Tiba Asili Kuzibua Mirija Ya Uzazi

mirija ya uzazi

Unatahitaji tiba asili kuzibua mirija ya uzazi ushike mimba mapema? kama jibu ni ndio basi unatakiwa kusoma makala hii mpaka mwisho na kuanza kufanyia kazi maelekezo

Mbegu na Yai Hukutana Kwenye Mirija ya Uzazi

Kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke, urutubishaji wa yai au utungaji wa mimba unafanyika kwenye mirija ya uzazi. Hapa ndipo mbegu inapokutana na yai lililopevuka na kiumbe kufanyikwa. Baada ya hapo kiumbe hiki husafiri maka kwenye ukuta wa kizazi na kujipachika ili kikue.

Endapo mrija mmoja umeziba, bado chansi ya kushika mimba ipo kupitia yai kutoka upande mwingine wa mfuko wa mayai. Japo kama mirija yote ya uzazi kushoto na kulia imeziba, itakuwa ngumu kwa mwanamke kushika mimba mpaka pale mirija itakapozibuliwa.

Nini Kinasababisha Kuziba kwa Mirija ya Uzazi

Kuziba kwa mirija ya uzazi kunaweza kusababishwa na

Kama unatafuta mimba kwa muda mrefu bila mafanikio na mirija yako imeziba, unawezaje kuwa unahitaji sana tiba asili za kukusaidia kuzibua mirija yako.

Usiogope Kujaribu Tiba Asili Kuzibua Mirija

Japo watu wengi wanasifia njia hizi kuwasaidia kuzibua mirija kwa kupunguza kuvimba kwenye mirija, bado hakuna utafiti wa kisayansi unahakiki uwezo wa tiba hizi asili. Lakini usiogope kujaribu, bahati inaweza kuwa upande wako ukashika mimba mwaka huu.

1.Vitamin C.

Vitamin C ni kiondoa sumu ambacho kinapunguza mpambano(inflammation) ndani ya mwili na pia kinaimarisha kinga yako. Kwa sababu hizi pekee, vitamin C inasemekana kuwa na uwezo wa kutibu makovu na hivo kusaidia mirija yako kuzibuka.

Vitamin C inapatikana kwa wingi kwenye matunda yenye uchachu kama limau na machungwa. Lakini pia waweza kupata kwenye matunda mengine kama kiwi papai na mboga ya broccoli.

Shirika la afya duniani linapendekeza upate vitamin C kutoka kwenye vyakula zaidi, japo kuna virutubishi pia waweza kutumia vilivyo katika mfumo wa vidonge. Kumbuka kuwa mwili hauwezi kuhifadhi vitamin C, hivo watakiwa kuipata kutoka kwenye chakula au virutubishi kila siku.

2.Binzari manjano(Tumeric)

Binzari manjano inafanana sana na tangawizi. Ni moja ya chakula kikubwa katika kupunguza mpambano na kuvimba ndani ya mwili(anti-inflammatory). Kiambata hai cha Curmin ndani ya binzari manjano ndicho hufanya kazi ya kuzuia mpambano huo.

Hakuna madhara yoyote ya kutumia manjano. Japo unashauriwa kutumia kujiko kimoja tu cha manjano kwa siku, kwa kutengeneza kama chai na kuweka na viungo vingine.

Pamoja na faida nyingi za manjano kiafya, lakini bado hakuna tafiti za kina juu ya uwezo wake katika kuzibua mirija ya uzazi.

3.Tangawizi

Kiambata hai cha gingerol kilichopo wenye tangawizi, kinasaidia kupunguza mpambano na kuvimba kwenye mwili. Pamoja na faida hii hakuna utafiti wa moja kwa moja juu ya uwezo wake katika kuzibua mirija ya uzazi.

4.Kitunguu saumu

Kitunguu saumu kinafahamika kwa kuimarisha kinga ya mwili, kuzibua mirija na kutibu maambukizi ya bakeria na fangasi. Menza punye tano za Tangawizi kila siku kufurahia uponyaj wake.

5.Dong quai(female ginseng)

Ni mmea unaopatikana zaidi barani Asia. Unafahamika kwenye kutibu changamoto mbalimbali za uzazi ikiwemo kuzibua mirija. Ni moja ya tiba maarufu sana kwenye tiba asili za watu wa China.

6.Kujifukiza ukeni(Vaginal steaming)

Kujifukiza ukeni ni moja ya tiba ya kale sana inayotumika mpaka leo kutibu changamoto mbalimbali za uzazi. Yatumika zaidi kusafsha uke, kupunguza maumivu ya hedhi na kuzinua mirija. Hakuna utafiti wa kisayanasi unaokubaliana na uwezo wa tiba hii. Soma kwanza makala yake hapa kabla hujaanza kujivukiza.

7.Fertility Massage

Baadhi ya wataalamu wa tiba asili wanapendekeza masaji ya tumbo ili kuzibua mirija. Masaji hii hufanyika kwa kutumia mafuta(essential oils) kama mafuta ya rose na mafuta ya mnyonyo. Masaji ya tumbo la uzazi inasaidia kuimarisha mzunguko wa damu na kuchochea utolewaji wa sumu kwenye via vya uzazi ikiwemo mirija.

8.Maca

Maca ni mmea unaopatikana hasa Marekani ya kusini. Mmea huu unasemakana kuwa tiba ya uzazi wa mwanamke kwa kuimarisha uwezo wa kushika mimba. Tafiti zinasema mmea wa maca unasaidia kuongeza uzalishaji wa mbegu kwa mwanaume. Bado hakuna utafiti wa kisayansi kuhusu uwezo wa maca kuzibua mirija.

9.Mazoezi

Kufanya mazoezi ya viungo mara 4 kwa week inasemekana kusaidia kuzibua mirija. Tenga muda walau nusu saa ya kufanya mazoezi kila siku asubuhi au jioni.

10.Yoni Pills(Uterus Cleanisng pills)

Inasemekana kwamba vidonge hivi vya asili vya kuweka ukeni vinasaidia kusafisha kizazi na kuzibua mirija. Weka tu akili kwamba kuna aina nyingi za vidonge vya kuweka ukeni, Hakikisha umefanya utafiti wako na kujiridhisha kuhusu wa vidonge kabla ya kuvinunua. Tembelea ukurasa huu unaaminika kuuza vidonge salama vya kusafisha kizazi.

Unajuaje kama Mirija yako imeziba?

Madaktari hutumia kipimo cha hysterosalpingography(HSG), ambapo ni aina ya X-ray kucheki mirija kama imeziba.

Pia daktari anaweza kutumia kipimo cha laparascopy kucheki kama mirija imeziba. Laparascopy ni upasuaji mdogo unaofanyikwa kwa kutoboa matundu madogo eneo la tumbo, kisha kifaa kuingizwa kwenye matundu haya mpaka kwenye mirija.

Tiba ya hospitali kuzibua mirija.

Hospitali kuna tiba ya kuzibua mirija. Kipimo cha laparascopy siyo tu kinatumika kucheki kama mirija imeziba bali pia hutumika kuzibua mirija. Daktari pia anaweza kuamua kukata eneo la mirija lililoziba na kuunganisha tena mrija.

Japo tiba hizi hugharimu pesa nyingi, mafanikio yake ni makubwa sana katika kuzbua mirija iliyoziba. Kama sehemu kubwa ya mrija imepata athari, itakuwa ngumu kwa mrija huo kutibika.

Tiba Kupitia Vidonge vya UCP-Uterus cleansing pills

Kwa mwanamke mwenye changamoto ya mirija ya uzazi kujaa maji na kuziba, tunashauri atumie uterus cleansing pill kusafisha kizazi. Uterus cleansing pill (UCP) ni vidonge 2 vilivyotengenezwa kitaalamu kwa kuzingatia uasili wa dawa kutatua changamoto za wanawake kama kuziba kwa mirija ya uzazi, fangasi na PID.

Dozi moja yenye vidonge viwili vinatumika kwa wiki moja, na yatakiwa utumie dozi mbili. Kidonge kimoja kinawekwa ukeni na kutolewa baada ya siku 3, kisha unapumzika masaa 24 unaweka tena kidonge kingine.

Gharama ni Tsh 100,000/= Kwa dozi mbili.

Angalizo pale unapotumia Uterus Cleansing Pill

Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge vyenye mfanano na hivi vya UCP, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb.

Dawa haitumiki kwa wanawake bikira na wajawazito. Usifanye tendo la ndoa wakati huo upo kwenye dozi, ukianza hedhi pumzika kutumia vidonge hivi mpaka pale utakapomaliza hedhi.

Hitimisho.

Endapo njia zote hizi hazijaleta matokeo, kuna njia zingine za kisayansi unazoweza kutumia kufanikisha kubeba mimba. Njia hizi ni kama kupandikiza mimba ama IVF kwa kutumia yai lako ama yai la mwanamke mwingine. Zungumza na daktari kwa kina akushauri namna ya kupandikiza mimba.

Tunapatikana Magomeni Dar, Tuandikie kwa whatsapp no-0678626254 kuanza tiba.

8 replies on “Tiba Asili Kuzibua Mirija Ya Uzazi”

Nimesoma nimeelewa sanaa mara nyingi sana huwa nasoma ila la kufanyia massage tumbo nimeshaanza, na vitunguu saumu na tangawizi…. hsg nilifanya inaumaaaa… hapa nimeandikiwa laparascopic.. natamani hii dawa ya laki moja Mungu anipatie pesa ninunue maana kiuhalisia umri umeenda jamani nalia kila siku….

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *