Categories
Hedhi salama Siku za hatari

Kumeza P2, Maswali na Majibu

vidonge vya p2
vidonge vya p2 kuzuia mimba

Nini Kinatokea P2 isipofanya kazi?

P2 ni vidonge vya kumeza kwa dharula tu ili kuzuia mimba isiyotarajiwa endapo hukutumia kinga. Lakini unaweza kuwa unajiuliza je kuna uhakika gani kama p2 zinakusaidia kuzuia mimba? Uwezo wake ni asilimia ngapi? Na vipi kama haitafanya kazi nini kitatokea?

Hapa chini kuna majibu ya maswali yako yote kuhusu p2 kutoka kwa watalamu na wabobezi wa afya ya uzazi. Tusome zaidi.

Je unaweza kushika mimba hata baada ya kumeza p2?

P2 ama morning after pill au plan B, ni dawa zilizopo kwenye kundi la levonorgestrel. Ambazo kazi yake ni kuzuia usishike mimba baada ya tendo endapo umesahau kinga, au kondomu imepasuka au ulifanya tendo ukiwa umelewa.

Dawa zinafanya kazi kwa kuzuia yai kutolewa kwenye ovary wakati wa ovulation, na hivo kuzuia mbegu na yai zisikutane kufanye kiumbe.

Muda sahihi wa kumeza p2 ni upi?

Kumbuka mbegu inapoingia kwenye uke inachukua saa 12 mpaka 48 kwenda kurutubisha yai. Na dawa inafanya kazi vizuri endapo utameza ndani ya masaa 12 baada ya kufanya tendo. Ukimeza ndani ya masaa 24 chansi ya kuzuia mimba ni asilimia 95 na zaidi.

Ukimeza kuanzia masaa 48 mpaka 72, yani siku 2 mpaka 3 baada ya kufanya tendo, chansi ya kuzuia mimba inapunguza mpaka asilimia 61 pekee. Kumbe sasa uwezekano wa kushika mimba hata kama ulimeza p2 unaongezeka kadiri unavochelewa kumeza kidonge.

Dalili gani nitapata baada ya kumeza p2?

Baada ya kumeza p2 tegemea kupata dalili ama side effects kama

  • kichefuchefu
  • maumivu ya tumbo
  • kichwa kuuma
  • kizunguzungu na
  • kutapika

Kama utatapika ndani ya masaa mawili bada ya kumeza dawa, unatakiwa umeze tena kidonge kingine ama utumie njia ingine ya kuzuia mimba kama condom.

Je uzito mkubwa na kitambi ni kikwazo cha p2 kufanya kazi?

Jibu ni ndio, tafiti zinaonesha kwamba wanawake wenye uzito mkubwa na kitambi wapo kwenye hatari ya kushika mimba hata kama wametumia p2 vizuri. Inashauri kama wewe ni mnene tumia kitanzi cha copper kama njia ya kisasa kuzuia mimba.

Dawa Zinapelekea P2 isifanye Kazi

Ni muhimu pia kujua kwamba baadhi ya dawa zinaweza kuathiri utendaji wa P2. Dawa kama za fungus, HIV, dawa za kifafa na baadhi ya antibiotic,. Sasa unapoenda dukani kununua P2, hakikisha unamweleza muhudumu hali yako ya kiafya na dawa unazotumia kwa muda huo.

Je p2 zinafanya kazi kwenye ovulation?

Dawa za p2 zinafanya kazi vizuri kabla ya ovulation, yani kabla yai halijatolewa. Hii ni kwasababu inazuia kabisa yai kutolewa kwenye ovari na hivo kuzuia urutubishaji.

Lakini hata kama yai limeshatolewa, kidonge kinazuia mbegu kulifikia yai, kwa kufanya ute wa ukeni uwe mzito sana kiasi mbegu zinashindwa kuogelea.

Kama pengine umechelewa kumeza kidonge, na tayari yai limerutubishwa, basi kidonge kinazuia kiumbe kujishikiza kwenye ukuta wa kizazi na hivo mimba haitakuwepo.

Je kuna madhara kwa mjamzito kumeza P2?

Ni muhimu pia kujua kwamba, endapo umemeza kidonge bahati mbaya bila kujua kumbe kuna mimba, haitakuwa na madhara. Kiumbe kitaendelea kukua pasipo shida.

Maelezo ya Mwisho Kuhusu P2

Meza p2 kwa emergency tu na siyo kila siku. P2 ziapelekea hedhi kuvurugika na homoni kuvurugika. Tumia kwa tahadhari na usizoee kuzimeza kila siku.

Endapo unatafuta njia ya kupanga uzazi ya mda mrefu, tafadhali tembelea hospitali uonane na muhudumu akupe maelekezo.

Kwa ushauri zaidi na tiba tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254

Soma hapa ikiwa hedhi yako Imevurugika na unataka kuiweka sawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *