufanyiwa na mpenzi wako na amefanya kupita kiasi hata wewe kushindwa kujitambua na kujikuta unatoa machozi tu. Yani ni kama umeshangwa zaidi na matukio ya tendo la ndoa kwa wakati huo.

Kushangazwa na mwitiko wa mwili wako

Hii inatokea sana kwa wanawake ambao hawakuwahi kufika kileleni hata mara moja, inapotokea amepata mpenzi wa kumkuna vizuri hapo ataishia kulia na kutoa machozi ya furaha kwa kushangazwa na namna mwili ulivoitika .

Lakini pia unaweza kulia kwa kushindwa kufaya tendo inavotakwa kiasi ya kusngazwa na mwitikio wa mwili wako, mfano kwa mwanamke kukosa hisia kabisa kwa mme wake na hivo kutofurahia tendo.

Mabadiliko ya kibaolojia mwilini

Wakati mwingine mwili wako unaweza kufanya jambo bila wewe kujitambua yani unajikuta tu umetokewa na hali fulani. Kwenye tendo la ndoa unaweza kujikuta umelia machozi bila sababu yoyote kutokana tu na mabadiliko ya homoni na kupelekea hisia kali sana zisizoelezeka.

Maumivu wakati wa tendo la ndoa

Maumivu wakati wa tendo yanaweza kukufanya ulie machozi. Kuna sababu nyingi zinazopelekea maumivu kama

Weka appointment na daktari endapo unapata maumivu wakati wa tendo ili kupata vipimo na tiba mapema.

Wasiwasi

Kulia ni kitendo mojawapo cha kupunguza mawazo, hofu na hata wasiwasi. Unapokuwa na wasiwasi ni ngumu sana kufurahia tendo. Unaweza kujikuta unapatwa na hisia mbalimbali zinazokufanya ulie machozi. Pengine wewe ni bikira na ni mara yako ya kwanza kufanya tendo, pengine una mashaka kama kweli utaweza kufanya tendo vizuri ukamridhisha mwenzako.

Aibu na kujihisi mkosaji

Kuna sababu nyingi zinazopelekea ujione mkosaji na aibu baada ya tendo na kukufanya ulie machozi. Pengine mzazi alikushauri usifanye tendo kabla ya kuolewa na umefanya. Unaanza kuhisi umekosea sana, au pengine umechepuka na kwenda kufanya ngono na mtu mwingine, kisha majuto na aibu inakujia baada ya hapo na kukufanya ulie. Au pengine umesahau kutumia kondomu na humuamini mwenzi wako hiyo inakufanya utoe machozi kwa kujutia.

Kuchanganyikiwa

Pengine kuna mambo mpenzi wako amekufanyia wakati wa tendo na wewe hukuyataka kabisa. Mfano hupendi ngono kinyume na maumbile lakini mpenzi wako anajaribu kufanya hivo katikati ya tendo, baada ya kumaliza utaanza kumtafakari na kushindwa kumpatia majibu na inakufanya ulie machozi.

Sonona

Kama ukijikuta unalia kila mara baada ya tendo inaweza kuwa kiashiria cha depression/sonona au tatizo lingine la kiafya. Dalili zingine za sonona ni kama

  • hasira
  • wasiwasi
  • kufura kila mara
  • kukosa umakini katika jambo
  • mabadiliko ya hamu ya kula
  • kukosa hamu ya tendo la ndoa

Maumivu ya zamani

Kama wewe ni muhanga wa unyanyasaji wowote hasa wa kingono, unapokutana na mpenzi mpya utaanza kukumbuka mambo ya zamani na kukupelekea ulie machozi. Pengine uliwahi kubakwa ukiwa mdogo, au ulidhalilishwa kwa namna yoyote kama kulazimishwa ngono na mtu mzima au ndugu yako kukutaka kimapenzi nk.

Nini cha Kufanya Pale Unapolia Baada ya tendo

Kwa maumivu ukeni baada ya tendo muhimu umwone daktari akufanyie vipimo kujua chanzo cha tatizo. Zaidi ya hapo fatilia na chanzo cha machozi yako, kwanini umelia je
Ni machozi mengine au ni machozi kidogo tu
Machozi ni ya kihisia ?
Nini kilikuwa kinaendelea akili mwako wakati unalia?
Je umelia sababu ya mahusiano yako au tukio la zamani?
Je baada ya kulia umejisikia nafuu au bado?

Kama kulia kwako ni kwasababu ya mahusiano yaliyopo basi huna haja ya kuwa na wasiwasi, fanya yafuatayo

  • jipe muda zaidi
  • ongea na mpenzi wako kama kuna jambo lolote msuluhishe mapema
  • zungumzeni kuhusu tendo la ndoa, kitu gani unapendelea na kipi hupendi kufanyiwa.

Kama mpenzi wao analia kila mara baada ya tendo, ongea nae kwa upole, muulize shida iko wapi, muulize kama kuna kitu unaweza kusaidia ili kuondoa machungu yake, usimgombeze hata kidogo, mbembeleze uliza taratibu kama kuna kitu umemkwaza.

Bofya kusoma makala inayofuata: Kuhusu kina cha uke wako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *