Kubana tumbo Baada ya Kujifungua

kubana tumbo baada ya kujifungua
mimba

Hatua 6 za kubana tumbo lako baada ya Kujifungua.

Ujauzito unaweza kuleta mabadiliko makubwa sana kwenye mwili wako ambayo mengine hutayafurahia na utahitaji kurudi kama ulivokuwa mwanzo. Baadhi ya mabadiliko hupotea baada ya kujifungua hasa ukubwa wa tumbo lakini ngozi iliyojiachia inabaki.

Ngozi imetengenezwa kwa misuli laini ambayo huvutika pale uzito unapoongezeka. Ngozi ikishavutika inaweza kuwa changamoto sana kurudi ilivokuwa mwanzo. Ni muhimu kujua kwanba inawezekana kabisa kuridia hali yako ya zamani, ila tu itachukua muda na yataka uvumilivu.

Hapa chini ni maelezo kwa hatua tano za kukusaidia kufikia malengo ya kubana tumbo baada ya kujifungua.

1.Weka ratiba ya kufanya mazoezi.(cardio exercise)

Mazoezi haya yatakusaidia kuchoma mafuta mengi kwenye tumbo lako na pia kukaza misuli ya tumbo. Jaribu kutembea kwa haraka kilomita 2 kwa siku, kuogela , kuendesha baiskeli au kukimbia walau kilomita tatu kwa siku.
Mazoezi ya mara kwa mara yatakusaidia kupunguza ngozi ya tumbo iliyozidi.

2.Kula vizuri ili Kubana Tumbo

Kula zaidi vyakula vya protein na mafuta mazuri yatakusaidia kujenga misuli imara. Mahitaji yako ya ishe yaendane na kiwago cha mazoezi unayofanya. Kula zaidi protein kutakusaidia pia hata kupata maziwa ya kutosha kwa ajili ya mto.

3.Jaribu mazoezi ya kutanua mwili(strength training)

Kujenga misuli imara, mazoezi haya ni kama pushups, kukaak chini na kusimama kwa haraka na yoga. Mazoezi haya yatakusaidia kukaza kwa viungo vya ndani na hivo kukufanya upunguze tumbo haraka.

Kama unahudhuria gym basi hakikisha unamjulisha trainer wako kwamba umetoka kujifungua hivi karibuni.

4.Kunywa maji ya kutosha

Maji yanasaidia kulainisha ngozi na kufanya iwe ya kuvutika. Mwili wako utafanya kazi zaidi unapopata maji ya kutosha. Utaweza kuchoma vizuri mafuta yaliyohifadhiwa kwenye eneo la tumbo.

5.Fanya masaji kupitia mafuta kubana tumbo

Baadhi ya mafuta kama ya lavender na almond ni mazuri katika kuondoa michrizi kwenye ngozi ya tumbo na kusaidia ngozi ya tumbo kukaza. Jaribu kuchanganya mafuta ya almond na mafuta ya jojoba au ya nazi kisha pakaa eneo la tumbo kila siku asubuhi na jioni.
Baada ya miezi kadhaa utaona mabadiliko kwa tumbo lako kuanza kupungua na kujikaza pia.

6.Jaribu kutumia baadhi ya virutubisho

Vinavyopatikana ili kukaza tumbo lako baada ya kujifungua. Hakikisha virutubisho hivi haviathiri mtoto maana bado unanyonyesha. Vitutubishi hivi viwe na vitamin C, collagen na retinoids.

Hitimisho kuhusu kubana tumbo baada ya Kujifungua

Ujauzito unabadilisha sana maumbile yako hasa eneo la tumbo. Kadiri mimba inavokuwa, ngozi nayo inatanuka. Baadaya kuzaa wanawake wengi huwa na tumbo kubwa lililojiachia.

Kama hupendelei tumbo kubwa, na unataka kurudisha urembo wako wa zamani, jaribu njia hizo hapo juu ambazo zimeleta matokeo kwa watu wengine wengi.

Unahitaji maoni na Ushauri? Tuandikie kwa Whatsapp namba 0678626254. Usipige simu namba ni ya whatsapp tu

Bofya kusoma makala inayofuata kuhusu Kitanzi na njia zingine kupanga uzazi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *