Vipele ukeni na vinundu , Chanzo, Ushauri na Tiba

Kama una changamoto ya kutokewa na vipele ukeni na vinundu na kwenye mashavu ya uke, fahamu kwamba haupo peke yako. Ni tatizo kubwa na linawatokea wanawake wengi katika umri wa kuzaa. Endelea kusoma zaidi kujifunza chanzo cha tatizo lako na lini unatakiwa umwone daktari.

Muundo wa uke

Mara nyingi watu wanaposema uke , humaanisha pia eneo la nje yaani mashavu na pia eneo la ndani. Uke ni kiungo chenye misuli na tishu laini, kinachoungaisha eneo la nje la mashavu na shingo ya kizazi.

Eneo la mashavu ya uke ya Vulva linatengenezwa tishu laini zinazovutika, pamoja na tezi zinazozalisha majimaji kulainisha na kukinga uke dhidi ya athari za bakteria.

Chanzo cha vipele ukeni na vinundu

Vipele kwenye uke na mashavu ya uke inaweza kuwa ni jambo la kawaida katika mazingira fulani. Ama yaweza kuwa ni kiashiria cha ugonjwa mbaya unaohitaji tiba ya haraka. Hapa chini ni sababu kuu 7 zinazopelekea vimbe na vipele ukeni.

1.Vimbe zenye maji kwenye mashavu ya uke (Vulvar cysts)

Mashavu yako ya uke yameundwa kwa tezi mbalimbali kama tezi za mafuta na tezi za kuzalisha ute ute(Batholin’s glands). Vimbe zinaweza kufanyika kutokana na kuvimba kwa tezi hizi. Na tezi zinaweza kuvimba kutokana na kuathiriwa na vimelea kama bakteria. Vimbe nyingi za namna hii huisha zenyewe baada ya siku kadhaa.

2.Vimbe maji kwenye uke

Kuna aina nyingi za vimbe kwenye uke. Vimbe hizi zinakuwa ngumu na zinakaa kwenye kuta za uke. Vimbe mara nyingi zinakuwa na ukubwa wa mbegu ya harage na mara nyingi hufanyika baada ya kutoka kujifungua ama majereha kwenye uke.

Uvimbe kwenye kuta za uke kwa kiasi kikubwa huwa haziumi labda tu wakati wa tendo la ndoa. Vimbe hizi hutakiwa kupasuliwa hospitali na maji yake kukaushwa.

3.Chunusi ni chanzo cha vipele ukeni

Chunusi hizi za ukeni hufanana kabisa na zile za usoni. Zinakuwa na usaha kwa ndani, na mara nyingi haziumi wala kuleta shida kubwa. Chunusi za ukeni hutokea sanasana nyakati za kubalehe.

4.Kuvimba kwa mishipa ya damu (varicosities)

Asilimia 10 ya wanawake wajawazito hupata tatizo hili. Uvimbe huonekana kwa rangi kama ya bluu kwenye mashavu ya uke. Uvimbe wa mshipa wa damu unaweza usilete maumivu yoyote ila unaweza kuwasha na kutoa damu.

Vimbe nyingi za namna hii mara nyingi huisha baada ya wiki 6 mama akishajifungua. Na zinaweza kujitokeza katika mimba ijayo.

5.Unywele kuota kuelekea ndani (ingrown hair)

Baada ya kunyoa au kuuvuta unywele wa mavuzi, inaweza kutokea unywele mpya kuota kuelekea ndani ya ngozi na siyo kutoka nje ya ngozi. Kitendo hichi husababisha uvimbe na kinundu kilichojaa usaha eneo la ngozi.

Usijaribu kuchokonoa unywele ulioota kuelekea ndani kwani yaweza kuleta maambukizi. Kwa kiasi kikubwa tatizo huisha enyewe bila hata tiba. Muone daktari kama uvimbe utazidi kuwa mkubwa zaidi

6.Uvimbe kwa wanawake waliokoma hedhi (lichen sclerosus)

Uvimbe wa namna hii mara nyingi huambatana na dalili hizi kama

  • muwasho
  • ngozi nyembamba zinazongaa ambazo humeguka kirahisi
  • kutokwa damu
  • maumivu wakati wa kukojoa na wakati wa tendo
  • malengelenge yenye damu au majimaji

7.Genital warts

Warts hutokana na maambukizi ya virusi wa papiloma (HPV). Uvimbe wa namna hii waweza kusambaa kwa njia tendo. Vimbe za namna hii kwa jina lingine hutiwa vigwaru, zinakuwa na rangi nyekundu ya kung’aa. Warts huambatana na dalili za kuuma kama kuunguza na muwasho. Unaweza kusoma zaidi tatizo la warts hapa.

8.Saratani

Saratani ya mashavu ya uke inatokea kwa watu wachache sana. Pengine uvimbe wako unaweza kuashiria uwepo wa saratani. Tazama kama unapata dalili hizi

  • kutokewa na malengelenge makubwa ukeni na kwenye mashavu ya uke
  • ngozi kuwa nyeusi sanaa au nyepesi sana kuliko eneo lingine la ngozi.
  • maumivu, muwasho na hali ya kuunguza
  • malengelenge yasiyipona mapema na
  • kutokwa na damu kusiko kawaida

Lini unatakiwa kumwona daktari

Ni jambo zuri kumwona daktari pale unapoona kuna mabadiliko yasiyo ya kawaida kwenye mwili wako. Unatakiwa kumwona daktari endapo umepata uvimbe au kinundu kisochoisha mapema. Pia kama una dalili za kutokwa damu na dalili za magonjwa ya zinaa.

Tuandikie kwa namba zetu 0678626254 kupata ushauri na tiba

9 replies on “Vipele ukeni na vinundu , Chanzo, Ushauri na Tiba”

Nashukuru kwa kunielimisha mi siko na smart lakini ninakitochi umeniambia nikopi maelezo alaf nikutumie
mi niko na vipele ukeni na nikijisafisha natoka dam na xijajamiiana na mwanaume yoyote je vitaisha vyenyewe au hadi niendehosital?

Docta nashukuru sana kwa elimu hii nam cna cm kubwa ila nina tatizo la kutokwa na vipele vnavyowasha sana na nkinyoa mavuz au kwapa

mm na ujauzito wa pili sasa,lakini nimetokewa na vipele kwenye tishu na nje ya uke.awali vilikuwa vikubwa kwasasa vimekuwa vipo vidogo,huwa na washwa na ninapo fanya mapenzi mme wangu anavitoa vikiwa vimenasha kama uji kwenye uume wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *