Mimba Kutunga Nje ya Kizazi

mima kutunga nje ya kizazi
mimba nje ya kizazi

Ectopic pregnancy/Mimba kutunga nje ya kizazi ni kitu gani?
Mimba ikishatungwa kwenye mirija ya uzazi inapitia hatua zingine nyingi mpaka kwenda kujishikiza kwenye ukuta wa kizazi.

Endapo inatokea yai lililorutubishwa kukwama kwenye mirija ya uzazi na kushijikiza hapo au likajishikiza kwenye mlango wa kizazi ndipo tunaita ectopic pregnancy ama mimba nje ya kizazi.

Yai lililorutubishwa haliwezi kukua nje ya kizazi. Tafiti zinasema kwamba katika ya wanawake 50 wenye mimba mmoja kati yao anakuwa na ectopic.
Kama tatizo halitatibiwa haraka linaweza kuleta madhara makubwa kwa mwanamke na kutishia hata uwezo wa kuzaa siku za mbele.

Nini Kinasababisha Mimba Kutunga Nje ya Kizazi?

Sababu hasa ya mimba kutunga nje ya kizazi bado haijafahamika. Wataalamu wanafikiri mambo haya yanaweza kuchangia mimba kutunga nje ya kizazi

 • kuvimba na kututumka kwa mirija ya uzazi kutokana na tatizo fulani la uzazi
 • changamoto za homoni
 • matatizo ya mabadiliko ya vinasaba
 • mwanamke kuzaliwa na mapungufu kwenye kizazi
 • changamoto za kiafya zinazoathri via vya uzazi kama vimbe na kuziba kwa mirija.

Daktari atakapokufanyia vipimo anaweza kukupa sababu hasa ya changamoto yako baada ya vipimo.

Wanawake Waliopo kwenye hatari zaidi ya mimba kutunga nje ya kizazi

Wanawake wote walio katika umri wa kuzaa wapo kwenye hatari ya kushika mimba nje ya kizazi. Hatari inaongezeka zaidi kwa makundi haya

 • kushika mimba katika umri zaidi ya miaka 35
 • historia ya kufanyiwa upasuaji kwenye kizazi
 • wanawake wenye historia ya kuharibikiwa mimba nyingi hapo awali
 • kizazi kupanuka
 • Kushika mimba baada ya kufunga kizazi
 • Kushika mimba baada ya kutumia dawa nyingi za uzazi
 • kuvuta sigara
 • historia ya kuugua magonjwa ya zinaa kama kaswende na chlamydia
 • mirija kuwa miyembamba sana kiasi ya yai kushindwa kusafiri inavotakiwa.

Kama upo kwenye makundi ya wanawake hawa, zungumza na daktari atakupa mwongozo mzuri kulingana na afya yako ili upunguze hatari ya mimba kutunga nje ya kizazi.

Dalili Za mimba Kutunga Nje ya Kizazi

Kupata kichefuchefu na matiti kuuuma ni dalili kuu za kwamba una mimba, aidha mimba ya kawaida ama mimba kutunga nje ya kizazi. Lakini dalili hapa chini zinajitokeza hasa ikiwa mimba yako iko nje ya kizazi na yahitaji kwenda hospitali haraka

 • maumivu makali yanayopita kama mshale tumboni, kwenye nyonga, mabega au shingoni
 • maumivu makali sana katika upande mmoja wa tumboni
 • kutokwa damu nzito ama nyepesi wakati una mimba
 • kukosa nguvu na kuanguka
 • kujisikia mgandamizo eneo la haja kubwa

Unahitajika kumwona daktari haraka endapo utapata dalili hizi kwani zaweza kukufanya ukapoteza maisha.

Matibabu kwa Mimba iliyotungwa Nje ya Kizazi

Mimba ya nje ya kizazi siyo salama kabisa kwa mama mjamzito. Hata hivo kiumbe hakitaweza kabisa kukua nje ya kizazi. Ni muhimu kwa kiumbe hicho kuondoloewa mapema iwezekanavyo ili kulinda afya ya mama. Tiba hutofautiana kwa kulingana na wapi mimba imetunga.

Daktari anaweza kuamua kukuanzishia dawa ili kuzuia kiumbe kutopasuka na kuleta madhara zaidi.
Daktari pia anaweza kupendekeza ufanyiwe upasuaji ili kutoa kiumbe na kutibu penye tatizo. Upasuaji huu huitwa laparatomy. Wakati wa upasuaji daktari anaweza kuamua kukata mrija endapo ikionekana umeathiriwa zaidi.

Huduma Baada ya Upasuaji

Daktari atakupa maelekezo sahihi ili ujiuguze na upone mapema ukiwa nyumbani kwako. Muhimu ni kuwa msafi na kidonda kiwe kikavu. Kila siku fatilia kidonda chako na kucheki dalili zisizo za kawaida kama

 • bleed isiyokata
 • kupata harufu kali kwenye kidonda
 • kidonda kuwa chekundu na
 • kuvimba kwa mshono

Ushauri huu hapa chini ni muhimu kuzingatia ili kupona mapema mshono wako

 • usinyanyue vitu vizito
 • kunywa maji ya kutosha ili kuzuia choo kigumu na kukosa choo
 • pata muda mwingi wa kupumzika ikiwemo kuacha kufanya tendo la ndoa mapaka upone.

Siku zote ukiona kuna dalili isiyo ya kawaida mpigie simu daktari mweleze akupe uhakika kwamba ni kawaida au kuna shida.

Bofya kusoma kuhusu kuziba kwa mirija ya uzazi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *