Tiba ya hedhi kuvurugika

tiba ya hedhi kuvurugika

Hedhi ni matokeo ya kubomoka kwa ukuta wa kizazi ulioandaliwa kushikilia mimba lakini kwa vile mimba haijashika ukuta huu humeguka na kutolewa nje kama damu . Inapotokea umepitisha mwezi bila hedhi au kupitisha zaidi ya siku 7 tayari una tatizo la hedhi kuvurugika.

Kwa kila mwanamke kuwa na mzunguko mzuri wa hedhi ni jambo la kujivunia na linaloleta heshima. Mzunguko wa hedhi unatoa picha kamili nini kinaendelea kwenye mwili wa mwanamke. Mzunguko unakujulisha endapo mfuko wa mimba unapata mzunguko mzuri wa damu, homoni zako zimebalansi, au kama mayai yanapevuka.

Wanawake huanza hedhi katika kipindi cha kubalehe kuanza miaka 10 mpaka 16 na hedhi huendelea mpaka pale wakifikia kukosa yani menopasue, miaka 45 mpaka 50

Nini kinasababisha Hedhi Kuvurugika?

1.Homoni kuvurugika:

Homoni au vichocheo vikuu vinazoratibu mpangilio wa hedhi yako ni estrogen na progesterone. Inaweza kuchukua miaka mingi kwa homoni hizi kuwa na uwiano sahihi. Vihatarishi ambavyo vinapelekea kuvurugika kwa homoni na hatimaye hedhi kuvurugika ni pamoja na

 • Matumizi ya uzazi wa mpango wa kisasa kama sindano,kitanzi, vidonge na njiti
 • Uzito mkubwa kupita kiasi na kitambi
 • Kupungua uzito kupita kiasi
 • Msongo wa mawazo
 • Changamoto za kushindwa kula vizuri na hivo kukosa virutibishi muhimu
 • Mazoezi makali mfano riadha

2.Vimbe kwenye mayai(polycstic ovarian syndrome)

Mfuko wa mayai kwa mwanamake huitwa ovary na mifuko hii huwa miwili kushoto na kulia. Kila mwezi mwanamke hutoa yai moja kwenye kikonyo chake katika upande mmoja ili liweze kurutubishwa. Inapotokea mayai kugoma kutoka kwenye mfuko ndipo uanageuka kuwa vimbe zenye maji (cyst) zikiwa nyingi huitwa polycyst. Changamoto hii ndio chanzo kikuu cha mwanamke kuvurugikiwa hedhi.

3.Kuugua maambukizi kwenye kizazi(PID) kwa muda mrefu

 Kama maambukizi haya yasipotibiwa mapema yanaweza kuathiri mirija ya uzazi pamoja na kizazi kwa ujumla na hivo kuvuruga mpangilio wa hedhi, soma kwa kina kwa kubofya hapa kuhusu ugonjwa huu wa PID, dalili na tiba pia.

4.Saratani kwenye kizazi 

Saratani inaweza kusababisha mwanamke kupata hedhi nzito sana ama hedhi katikati ya mzunguko wake.

5.Matatizo ya tezi ya shingoni (thyroid gland)

Tezi hii ndio inayoratibu utolewaji wa homoni za estrogen na progesterone, tezi ikipata hitilafu inapelekea kuvurugika kwa homoni na hivo hedhi pia kuvurugika.

6.Kuvimba kwa kiazi(endometriosis)

Hali hii hutokea pale seli za ndani ya mfuko wa mimba zinapoota na kutoka nje ya mfuko wa mimba, hali hii hisababisha maumivu makali wakati wa hedhi lakini pia yaweza kusababisha mabaki ya hedhi kwenye kizazi.

Jinsi ya Kuhesabu Siku za Mzunguko wa Hedhi

Siku ya kwanza ya mzunguko ni siku ambayo unapata hedhi katika mwezi husika. Siku zote kati kuanzia siku ya kwanza ya hedhi mpaka siku ya ovulation (yai kutolewa) huitwa follicular phase. Kipindi hiki kikawaida huchukua siku 14 lakini hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke.

Luteal phase ni kipindi kati ya ovulation(siku ambapo yai limetolewa) na siku ya kwanza kupata hedhi katika mwezi,ni katika kipindi hiki ambapo yai lililorutubishwa hujishikiza kwenye ukuta wa uterus. Kama kipindi (luteal phase) kitakuwa kifupi sana chini ya siku 12 basi itakuwa ngumu kwa kiumbe kujishikiza kwenye ukuta.

Mzunguko wa kawaida ni upi?

Mzunguko wa kawaida unatakiwa kuchukua siku 21 mpaka 35. Baadhi ya wanawake wanaweza kuwa na mzunguko mfupi zaidi au mrefu kuliko huu. Kiwango cha homoni na utolewaji wa yai ndivyo vinatengeneza uwiano wa mzunguko wa hedhi. Kama yai halitatolewa itapelekea kuvurugika kwa hedhi na tena kupelekea yai kutotolewa, inakuwa ni kitu endelevu.

Tiba asili kupitia vidonge vya Evecare

Dawa ni asili na imetengenezwa nchini India kupitia mimea ua Ashoka, Asaparagus na lodh tree. Kwa miaka zaidi ya mitano ambayo tumekuwa tukihudumia wagonjwa wetu wa matatizo ya hedhi, tumepokea shuhuda lukuki. Evecare inakuwa na vidonge 30, unameza vidonge viwili kila siku kwa muda wa wiki mbili kurekebisha.

Baada ya kutumia Evecare tegemea kupata matokeo haya

 • Mzunguko wa hedhi kurekebika na kuanza kupata kila mwezi
 • Hedhi kutoka vizuri kwa siku chache siyo zaidi ya siku 5 ama 7
 • Maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi kuisha kabisa
 • Homoni kubalansi
 • Kupata hedhi nyepesi ya kawaida
 • Kizazi kuimarika sana hata kuongeza chansi ya kushika mimba kama wewe ni muhanga wa kukosa mimba kwa muda mrefu.

Kabla hujaanza tiba hakikisha

 • Umefanya utrasound na kizazi hakina vimbe(kama una vimbe utibiwe kwanza mpaka upone
 • Umeshaacha kutumia uzazi wa mpango

Tahadhari

Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge fake vya evecare, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb

Gharama za dawa ni Tsh 75,000/=, Tuandikie whatsapp no- 0678626254 upate huduma. Ofisi ipo hapa Mwembechai Dar.