Categories
Uncategorized

Dalili za yai Kupevuka kwenye siku za hatari

yai kupevuka

Ikiwa unatafuta kushika mimba, kukwepa kushika mimba isiyotarajiwa au pengine unataka tu kuelewa mwenendo wa mwili wako, kuelewa mzunguko wako ni jambo la muhimu sana. Yai kupevuka kitaalamu tunaita ovulation. Ni kipindi kifupi sana lakini chenye matokeo makubwa kwa mwili wako.

Nini maana ya yai kupevuka?

Kwanza muhimu kujua ovulation ni nini? Ovulation ni kipindi katika mzunguko wa hedhi wa mwanamke ambapo yai lililokomaa linatolewa kwenye mfumo wa mayai(ovari), kwa ajili ya kufanyiwa urutubishaji na mimba ifanyike. Yai likishatolewa kwenye ovari, linaenda mpaka kwenye mrija wa uzazi, hapo yai linaweza kuishi mpaka saa 48. Endapo hakuna mbegu imerutubisha yai basi litavunjika na kutolewa nje.

Je ni Lini yai linapevuka kwenye mzunguko wa hedhi?

Hili ni swali zuri sana ambalo kila mwanamke huwa anajiuliza. yai linatolewa hasa baada ya siku 14 hedhi ilipoanza, kwa mzunguko wa siku 28.

Lakini muhimu ujue kwamba siyo kila mwanamke basi siku yake ya hatari ni ya 14. Wengine wana mzunguko mfupi zaidi mpaka siku 21 na wengine mizunguko mirefu mpaka siku 35. Endapo hujui mzunguko wako basi bofya makala hii (Jinsi ya kufatilia siku za hatari kwa mizunguko yote) usome kwanza kisha urudi kumalizia makala ya sasa.

Je ovulation inaisha baada ya masaa mangapi?

Mchakato mzima wa yai kutolewa inachukua masaa 36. Kitendo chenyewe cha yai kutoka kwenye ovari ni cha haraka, ispokuwa mabadiliko ya homoni kuelekea zoezi husika yanaanza mapema zaidi.

Ni zipi dalili za yai kupevuka?

Habari njema ni kwamba mwili wa mwanamke unatoa viashiria vingi kuonesha kwamba hizi ni siku za hatari na yai limevevuka tayari kwa kurutubishwa. Siyo kila mtu atapata dalili hizi zote, lakini lazima kuna dalili kadhaa utaziona endapo utausikiliza mwili vizuri. Kwahivo usijione mnyonge na kuhisi yai halijapevuka endapo utapata dalili chache katika hizi nitakazokuelezea leo.

1.Uteute wa kuvutika

Lazima utakuwa umewahi kusikia kuhusu ute wa uzazi ama ute wa ovulation, ama kuona uchafu mwembemba unaovutika kwenye chupi. Huu ndio ute unaoashiria kwamba yai limepevuka na litatolewa ndani ya masaa 24 tangu ute umeanza kutoka. Uteute huu unakuwa mwepesi kama yai, unavutika na hauna harufu.

2.Tumbo kujaa kipindi ya yai kupevuka

Yawezekana umewahi kuhisi tumbo kujaa katika siku flani katikati ya mzunguko wa hedhi na usijue kwanini. Mabadiliko ya homoni hasa kuongezeka kwa homoni la LH inaweza kufanya tumbo kubakiza maji na hivo kuvimba kiasi. Lakini usiogope sana hali hii ni ya masaa machache na utakuwa sawa.

3.Kichefuchefu kwenye siku za yai kupevuka

Unaweza kupata hali ya kuhisi kichefuchefu ukiwa kwenye siku ya ovulation, hii pia ni kutokana tu na mabadiliko ya homoni. Endapo utapata na hali hii, jaribu kutembea nje upate hewa safi na utafune tangawizi.

4.Mabadiliko ya joto la mwili kipindi cha cha yai kupevuka

Kwenye siku za hatari, hasa siku yenyewe yai linapotolewa, joto la mwili huongezeka kidogo kwa centigrade 0.3. Unaweza kununua kipimajoto pharmacy ukajipima mwenyewe nyumbani na kuona mbadiliko haya.

5.Maumivu ya tumbo upande mmoja, kutokwa na matone ya damu

Je wafahamu kwamba unaweza kupata maumivu kipindi cha yai kutolewa? Maumivu haya yanatokana na kitendo cha yai kutoka kwenye kikonyo chake ambacho ni mfumo wa mayai(ovari). Kitendo hiki pia chaweza kupelekea damu itoke kwenywe kovu na hivo ukaona matone kidogo kwenye chupi. Kuanzia sasa endapo utaona damu kidogo katikati ya mzunguko basi usiogope, jua tu kwamba ni yai linatolewa.

Ni muda gani sahihi kufanya tendo endapo unatafuta mimba kwa mda mrefu bila mafanikio?

Pengine sasa unajiuliza wewe na mwenzi wako mkutane lini ili kuongeza chansi ya kupata mimba haraka? Siku nzuri na yenye chansi kubwa kupata mimba ni siku ambapo yai limetolewa na masaa 24 yanayofuatia. Na pia siku 5 kabla ya yai kutolewa.

Kwanini siku 5 kabla? kwasababu mbegu zinaweza kuishi mpaka siku 5 kwenye kizazi baada ya kufanya tendo. Kwahivo kumbe mbegu zaweza kulisubiri yai litolewe hukohuko ndani.

4 replies on “Dalili za yai Kupevuka kwenye siku za hatari”

Wow! Nice teachings.I admired to know so much about ovulation,coz i would like to get pregnant.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *