Aina za Uchafu Ukeni

uchafu ukeni wenye harufu
Uchafu ukeni wenye harufu

Kutokwa na uchafu ukeni ni jambo la kawaida kabisa kwa mwanamke. Hata hivo kuna aina zingine za uteute ambazo zaweza kuashiria kuna maambukizi.

Uchafu usiyo wa kawaida unaweza kuwa na rangi ya kijani, njano na wenye harufu mbaya. Maambukizi yanayowapata sana wanawake ni ya baketria ya ya fangasi na kupelekea kutokwa na uchafu usio wa kawaida unaoambatana na harufu mbaya.

Aina za Uchafu Ukeni

Kuna aina nyingi za uchafu ukeni. Aina zifuatazo zimegawanywa kwa kulingana na rangi na kiwango cha utokaji wake. Utaona kwamba aina zingine za uchafu ni salama na uchafu mwingine siyo salama, unaashiria kuwepo kwa ugonjwa

Uchafu Mweupe Ukeni

Kutokwa na uchafu mweupe hasa mwanzoni mwa hedhi au mwishoni mwa hedhi ni jambo la kawaida. Hata hivo kama uchafu huu unaambatana na muwasho na ni mzito sana kama maziwa ujue siyo kawaida na inahitaji upate vipimo na tiba hospitali kwani ni kiashiria cha fangasi ukeni.

Uchafu Mwepesi Kama Maji

Uchafu mwepesi kama maji ni kawaida kabisa. Unaweza kupata uchafu huu muda wowote katika mzunguko wako na hasa baada ya kufanya mazoezi.

Uchafu mwepesi unaovutika

Ukiona uteute mwepesi na unavutika kama ute wa yai basi ujue upo kwenye ovulation, yaani siku za hatari na yai limepevuka tayari kwa kurutubishwa. Uteute huu ni wa kawaida.

Uchafu wa brown unaoambatana na damudamu.

Kama unapata uteute huu kabla ya hedhi na ulifanya tendo bila kinga basi kuna uwezekano ukawa umeshika mimba. Kama uchafu huu unatoka wakati mimba yako bado ni changa basi yaweza kuashiria kwamba mimba inaharibika unatakiwa kuwahi hospitali haraka.

Kwa kesi chache sana uchafu wa brown wenye damu damu ni kiashiria cha saratani ya shingo ya kizazi ama pia uvimbe kwenye kizazi(fibroids) ama uvimbe mwingine kwenye kizazi. Ndio maana ni muhimu sana kufanya utrasound kucheki hali ya kizazi endapo utaona dalili zisizo za kawaida kama hizi.

Uchafu Wa njano au kijani

Kama unapata uchafu wa kijani au njano unaoambatana na harufi mbaya siyo jambo la kawaida. Uchafu wa namna hii ni kiashiria kwamba kuna maambukizi ya ugonjwa wa zinaa. Inahitaji uende hospitali haraka kupata vipimo na tiba.

Lini unatakiwa Kumwona Daktari

Kama unapata uchafu usio wa kawaida na unaambatana na dalili hizi muhimu umwone daktari haraka

  • homa
  • maumivu chini ya kitovu
  • kuishiwa nguvu
  • maumivu wakati wa kukojoa na
  • kukojoa mara kwa mara

Utegemee nini unapofika Hospitali kumwona Daktari

Unapomwona daktari kwa ajili ya uchafu unaokutoka usio wa kawaida, atakufanyia vipimo vya uzazi na vipimo vya kutumia macho na mikono(physical exam).

Daktari pia atakuuliza baadhi ya maswali kuhusu dalili unazopata, mzunguko wako, na hali ya tendo la ndoa.

Kama daktari hatagundua tatizo mapema basi anaweza kuagiza ufanyiwe baadhi ya vipimo kama una saratani ya kizazi ama virusi wa HPV. Daktari anaweza pia kuagiza sampuli ya uteute wako kuchukuliwa na kupelekwa maabara kwa ajili ya vipimo zaidi.

Namna ya kujihudumia nyumbani kwa tatizo la kutokwa na uchafu ukeni

Kujikinga usipate maambukizi, zingatia usafi wa uke na kuvaa chupi za cotton. Zingatia usalama kwenye tendo la ndoa kwa kutumia kinga kama huna imani na mpenzi wako kuepusha magonjwa ya zinaa.
Tumia maziwa mgando mara kwa mara ili kurejesha mazingira mazuri ya bakteria ukeni na kulinda uke dhidi ya fangasi.

Tumia Vidonge Asili vya UCP-Vinasafisha uke na kurejesha ute mzuri.

Uterus cleansing pills (UCP) ni dawa yenye vidonge 2 kama vinavyoonekana kwenye picha hapo juu. Vinatumika kwa wiki moja kusafisha uke, kurejesha uteute mzuri na kutibu maambukizi ukeni. Matumizi ya vidonge ni kwa kuweka kidonge ukeni na kutoa kila baada ya siku tatu, unapumzika masaa 24 unaweka kidonge kingine.

Vidonge vimetengenezwa kitaalamu kupitia muunganiko wa mimea na kuhifadhiwa vizuri ili kutunza uasili wa dawa pasipo kuwekwa kemikali.
Angalizo: Vidonge havifai kutumika kwa mjamzito na bikira.

angalizo

Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge vyenye mfanano na hivi vya UCP, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb.

Gharama ni Tsh 50,000/=
Tuandikie whatsapp no: 0678626254 kuanza Tiba.

Bofya kusoma makala inayofuata Kuhusu: Aina za harufu ukeni

2 replies on “Aina za Uchafu Ukeni”

Jee unaweza kumaliza bleed na ukaendelea kutoka uchafu kwa siku tatu au zaidi je inaashiria nn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *