Kipandikizi/njiti kuzuia mimba na kupanga uzazi

kipandikizi au njiti kwa ajili ya kupanga uzazi
mwonekano wa vipandikizi

Kipandikizi au njiti ni njia mojawapo ya kisasa inayotumika kuzuia usishike mimba kabla hujapangilia. Vipandikizi kama ilivyo kwa sindano na vidoonge vinakuwa na kemikali za progestin ambazo zinabadili mpangilio wa homoni zako. Kipandikizi kinakuwa na mwonekano wa kipande kidogo cha plastic kama njiti ya kiberiti, na kinawekwa eneo a juu la mkojo wako chini ya ngozi.

Namna kipandizi kinavyofanya kazi

Kipandikizi kinatoa kichocheo au homoni inayoitwa etonogestrel kwenye mwili. Homoni hizi zinazuia mayai kupevuka na kutolewa kwa ajili ya urutubishaji. Pia homoni hii inafanya uteute wa ukeni kuwa mzito sana ili kuzuia mbegu kuogelewa kwenda kurutubisha yai.

Kama utawekewa kijiti ndani ya siku tano baada ya kuanza hedhi, hapo hutaweza kushika mimba kwa mwezi huo. Lakini kama njiti itawekwa siku ingine kwenye mzunguko hapo waweza kushika mimba kwenye mwezi husika. Njiti ama kipandizi kinaanza kufanya kazi vizuri baada ya siku saba.

Je kuna madhara ya kutumia njiti/kipandikizi?

Baadhi ya wanawake hupata madhara wanapotumia kipandizi, japo wengi hawapati changamoto. Kuvurugika kwa hedhi ni dalili kubwa sana. Pia hedhi yaweza kuwa nyepesi sana, nzito sana au usipate kabisa hedhi. Madhara mengine ya njiti ni pamoja na

Matokeo haya kwa kiasi kikubwa huisha ndani ya miezi michache, na kwa kiasi kidogo athari inaweza kuendelea zaidi.

Jinsi ya kutumia kipandizi au njiti

Kuanza kutumia njiti au kipandikizi yatakiwa uende hospitali umuone daktari. Baada ya kupimwa, daktari ataingiza kifaa kidogo cha plastic mithili ya njiti chini ya ngozi kwenye eneo la juu la mkono. Kipandikizi kinaweza kukaa mpaka miaka mitatu kikakulinda usishike mimba. Kitendo cha kuwekewa kijiti ni rahisi sana na kinachukua dakika chache tu.

Baada ya kuwekewa kipandikizi, muhudumu atakufunga bandage na utaruhusiwa kwenda nyumbani siku hiyo hiyo. Unaweza kupata kovu, maumivu na kuvimba kidogo baada ya kuwekewa njiti. Baada ya miaka mitatu kijiti kitapungua nguvu na utahitaji kubadilisha kingine

Muda wa kutoa kipandikizi

Kipandikizi kinatakiwa kutolewa baada ya miaka mitatu. Pia kama umeamua kushika mimba mapema kabla ya miezi mitatu unaweza kutoa kipandikizi. Endapo utaamua hivo, nenda hospitali na daktari atakata kidogo eneo lenye kipandikizi na kukitoa.

Faida za kutumia kipandikizi

Moja ya sababu kwanini njiti ni njia bora kuzuia mimba ni kwasababu ni rahisi kutumia. Faida zingine ni pamoja na

  • huhitaji kubadili njia ingine ya kupanga uzazi kwa miaka mitatu
  • uwezo wa kushika mimba utarejea mapema tu baada ya kutoa njiti
  • inafaa sana wa wanawake ambao miili yao inakataa njia za kuzuia mimba zenye homoni ye estrogen.

Zipi ni hasara za kutumia kipandikizi?

  • Kipandikizi hakitakuzuia kupata magonjwa ya zinaa kama ukimwi na kisonono
  • Uwekaji wake unahitaji mtaalamu ama daktari
  • Wakati wa kutoa inaweza kuwa changamoto kwa mtoa huduma kukiona

Soma zaidi kuhusu: sindano za kupanga uzazi

Leave a Reply

Your email address will not be published.