Kuvimba fizi na kuuma

kuvimba fizi
fizi zilizovimba

Kuvimba fizi kitaalamu gingivitis ni changamoto ya meno inayotokea kila mara na mara chache sana huleta tatizo kama isipotibiwa haraka. Dalili za kuvimba fizi ni pamoja na fizi kututumka na kuwa nyekundu sana.

Changamoto ya fizi kuvimba mara nyingi huisha yenyewe kwa kuzingatia tu usafi wa kinywa, kama kupiga mswaki mara mbili kwa siku. Kwa nyongeza unaweza kufanya coconut oil pulling kusafisha meno badala ya kutumia mouthwash ambazo zina madhara.

Aina ya Tatizo la kuvimba fizi

Kuna aina kuu mbili za tatizo la kuvimba fizi

Dental paque-induced gingival disease: Hii yaweza kusababishwa na utando kwenye jiono, matumizi ya dawa fulani na ukosefu wa lishe bora

Non-plaques induced gingival lesions: Hii inaweza kusababishwa na aina fulani ya bakteria, virusi au fangasi. Pia yaweza kusababishwa na changamoto za kurithi, vidonda na aleji ya vitu vya nje.

Nini kinasababisha kuvimba fizi?

Chanzo kikuu cha kuvimba fizi ni utando wenye mrundikano wa bakteria katikati ya meno. Utando huu unapelekea kinga ya mwili kupamba na bakteria na hivo kupelekea tishu za karibu kuumia na kuvimba. Pia inaweza kupelekea tatizo kubwa la kuoza jino kabisa endapo hutapata tiba mapema.

Utando wa kwenye jino hufanyika ili kulinda jino lisihsambuliwe na vimelea wabaya. Lakini utando huu usipoondolewa mapema kwa kupiga mswaki, unageuka kuwa nta chini ya jino na kwenye fizi. Nta hii huwa na rangi ya njano na hupelekea fizi kuvimba.

Vyanzo vingine vya fizi kuvimba

 • Mabadiliko ya homoni: Hii inaweza kutokea wakati wa kubalehe, kukoma hedhi-menopause, kwenye mzunguko wa hedhi na wakati wa ujauzito.
 • Baadhi ya magonjwa: Kama saratani, kisukari, HIV hupelekea fizi kuvimba
 • Dawa: Afya ya kinywa inaweza kuathiriwa na matumizi ya baadhi ya dawa , hasa zile zinazopunguza kiwango cha mate mdomoni.
 • Kuvuta sigara: Wavtaji wa sigara wapo kwenye hatari zaidi ya kuvimba fizi ukilinganisha na wale wasiovuta sigara
 • Umri: Hatari ya kuvimba figo inaongezeka zaidi kadiri unavyozeeka
 • Lishe mbovu: Upungufu wa vitamin C kwenye lishe yako ni hupelekea magonjw aya fizi.
 • Historia ya kuugua kwenye familia: Kwa wale ambao wazazi wao wana matatizo ya fizi, wako kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo.

Dalili za Fizi Kuvimba

Kwa tatizo likiwa dogo, unaweza usipate shida yoyote na pengine usigundue kabisa kama fizi zimevimba. Kwa tatizo kubwa unaweza kupata dalili hizi

 • fizi kuwa nyekundu sana
 • kulainika kwa fizi na kuuma
 • kutokwa damu kwenye fizi wakati wa kuswaki
 • harufu mbaya mdomoni

Vipimo kugundua tatizo

Mtaalamu wa magonjwa ya meno (dentist) atakuchunguza uwepo wa nta na utando na kukuuliza dalili unazopata.

Matibabu ya kuvimba fizi

Tiba kwa changamoto ya kuvimba fizi inahusisha huduma kutoka kwa mtaalamu wa meno, usafi wa meno ukiwa nyumbani na pia kuendelea kuhudhuria kliniki ya meno kaa daktari atakavyoshauri.

Huduma ya nyumbani

Kulinda afya ya meno yako tunashauri

 • kusafisha meno mara mbili kwa siku, asubuhi na usiku kabla ya kulala
 • tumia uzi wa kusafisha uchafu katikati ya meno
 • baada ya kula suuza mdomo wa maji na uteme
 • tumia coconut oil pulling kusafisha meno (maelezo ya kina yanapatikana hapa)

Kama umependezwa na huduma yetu na unahitaji kutuchangia chochote ili tuendelee kutoa zaidi elimu hii, Wasiliana nasi kupitia whatsapp namba 0678626254.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *