Categories
Afya ya uke Aina za Uchafu Ukeni

Uchafu wa njano ukeni maswali na majibu

uchafu wa njano ukeni
uchafu wa njano

Kutokana na sababu kadhaa, kutokwa na uchafu wa njano ukeni yaweza kuwa salama au hatarishi. Zifuatazo ni njia za kutambua kama uchafu wako ni salama ama ni kiashiria cha ugonjwa.

Aina za uchafu wa njano ukeni

Kutambua kama uchafu wako ni salama au hatari, unatakiwa kufatilia na kuzingatia baadhi ya mambo. Kuna aina nyingi sana za uchafu wa ukeni, hivo unahitajo kufatilia rangi, mwonekano, uzito na wepesi na harufu ya uchafu ili kujua kama watakiwa umwone daktari.

Kama uchafu wako wa njano hauna harufu kwa kiasi kikubwa huhitaji kumwona daktari. Uchafu wenye harufu unaweza kuashiria mamabukizi flani. Na kama uchafu wako unanuka, tambua kwamba ile rangi ya njano ni kiashiria cha aina ya maambukizi husika.

Uchafu mwepesi wa njano usiokolea na ambao hauna harufu wala dalili zozote mbaya kama maumivu ya tumbo, maumivu kwenye uke au muwasho, hapo hakuna tatizo ni uchafu wa kawaida.

Njano iliyokolea na uchafu mzito, ukiwa unaambatana na harufu mbaya, huu ni uchafu usio kawaida na unaashiria maambukizi.

Je ni kawaida mwanamke kupata uchafu wa njano ukeni?

Katika baadhi ya mazingira ni kawaida kupata uchafu wa njano. Siku chache baada ya hedhi unaweza kuona ute wa njano kama cream au unaonata.

Utakapokarbia hedhi, uchafu waweza kuwa mweusi kutokana na vipande vya damu kujichanganya na uchafu wa ukeni.

Kadiri hedhi inavokaribia kuisha rangi ya damu inabadilika kutoka kuwa nyekundu na kuwa brown na baadae kuwa na unjano. Huu uchafu wa njano ni masalia ya hedhi ya mwisho iliyobaki kwenye kizazi.

Uchafu wa njano ukeni ni wa kawaida endapo haujaambatana na harufu mbaya, muwasho, maumivu chini ya kitovu, maumivu kwenye tendo na maumivu wakati wa kukojoa.

Kama uchafu wa njano unanuka na kuna muwasho nini chanzo??

1.Maambukizi ya fungus -yeast infection

Uke wako unatakiwa kuwa na uwiano sawa wa vimelea na utindikali pia. Pale inapotokea mazingira yakavurugika, bakteria na fungus huanza kukua kupita kiasi na kukufanya uumwe. Kufanya tendo la ndoa na watu wengi, kutumia antibiotic mara kwa mara, kuosha uke mpaka ndani na kuvurugika kwa homoni inaweza kuvuruga mazingira ya uke.

Fungus ukeni, ni ugonjwa unatokea sana kwa wanawake wengi. Ugonjwa unatokea pale vimelea wa fungus wanapokua kupita kiasi.

Dalili kubwa za fangas ukeni ni pamoja na

 • muwasho kwenye mashavu ya uke
 • kuvimba kwa mashavu ya uke
 • maumivu wakati wa tendo
 • maumivu na hali ya kuungua wakati wa kukojoa
 • uke kuuma na kuvimba
 • uchafu mweupe wa kuganda kama mtindi

2.Ugonjwa wa Trichomoniasis

Ni ugonjwa unaotibika na unaambukiwa kupitia zinaa. Watu wengi waliathiriwa na ugonjwa huu hawakujua kama wameshaambukiwa sababu dalili huwa zinachelewa kujionesha.

dalili za trichomoniasis ni pamoja na

uchafu wa njano au kijani wenye harufu mbaya
kuvimba kwa mashavu ya uke na uke wote
kuhisi haja ndogo mara kwa mara
maumivu wakati wa tendo la ndoa na
maumivu wakati wa kukojoa

Ugonjwa unatibika kupitia antibiotics, endapo utapimwa na kugundilika na ugonjwa hakikisha unampeleka na mpenzi wako kupimwa.

3.Kisonono na Chlamydia

Magonjwa haya yote yanaabukizwa kwa zinaa. Magonjwa haya yanatibika kupitia antibiotics endapo utaanza tiba mapema. Kama hautapata tiba mapema, yaweza kupelekea upate PID, mirija kuziba na maumivu makali ya nyonga kutokana na makovu kwenye kizazi.

Ndiomaana ni muhimu sana kupima magonjwa ya zinaa mara kwa mara, hasa kama una wapenzi wengi au kama umekutana bila kinga na mpenzi mpya.

Dalili kubwa za chlamydia na kisonono ni pamoja na

 • kuongezeka kwa kiwango cha uchafu ukeni
 • maumivu wakati wa kukojoa na kwenye tendo
 • kutokwa na bleed katikati ya mzunguko
 • maumivu makali ya nyonga

4.PID

Pid ni kifupi cha pelvic inlafammatory disease. Ni athari kwenye via vya uzazi kwa mwanamke, na inatokea pale magonjwa kama chlamydia na kisonono yasipotibiwa vizuri na kuisha mpaka kusambaa kwenye mirija, na mayai. Aina nyingi za maambukizi ya bakteria zaweza kupelekea uugue PID.

Endapo PID haitatibiwa vizuri yaweza kupelekea changamoto kama mimba kutunga nje ya kizazi, mimba kuharibika na maumivu makali ya nyonga.

Dalili za PID ni pamoja na

 • uchafu wa njano au kijani ukeni wenye harufu mbaya
 • hedhi kuvurugika
 • maumivu wakati wa tendo
 • maumivu wakati wa kukojoa
 • kutokwa damu wakati na baada ya tendo
 • kuhisi homa na kichefuchefu

Uchafu wa njano wakati wa ujauzito

Mimba inakuja na mabadiliko mengi sana kutokana na kuongezeka kwa baadhi ya homoni. Wajawazito wengi wanashuhudia ongezeko la uchafu unaotoka ukeni kutokana na kuongezeka kwa homoni za estrogen na progesterone.

Kama unapata uchafu mweupe , mwembamba usio na harufu mbaya hiyo ni kawaida. Kitaalamu uchafu unaitwa leukorrhea.

Kama utaona uchafu wa kijani au njano wenye harufu mbaya, hiyo yaweza kuashiria maambukizi. Wajawazito wanaugua sana fungus ukeni. Unatakiwa kwenda hospital mapema upate vipimo na dawa.

Endapo hujatibiwa fungus au magonjwa ya zinaa, inaweza kuhatarisha afya ya mtoto wakati anazaliwa. Maana mtoto anaweza kupata maambukizi.

Mwisho kabisa

Kama wewe ni mwanamke, ujue kwamba lazima utakutana na changamoto nyingi kwenye uke wako hasa wala la uchafu ukeni. Ni muhimu sana kujielimisha na kujua uchafu upi ni hatari na upi ni salama ili umwone daktari mapema.

Kwa ushauri na tiba tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *