Categories
Afya ya mwanamke na uzazi

Fahamu Kina cha Uke

kina sahihi cha uke wako
uke

Ni kipi kina cha uke ambacho ni sahihi?

Kuna imani potofu nyingi sana kuhusu maumbile, kina cha uke wako na namna ya kutunza afya ya uke. Baadhi ya watu wanafikiri uke ni mrefu kuelekea tumbo la chakula.

Kama na wewe umekuwa ukijiuliza maswali mengi kuhusu afya na maumbile ya uke wako, endelea kusoma makala hii utapata majibu yote.

1.Uke wako una urefu kiasi gani?

Uke wako siyo mrefu kihivyo kama unavowaza. Kikawaida urefu wa uke kuelekea ndani ni nchi tatu mpaka 6. Ni sawa na urefu wa mkono wako. Kina cha uke kinaweza pia kubadilika katika nyakati tofauti mfano wakati wa tendo la ndoa na kipindi cha kujifungua.

2.Je kina cha uke wako kinaongezeka ukiwa na hisia za kimapenzi?

Wakati wa tendo la ndoa, mwili huamshwa na hisia za mapenzi na hivo kupelekea kina cha uke kuongezeka ili kuruhusu uume kuingia vizuri.
Hisia za mapenzi hufanya shingo ya kizazi na kizazi kupanda juu kidogo na hio nafasi hiyo kuchukuliwa na uke.

Kama unahisi uume umeingia na unagusa shingo ya kizazi, inawezekana kabisa hujaandaliwa vizuri na haupo tayari kuingiziwa uume. Japo hii siyo sababu pekee ya kuguswa kizazi. Sababu ingine yaweza kuwa ni urefu kupita kiasi wa uume , zaidi ya inch 5.

Unataka kujifunza namna ya kupima urefu wa uume? bofya hapa kusoma zaidi

3.Uke unawezaje kutanuka wakati wa kuzaa?

Wakati wa kujifungua misuli ya uke wako inaweza kutanuka mpaka mwisho wake, kuruhusu mtoto kuzaliwa. Baadhi ya wanawake waliozaa kwa njia ya uke huona mabadilko. Mabadiliko kama kuhisi uke ni mpana kuliko kawaida baada ya kuzaa.

Baada ya kuzaa uke wako unatakiwa kurejea hali ya mwanzo baada ya siku chache. Japo uke uke wako hautarudi kwa asilimia mia kama mwanzo ila misuli itajikaza na utaweza tena kufurahia tendo.

4.Kuna haja ya kufanya mazoezi kukaza misuli ya uke?

Kadiri umri unazoenda, misuli ya uke wako itaanza kulegea kutokana na sababu mbali mbali kama

  • Kujifungua
  • Upasuaji
  • Kujikaza wakati wa kukohoa na kutoa choo
  • kuongezeka uzito

Mazoezi ya kegel yatakuzaidia kukaza misuli ya ndani ambayo inashikilia uke, kibofu, kizazi , na utumbo. Mazoezi ya kegel pia yatakusaidia kuongeza uwezo wa kubana mkojo na kuzuia kutokwa na mkojo na kinyesi bila kujitambua.

5.Je kisimi hubadilika ukubwa na kuvimba?

Jibu ni ndio! Unapokuwa kwenye hisia za mapenzi, kisimi chako ama kinembe huvimba na kuongezeka ukubwa. Hii ni kutokana na kuongezeka kwa mzunguko wa damu kuelekea kwenye via vya uzazi.

6.Je wanawake wote wanafanana maumbile ya uke?

Jibu ni hapana. Maumbile ya uke, mashavu ya uke, na urefu wa kuma unatofautiana kwa kila mwanamke. Uke wako unaweza kuwa mweusi kuliko maeneo mengine ya mwili, kisimi chako chaweza kuwa kidogo na hiyo ni kawaida, usijilinganishe na mwanamke mwingine.

7.Kwanini rangi ya ngozi chini kwenye uke ni nyeusi zaidi?

Ni kawaida kabisa kwa maeneo ya huko chini kuwa na rangi nyeusi zaidi kuliko maeneo mengine ya mwili. Mfano baadhi ya wanawake huwa na mashavu ya uke ya brown na wengi rangi nyeusi, wengine ya pink. Kama unahofu na rangi ya uke wako muone daktari mapema.

8.Je kuna faida yoyote ya mavuzi?

Kuwa na kutokuwa na nywele zehemu za siri hakuna athari yoyote kwa afya ya uke. Ila tu kuna changamoto unaweza kupata kwa kunyoa mavuzi kulingana na aina ya kifaa ulichotumia. Unaweza kupata muwasho na malengelenge.

9.Je ni salama kuosha uke mpaka ndani kwa maji?

Japo kitendo hichi ni maarufu sana kama kuflush uke au douching, madaktari wanapendekeza usijizoeshe kuosha uke kwa namna hii. Kuosha uke mpaka ndani kunaondoa na bakteria wazuri na hivo kukuweka katika hatari ya kutokwa na harufu mbaya na kuugua fangasi.

10.Je harufu ya uke inatofautiana kila siku kwenye mzunguko?

Najua waweza kuwa unashtuka sana na kupata hofu pale unapopata harufu fulani ukeni. Ni kawaida kabisa uke kuwa na harufu. Mfano unaweza kuona mabadiliko ya harufu baada ya kula samaki, tangawizi au kutumia virutibisho fulani.

Kama harufu ni mbaya sana na imekutoka kwa siku nyingi, harufu pengine inaabatana na uchafu wa kijani. Hapo muone daktari mapema. Dalili hizi zaweza kuashiria maambukizi ya bakteria na magonjwa ya zinaa

Unahitaji maoni na Ushauri? Tuandikie kwa Whatsapp namba 0678626254. Usipige simu namba ni ya whatsapp tu

Bofya kusoma makala inayofuata: Faida na hasara za uzazi wa mpango

16 replies on “Fahamu Kina cha Uke”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *