Kukausha maziwa baada ya kuacha kunyonyesha

kukausha maziwa baada ya kuacha kunyonyesha
kunyonyesha

Kuna sababu nyingi zinazoweza kukusukuma umwachishe mtoto ziwa la mama. Kwasababu yoyote ile, kuacha kunyonyesha taratibu ni nzuri kwa afya yako na kwa afya ya mtoto pia. Kutasaidia kukausha maziwa mapema. Muda sahihi wa kuacha kunyonyesha ni pale mtoto na mama wote wanapohitaji.

Wakati mwingine waweza kulazimika kuacha kunyonyesha mapema zaidi kuliko ulivyopanga. Kuna sababu nyingi zinachangia kukauka kwa maziwa ya mama ikiwemo umri wa mtoto na kiwango cha maziwa kinachozalishwa na mwili wako.

Kukausha maziwa baada ya kuacha kunyonyesha

Baadhi ya wanawake maziwa hukauka siku chache tu baada ya kuachisha mtoto ziwa. Na kuna wengine huchukua wiki kadhaa kwa maziwa kukauka. Pia inawezekana kabisa chuchu zikaendelea kulowana kwa miezi kadhaa baada ya kuachisha mtoto ziwa.

Kumwachisha mtoto ziwa taratibu ni jambo zuri zaidi na inashauriwa hivo. Kuacha kunyonyesha kwa haraka ni hatari kwani unaweza kupata maambukizi kwenye matiti. Muhimu kuongea na daktari vizuri akupe mwongozo wa kufuata.

Njia za kukausha maziwa baada ya kuacha kunyonyesha

1.Kumwachisha mtoto ziwa haraka

Endapo ataacha kunyonyesha kwa haraka, maziwa yatapungua kuzalishwa taratibu kadiri siku zinavoenda. Yategemea pia kwa muda gani umekuwa ukinyonyesha na itachukua muda.

Endapo unapanga kumwachisha mtoto ziwa kwa haraka weka, zingatia haya

  • kuvaa bra inayoshikilia matiti vizuri
  • tumia dawa za maumivu zinazopatikana famasi kupunguza maumivu ya matiti
  • binya matiti ili kutoa maziwa yaliyozidi, itasaidia kupunguza kuvimba kwa matiti.

2.Kabeji

Majani ya kabeji yanaweza kusaidia kukausha maziwa na kupunguza kuvimba kwa matiti kama yakitumika kwa muda mrefu. Kutumia kabeji fanya haya

  • osha kebeji yako vizuri kwa maji mengi
  • chukua maganda yake na unayweke kwenye kifaa kidogo kisha weka kwenye friji.
  • weka ganda moja moja kwenye kila titi kabla ya kuvaa bra
  • badili majani ya kabeji kila baada ya masaa mawili

Majani ya kabeji yanaweza kusaidia kutibu kuvimba kwa matiti kadiri uzalishaji wa maziwa unavopungua. Pia yanaweza kutumika kipindi cha awali cha kunyonyesha endapo maziwa yanavimba.

3.Uzazi wa mpango

Vidonge vya kupanga uzazi vyenye hormone ya estrogen vinaweza kusaidia kuacha kunyonyesha. Siyo kila mwanamke ataona upungufu wa maziwa baada ya kutumia njia hii. Ongea na daktari akweleze muda mzuri wa kuanza kutumia vidonge vyenye estrogen baada ya kujifungua.

4.Vitamin Baadhi

Dozi kubwa ya vidonge vya Vitamin B-1, B-6 na B-12 vinaweza kukufanya uachiche kunyonyesha.

Njia zingine asili za kukausha maziwa

Njia hizi zimekuwa zikitumika na jamii mbali mbali kwa miaka mingi japo hazijathibitishwa kisayansi ila zinaleta matokeo.

1.Kufunga matiti

Nia hii imeanza kutumiaka miaka ya zamani ili kukausha maziwa . Njia hii inajumuisha kuyafunga matiti wa nguvu sana ili kutozalisha maziwa. Madhara ni pamoja na kuvimba matiti na kuvuta kwa maziwa, ndio maana haishauriwi sana kutumia njia hii.

2.Kupunguza maji maji

Kikawaida wanawake wanaonyesha hushauriwa kunywa maji ya kutosha ili kuzalisha maziwa mengi. Baadhi ya watu wanaamini kwamba kupunguza matumizi ya vyakula na vinjwaji vyenye maji mengi husaidia kupunguza uzalishaji wa amaziwa na hatimaye ukaachisha kunyonyesha.

3.Kushika mimba

Endapo unanyonesha na ukashika mimba, ladha ya maziwa itabadilika na pia kiwango cha maziwa kitapungua.

Muda gani inachukua maziwa kukauka baada ya kuacha kunyonyesha?

Maziwa kukauka baada ya kumwachisha mtoto kunyonya inategemea na aina ya njia uliyotumia na pia kwa muda gani umekuwa ukinyonyesha.

Hata baada ya maziwa kukauka , unaweza kuendelea kuzalisha majimaji kidogo miezi kadhaa mbele. Endapo maziwa yatarudi na kuanza kutoka, mjulishe daktari mapema, kwani waweza kuwa na tatizo la homoni.

Lini unatakiwa kumwona daktari?

Kipindi cha kuacha kunyonyesha kinaambatana na changamoto nyingi. Kama ukijisikia maumivu na dalili zingine mbaya, usisite kumuona daktari haraka.

Wakati mwingine kuziba kwa mrija wa maziwa kunatibika kwa kufanya masaji kwenye titi. Edapo umefanya hivo na hapajazibuka na unapata homa kali, nenda hospitali mapema

Tumia breast care tea kukausha maziwa yako

breast care tea kwa ajili ya afya ya matiti yako

Kazi na faida za breast care tea

  1. Kutibu shida ya kutokwa na majimaji na maziwa kwenye matiti wakati hunyonyeshi
  2. Kutibu chuchu na matiti yanayouma na kuvimba mara kwa mara
  3. Kuimarisha mzunguko wa damu kwenye matiti na kuondoa damu iliyoganda. Damu kuganda kwenye mishipa ndio chanzo kikubwa cha uvimbe kwenye matiti.
  4. Kukukinga dhidi ya changamoto za matiti kama saratani
  5. Kuzuia kujitokeza kwa saratani baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye matiti na
  6. Kuimarisha kinga ya mwili

Gharama ni Tsh 65,000/=

Wasiliana nasi kupitia whatsapp namba 0678626254 kama wahitaji tiba hii asili.