Dawa ya fluconazole kutibu fangasi

dawa ya fluconazole
fluconazole

Dawa ya fluconazole ni dawa inayotumika kutibu fangasi mbalimbali. Fluconazole ipo kwenye kundi la dawa za azole antifungals, inafanya kazi kwa kuzuia kusambaa kwa aina nyingi za fangasi.

Dawa ya Fluconazole inatumikaje?

Kabla hujaanza kutumia dawa muhimu usome karatasi ya maelezo kutoka kwa mfamasia anayekuhudumia. Kama una swali muulize muhudumu mapema.

Meza dawa baada au kabla ya kula kama ulivoelekezwa na daktari, mara nyingi fluconazole hutumia mara moja kwa siku.

Kama unatumia fluconazole ya maji, hakikisha unatikisa chupa vizuri kabla ya kutumia. Pima vizuri kiwango cha dawa kwa kutumia kijiko kilichokuja na dawa ili kupata dozi sahihi. Kamwe usitumie kijiko cha nyumbani kwani hutapata kiwango kinachohitajika cha dozi yako.

Dozi ya fluconazole

Dozi yako ya dawa inaweza kuegemeana na aina na ukubwa wa tatizo lako baada ya uchunguzi wa daktari. Kwa watoto dozi yao hutegema pia na uzito. Kwa ujumla dozi ya watoto haitakiwi kuzidi milligram 600 kwa siku, labda kama daktari atapendekeza vingine.

Dawa inafanya kazi vizuri endapo itatumika katika muda ule ule na kwa kiwago kile kile kila siku. Kwahivo muhimu tumia dawa saa ile ile kila siku,mfano saa 6 kamili mchana kila siku.

Endelea kutumia dawa mpaka dozi yote itakapoisha, hata kama utaanza kujisikia nafuu mapema. Kuacha kutumia dozi mapema itafanya vimelea wa fangasi kuendelea kukua na kuleta madhara zaidi. Mjulishe daktari kama hali itazidi kuwa mbaya.

Matokeo ya fluconazole

Kichefuchefu, kuharisha, tumbo kuvurugika, kichwa kuuma, kuishiwa nguvu na nywele kunyonyoka, ni dalili unazoweza kuzipata wakati wa dozi ya fluconazole. Kama moja ya dalili hizi itakuwa baya zaidi, mjulishe daktari au mfamasia aliyekuhudumia mapema.

Kumbuka kwamba daktari ameamua kukupa dawa hii kwasababu tayari ameshajiridhisha faida utakazopata ni kubwa kuliko madhara. Watu wengi wanaotumia dawa hii hawapati madhara makubwa, na dalili mbaya zinatoweka mapema tu baada ya kumaliza dozi.

Muhimu tu umjulishe daktari endapo utaanza kupata dalili mbaya zaidi kama kukosa hamu ya kula, kuchoka kupita kiasi na uzito kupungua. Pia dalili zingine mbaya kama mabadiliko ya mapigo ya moyo na kupoteza fahamu yanahitaji usaidizi wa hospitali haraka sana.

Madhara yanayoweza kutokea baada ya kutumia fluconazole

Kwa kiwango kidogo sana dawa hii ya fluconazole inaweza kuathiri ini na kusababisha magonjwa ya ini. Nenda hospitali mapema kama utaanza kupata dalili za ini kuathirika. Dalili kama maumivu makali ya tumbo, kutapika muda wote, ngozi kuwa ya njano na mkojo mweusi.

Aleji kutokana na dawa inatokea mara chache zaidi. Nenda hospitali haraka endapo utaona dalili za aleji kama

  • homa kali isiyoisha
  • kuvimba mtoki kupita kiasi,
  • muwasho na kuvimba hasa sehemu za uso,
  • ulimi na koo na
  • kushindwa kupumua vizuri.

Tahadhari unapotumia dawa ya fluconazole

Kabla ya kuanza kutumia fluconazole, mjulishe daktari au mfamasia kama una aleji nayo au una aleji na dawa zingine za fangasi kama ketoconazole na itraconazole. Dawa hii yaweza kuwa na kiambata hai kinacholeta aleji kwa baadhi ya wagonjwa.

Kabla ya kuanza dawa, mjulishe daktari au mfamasia historia yako ya kuumwa, hasa kama una magonjwa ya figo na ini.

dawa ya fluconazole na Tatizo la moyo

Fluconazole inaweza kuleta mabadiliko kwenye mwenendo wa mapigo ya moyo. Dalili kama kupoteza fahamu na usingizi kupita kiasi zinahitaji uangalizi haraka wa hospitali.

Hatari ya kubadilika kwa mapigo ya moyo endapo una magonjwa mengine ya moyo yanayokusumbua kwa muda mrefu. Mjulishe daktari mapema historia yako, hasa kama una magonjwa ya moyo.

Kiwango kidogo cha madini ya potasssium au magnesium kwenye damu inaongeza hatari ya kuathirika mapigo ya koyo. Dawa za kutoa mkojo mwingi kwa haraka (diuretics) zinafanya madini haya kupungua. Pia kama una changamoto ya kutokwa na jasho jingi zaidi, kuharisha na kutapika sana ni chanzo cha kuishiwa madini. Zungumza na daktari vizuri kabla hujaanza kutumia fluconazole.

dawa ya Fluconazole na kizunguzungu

Japo inatokea mara chache sana, fluconazole yaweza kukufanya upate kizunguzungu. Matumizi ya pombe na bangi wakati unaendelea na dawa itafanya hali kuwa mbaya zaidi. Usiendeshe vitu vovyote vya moto wakati upo kwenye dozi. Punguza matumizi ya pombe na bangi kama unatumiaga.

Kabla ya upasuaji wowote mjulishe daktari endapo upo kwenye dozi ya fluconazole, au dawa zozote zingine pamoja na tiba asili au virutubisho.

Kwa mjamzito, dawa itumike tu endapo kuna ulazima wa kuitumia. Na hilo utaambiwa na daktari hospitali baada ya kuchambua hali ya afya yako na kuona dawa ipi akupatie. Dawa inaweza kumuathri mtoto aliye tumboni endapo itatumika miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito.

Fluconazole yaweza kupenya mpaka kwenye maziwa lakini ni ngumu kuleta athari kwa mtoto. Zungumza na daktari kama unanyonyesha kabla hujaanza tiba.

Muhimu kuzingatia

  • Usichangie na mtu mwingine dozi uliyopewa hospitali
  • Dawa inatumika tu kwa maambukizi ya fangasi na siyo maambukizi mengine ya bakteria au virusi
  • Usitumie dawa zilizobaki kujitibu kwa siku sijazo .

Endapo utasahau kumeza dozi, meza mapema pale unapokumbuka. Meza dawa muda ule ule kila siku. Na kama unapata dalili mbaya zaidi muone daktari mapema

Uhifadhi wa dawa

Tunza dawa kwenye joto la wastani mbali na mwanga mkali na pasiwe na unyevunyevu. Usitunze dawa chooni. Dawa isiyotumia itupe. Hifadhi dawa mbali na watoto. Tupa dawa kama imepita muda wake wa matumizi (expire date)

Unahitaji maoni ama ushauri? Tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254 utajibiwa, Usipige simu namba ni ya whatsapp tu.

Bofya kusoma kuhusu: fangasi mdomoni

One reply on “Dawa ya fluconazole kutibu fangasi”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *