Faida za majani ya Forosadi au chai ya Raspberry

Majani chai ya Raspberry nyekundu kwa kiswahili forosadi, ni maarufu sana kwa faida zake lukuki kwa mwanamke mjamzito. Japo majani haya yanafaa pia kwa wanawake wasio wajawazito.

Baadhi ya tafiti zinasema kwamba wanawake wamekuwa wakishuhudia faida za majani ya raspberry kwenye kurekebisha changamoto za hedhi. Changamoto kama kutapika, maumivu ya kiuno na tumbo a kichefuchefu.

Tiba kwa changamoto za hedhi

Majani ya forosadi/raspberry nyekundu yana kiambatana cha fragarine. Kiambata ambacho kinasaidia kukaza misuli ya eneo la nyonga, na hivo kupunguza maumivu ya hedhi.

Japo bado hakuna mapendekezo ya kiwango sahihi unachotakiwa kutumia. Kunywa chai kidogo ya majani ya raspberry nyekundu yatakusaidia kurekebisha dalili mbaya za kwenye hedhi.

Faida za Chai ya Raspberry kwa mjamzito.

Chai ya majani ya forosadi inapendekezwa kutumika kwa mjamzito akiwa kwenye miezi mitatu ya pili na ya tatu. Wanawake wengi wajawazito wanatumia chai ya mforosadi kupungua dalili mbaya yani morning sickness kama kutapika na kichefuchefu.

Chai ya raspberry pia inafaa sana kwa kuimarisha kizazi, kuzuia damu nyingi kutoka wakati unajifungua na pia kukufanya ujifungue vizuri.

Chai ya raspberry itakusaidia kupunguza muda wa kujifungua yaani labor.
Wanawake wengi waiotumia chai ya raspberry kwa muda wa ujauzito, walichukua muda mfupi tu kujifungua yani walikaa labor kwa muda mfupi sana.

Kurahisisha kujifungua salama

Hii ni kutokana na uwepo wa kiambata cha fragarine. Kiambata ambacho husaidia kukaza misuli ya eneo la nyonga, ikiwemo misuli ya tumbo la uzazi na kufanya kitendo cha kujifungua kuwa rahisi kabisa.

Chai ya majani ya Raspberry hukupunguza changamoto za uzazi wakati wa kujifungua

Utafiti unaonesha kwamba wanawake wanaotumia chai ya raspberry, wanapunguza hatari ya mlango wa kizazi kufunguka mapema baada ya wiki 20 na kabla ya wiki 37 za ujauzito. Pia chai ya raspberry imesaidia kupunguza hatari ya mlango wa kizazi kuchelewa kufungua baada ya wiki 42 za ujauzito.

Hitimisho

Chai ya raspberry ni msaada mkubwa kwa mwanamke katika kuimarisha misuli ya kizazi na hivo kuzuia mama kujifungua kabla ya wakati. Na pia kuepusha tatizo la mama kuchelewa kujifungua muda ukishafika.

Kwa watu wengi inaonekana ni salama kunywa kikombe kimoja mpaka vitatu kwa siku cha chai ya raspberry. Kwa mjamzito asitumie zaidi ya kikombe kimoja.

Soma kuhusu faida za green tea