Tiba asili ya Kiungulia

kiungulia
kiungulia

Kiungulia ni moja ya changamoto inayosumbua sana ya mfumo wa chakula. Hutokea pale tindikali ya tumboni inapopanda juu mpaka mdomoni na kusababisa kuungua kwa tishu laini za koo pamoja na maumivu makali ya kifua.

Sababu nyingi zinapelekea kiugulia ikiwemo kula vyakula vinavyowasha mfano pilipili. Hapa chini ni tiba asili unazoweza kutumia ukiwa nyumbani kutibu kiungulia.

Tiba asili za kiungulia

1.Apple cider vinegar

Apple cider vinegar au siki ya matunda ya apple inasaidia kurekebisha utindikali kwenye tumbo na hivo kupunguza acid ya tumboni. Nenda supermaket au sokoni tafuta apple vinagar yenye sifa hizi

  • Organic
  • Unfiltered
  • With the mother

Matumizi ya apple vinegar kwa kiungulia

Chukua kijiko kimoja cha apple vinegar, changanya na maji ya kunywa nusu kikombe cha chai, kisha kunywa mchanganyiko huu nusu saa kabla ya kula. Fanya hivo kila uapojiandaa kula ili kutibu kiungulia.

2.Baking soda

Baking soda ni moja ya bidhaa ingine inayopatikana kwa urahisi itakayokutibu kiungulia chako. Kumbuka tu kwamba kuna tofauti kati ya baking soda na baking powder. Ukienda dukani au supermaket ulizia baking soda.

Matumizi ya baking soda kutibu kiungulia

Chukua kijiko kidogo cha baking soda, changanya na maji nusu glass kisha kunywa haraka kabla povu halijaisha.

Angalizo

Usitumie baking soda mara mara kwa mara kwani yaweza kupelekea chakula kutosagwa tumboni na kukufanya uvimbiwe na kuharisha.
Pia baking soda isitumike kwa mgonjwa wa presha, ama mgonjwa aliyekatazwa kula chunvi kwani ina sodium kwa wingi. Ongea daktari kabla ya kutumia baking soda endapo unaumwa presha.

3.Juisi ya Aloe vera

Aloe vera ni moja ya mimea adhimu sana kutokea kwani inatibu magonjwa mengi. Hakikisha unapata juisi salama ambayo haijawekwa kemikali mbaya. Mmea wa aloe vera ni mchungu sana, kabla hujaanza kutumia tafuta kwanza kwenye maduka ya tiba asili kama utapata juisi ya aloe vera iliyopunguzwa makali.

Matumizi ya aloe vera kutibu kiungulia

Kutibu kiungulia kunywa robo kikombe cha juisi ya aloe vera kila siku asubuhi kabla hujala chochote. Endapo utakosa juisi, unaweza pia kutafuta vidonge vya aloe vera vitakufaa sana kutibu kiungulia.

4.Tangawizi

Tangawizi moja ya dawa asili kabisa ya kutibu maumivu ya mwili. Pia tangawizi ni nzuri kwa kuuimarisha usagaji wa chakula tumboni na kuzuia asidi ya tumbo kupanda juu. Tangawizi pia inazuia athari ya bakteria wabaa tumboni.

Matumizi ya tangawizi kwa kiungulia

Kutibu kiungulia, tengeneza chai ta tangawizi na unywe baada tu ya kumaliza kula.

5.Binzari nyembamba(Cumin)

Moja ya tiba ingine makini sana ya kiungulia inayopatikana jikoni kwako ni binzari nyembamba ambayo hutumika sana kwenye kupika pilau. Gesi inapojaa tumboni inaweza kusababisha kiungulia pia. Kutumia binzari nyembamba itakusaidia kuondoa gesi tumboni a hivo kuepusha kiungulia.

Matumizi ya binzari nyembamba

Chukua kijiko kimoja cha bidhaa nyembamba chemsha pamoja na maji nusu lita kisha kunywa mara tatu kwa siku baada ya mlo wako.

6.Tui la nazi

Utashangaa kwamba kiungo hichi ambacho umekuwa ukitumia kila siku kupika wali na maharage, kinaweza kutibu changamoto yako ya kiungulia pasipo kumeza dawa.

Matumizi

Baada ya kukuna nazi yako, weka machicha ya nazi kwenye sufuria, sagia na tangawizi kidogo pamoja na maji lita moja kisha chemsha kwa dakika 5 epua. Chuja tui lako kisha kunywa glass moja asubuhi na jioni kabla ya kula.

Tumia Dawa asili za kayam kutibu Kiungulia chako

Vidonge hivi asili vimekuwa yakitumika kwa muda mrefu huko india kwa ajili ya changamoto mbalimbali kama kiungulia, gesi tumboni , maumivu ya kichwa, na kukosa choo.
Hivi sasa viodonge hivi yameonekana kutibu magonjwa mengine zaidi kama bawasili, kuharisha na kuimarisha usagaji wa chakula tumboni.

Matumizi: Meza vidonge viwili usiku kabla ya kula, kila siku kwa siku 15. Gharama ni Tsh 35,000/= kwa dozi ya wiki mbili.
Tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254 upate Dawa.

Bofya kusoma kuhusu: Tatizo la kula udongo na suluhisho lake