Dawa ya Azuma/azithromycin

Dawa ya azuma au azithromycin ipo kwenye kundi la dawa za antibiotics. Yatumika kutibu magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na bakteria. Magonjwa kama UTI, homa ya mapafu, maambukizi kwenye koo na pua.

Dawa inafanya kazi kwa kuzuia kuenea kwa bakteria. Azuma haitafanya kazi kwa maambukizi ya virusi mfano mafua. Kumbuka matumizi ya azuma yasiyo ya lazima hupelekea usugu wa dawa.

Jinsi ya kutumia azuma

Kabla hujaanza kutumia dawa, muhimu usome karatasi ya maelekezo inayokuja na dawa. Kama una maswali, muulize daktari au mfamasia anayekuhudumia mapema.

Meza dawa kama ulivyoelekezwa na daktari. Mara nyingi matumizi ni mara moja kwa siku kabla au baada ya kula. Dozi ya dawa itategemea na aina ya tatizo lako na historia ya kuumwa.

Zingatia masaa ya kumeza dawa

Kwa dawa kufanya kazi vizuri, hakikisha unameza dawa muda ule ule kila siku. Meza dawa saa kamili ili upate kukumbuka vizuri, mfano saa 4 kamili asubuhi kila siku.

Endelea kumeza dawa mpaka umalize dozi kwa jinsi daktari alivyokwandikia. Kuacha dozi katikati itafanya bakteria waendelee kukua na kukushambulia zaidi kwa siku zijazo.

Mwingiliano wa azuma na dawa zingine

Dawa za kupunguza acid maarufu kwa jina antiacids zina madini ya alminium na magnesium ambayo yanapunguza uwezo wa mwili kunfyonza daw aya azuma, endapo utameza kwa pamoja. Subiri walau masaa mawili baada au kabla ya kumeza azuma, endapo upo kwenye dozi ya antiacids.

Madhara/ matokeo ya dawa ya azuma

Mgonjwa anayetumia azuma anaweza kupata dalili za tumbo kuvurugika, kuharisha au choo kilaini, kichefuchefu, kutapika na maumivu ya tumbo. Kama dalili zitaendelea bila kukoma mjulishe daktari mapema.

Kumbuka kwamba daktari amependekeza utumie dawa hii kwasababu amejiridhisha faida utakazopata ni kubwa kuliko madhara. Wagonjwa wengi wakitumia dawa ya azuma hawapati madhara makubwa.

Mjulishe daktari endapo utaanza kupata dalili zingine mbaya zaidi kama kutosikia vizuri, matatizo ya kuona, ugumu wa kuongea na kumeza, misuli kulegea, dalili za ini kuathirika kama kutapika mfululizo, maumivu makali ya tumbo na ngozi kuwa ya njano.

Tahadhari kabla ya kuanza kutumia azuma

Kabla ya kuanza kutumia azuma, mjulishe daktari au mfamasia endapo una aleji na dawa, au aleji ya antibiotics zozote kama erythromycin; au kama una aleji ya kitu chochote

Kabla ya kuanza dawa, mjulishe daktari historia ya magonjwa yote yanayokusumbua hasa magonjwa ya ini, figo na misuli.

Mabadiliko ya mapigo ya moyo

Azuma/azithromycin inaweza kuleta mabadiliko kwenye mwenendo wa mapigo ya moyo. Dalili kama kupoteza fahamu na usingizi kupita kiasi zinahitaji uangalizi haraka wa hospitali.

Hatari ya kubadilika kwa mapigo ya moyo inaongezeka endapo una magonjwa mengine ya moyo yanayokusumbua kwa muda mrefu. Mjulishe daktari mapema historia yako, hasa kama una magonjwa ya moyo.

Kiwango kidogo cha madini ya potasssium au magnesium kwenye damu inaongeza hatari ya kuathirika mapigo ya koyo. Dawa za kutoa mkojo mwingi kwa haraka (diuretics) zinafanya madini haya kupungua.

Pia kama una changamoto ya kutokwa na jasho jingi zaidi, kuharisha na kutapika sana ni chanzo cha kuishiwa madini. Zungumza na daktari vizuri kabla hujaanza kutumia azuma.

Dawa ya azuma huleta Kizunguzungu

Japo inatokea mara chache sana, azuma yaweza kukufanya upata kizunguzungu. Matumizi ya pombe na bangi wakati unaendelea na dawa itafanya hali kuwa mbaya zaidi.

Usiendeshe vyombo vya moto wakati upo kwenye dozi. Ukiwa kwenye dozi punguza matumizi ya pombe na bangi kama unatumiaga.

Kabla ya upasuaji wowote mjulishe daktari endapo upo kwenye dozi ya azuma, au dawa zozote zingine pamoja na tiba asili au virutubisho.

Kwa mjamzito, dawa itumike tu endapo kuna ulazima wa kuitumia. Na hilo utaambiwa na daktari hospitali baada ya kuchambua hali ya afya yako na kuona dawa ipi akupatie. Dawa inaweza kumuathri mtoto aliye tumboni endapo itatumika miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito.

Muhimu sana kuzingatia hili

Usichangie dozi ya azuma na mtu mwingine. Wala usitumie dawa zilizoachwa na mgonjwa mwingine. Dawa hii umepewa kwa changamoto yako ya sasa. Baada ya kupona kama dawa zimebaki zitupe, na usitumie kabisa tena kwa wakati ujao.

Bofya kusoma: Siri moja usiyoijua ya kumkojoza mwanamke kwenye tendo

13 replies on “Dawa ya Azuma/azithromycin”

Kama korodani zinakuwa zinavimba wakati ukiwa na mpenzi wako na kuanza kuuma tatizo nini?? 0622632660

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *