Kukojoa Usaha na Vitu Vyeupe

kukojoa usaha

Kuna changamoto nyingi zaweza kupelekea mtu kukojoa usaha na vitu vyeupe. Na habari njema ni kwamba matatizo mengi yanatibika hospital, l;akini unatakiwa tu kuwahi hospital kupata vipimo kila unapoona dalili mbaya. Endelea kusoma zaidi kujua kwanini unatokwa na usaha kwenye mkojo na hatua za kuchukua

Maambukizi ya Bakteria Kwenye Njia ya Mkojo-UTI

UTI ni kifupi cha urinary tract infection. Ni chanzo kikubwa sana cha kufanya utokwe na vitu vyeupe wakati wa kukojoa. UTI ni maambukizi kwenye njia ya mkojo yani mrija wa kutolea mkojo, kibofu cha mkojo na figo.

Wanawake na wanaume wote wanaugua UTI na wanaweza kupata hii hali ya kutokwa na uchafu mweupe wakati wa kukojoa.

Dalili zingine za UTI

 • kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
 • kupata haja ndogo mara kwa mara
 • kuongezeka kwa hamu ya kwenda kukojoa
 • kushindwa kutoa mkojo mwingi kwa pamoja
 • damu kwenye mkojo
 • kuhisi mgandamizo uzito eneo la nyonga
 • kutoa mkojo wenye harufu kali
 • maumivu eneo la mkundu wa wanaume
 • maumivu kwenye nyonga kwa wote wanaume na wanawake na
 • maumivu kwenye tumbo la chini

Kumbuka maambukizi mengi ya bakteria yanatibika tu kwa antibiotic. Ni mara chache sana UTI ikashambulia eneo la juu la figo. Hii ikitokea utahitaji kupigwa sindano za antibiotics.

Usipuuze dalili mbaya hata sku moja. Nenda hospital endapo utaanza kupata dalili hizi

 • homa kali
 • mwili kutetemeka
 • kichefuchefu na kutapika
 • maumivu makali chini ya kitovu na pande za kulia na kushoto

Mimba

Kwa mwanamke mjamzito kutokwa na vitu vyeupe kwenye uke ni jambo la kawaida endapo hakuna dalili zingine mbaya. Uchafu mweupe kitaalamu leukorrhea hutolewa ili kusafisha uke na kuzuia mjamzito asipate maambukizi. Uchafu huu ni mwupe, mwembamba usio na harufu mbaya.

Muone daktari haraka endapo utaanza kupata uchafu mweupe wa kuganda kama maziwa, hii inaashiria fangas. PIa ukipata uchafu mweupe na wenye harufu wakati una mimba, mwone daktari.

Mawe kwenye figo

Mawe ya figo ni matokeo ya mkusanyinko wa madini ya calcium na tindikali ya uric kupita kiasi. Mkusanyiko huu hupelekea vitu vigumu vyeupe kwenye figo na kibofu pia.

Endapo una vijimawe vidogo, vitameguka na kupenya mpaka kwenye kibofu, kisha kutolewa kwa njia ya mkojo. Kama mawe ni makubwa sana inaweza kuhitajika upasuaji kuyaondoa, ama utumie tiba asili.

Dalili zingine kwamba una mawe kwenye figo ni pamoja na

 • kupata haja ndogo mara kwa mara
 • maumivu eneo la tumbo kushoto au kulia na kwenye kibofu
 • mkojo mchafu wenye harufu mbaya
 • kukojoa damu
 • kutapika na kichefuchefu
 • homa kali

Magonjwa Ya Zinaa

Haya ni magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya tendo, na yanapelekea utokwe na usaha kwenye mkojo. Unaweza kupata maambukizi haya hata kwa kunyonya uke au uume. Magonjwa haya ni kama kisonono, kaswende, trichomoniasis, ukimwi nk.

Dalili za magonjwa ya zinaa

Pale unapoenda kukojoa, uchafu unatoka na kumwagika chooni, na kufanya mkojo kuwa wa mawingu ama usaha.

Wanaume hupata dalili chache sana wakiwa na magonjwa haya ya zinaa. Dalili kwa wanaume ni pamoja kupata mkojo wa kuchoma na maumivu makali.

Wanawake ukiacha kutokwa na vitu vyeupe wanapata, muwasho ukeni na maumivu ya nyonga.

Kama unahisi ulikutana kimapenzi na mtu usiyemwelewa, nenda hospitali upime magonjwa ya zinaa. Magonjwa mengi yanatibika vizui hospital.

Sababu za kutokwa usaha na vitu vyeupe kwa wanawake tu

Kuugua UTI kirahisi

Kutokana na maumbile ya mwanamke, wanaugua kirahisi sana magonjwa ya njia ya mkojo. Mambo mengine yanayowahusu wanawake tu ni pamoja na

Yai kupevuka(ovulation)

Wakati wa siku za hatari, mwili wa mwanamke huzalisha kwa wingi ute mweupe wa kuvutika kwenye mlango wa kizazi. Ute huu unasaidia mbegu kuogelea ili kutubisha yai.

Kabla ya ovulation, unaweza kupata ute ute ambao siyo wa kuvutika. Na ute huu waweza kutoka hata wakati wa kukojoa, na ni kawaida. Endapo utapata uchafu wenye harufu mbaya, wa kijani ama wenye damu , hiyo ni hatari unatakiwa uomwone daktari mapema.

Ukuaji wa Bakteria wabaya kupita kiasi(bacterial vaginosis)

Vaginosis ni kuvimba kwa eneo la uke kutokana na mazingira ya uke kuvurugika. Sababu kubwa inayopelekea kuvurugika kwa mazingira ya uke ni kufanya ngono na wanaume tofautitofauti.

Wanawake pia wasiofanya ngono mara kwa mara wanaweza kupata tatizo hili kutokana na mabadiliko ya homoni na kusafisha uke kupita kiasi.

Dalili zingine zinazoonesha una bacterial vaginosis ni pamoja na

Fungus Ukeni

Fungus kwenye uke ni matokeo ya kukua kupita kiasi kwa vimelea wa candida. Dalili kubwa ya fungus ukeni ni uchafu mzto usio na harufu kama maziwa mtindi. dalili zingine za fangas ukeni ni pamoja na

 • muwasho
 • kuungua nyakati za kukojoa au tendo
 • uke kuwa mwekundu
 • kuvimbe uke na
 • maumivu wakati wa tendo

Kama una fungus ukeni daktari anaweza kukupa cream ya kupaka ama vidonge vya kuweka ukeni. Pia unaweza kununua dawa zingine kwenye duka la dawa karibu yako. Endapo tatizo ni sugu daktari anaweza kukupa dawa za kumeza kama fluconazole.

Kukojoa Usaha na Vitu Vyeupe Kwa Wanaume tu.

Mbegu kurudi ndani(retrograde ejaculation)

Wanaume wenye tatizo hili hawatoi mbegu baada ya kufika kileleni yani dry orgasms. Ukiwa na tatizo hili mbegu badala ya kutoka nje , zinarudi ndani kwenda kwenye kibofu cha mkojo. Tatizo linatokana na msuli wa kwenye mrija wa mkojo kutofunga vizuri wakati wa tendo. Hali hii yaweza kupelekea baadae ukojoe vitu vyeupe ambavyo ni mbegu.

Japo wanawaume wengi hupata hii hali, na yaweza isiwe tatizo kubwa ila itakukwamisha kumpa mwanamke mimba.

Tembelea hospitali edapo unashindwa kumpa mwanamke mimba na una hilo tatizo. Daktari atakupa dawa za kumeza wakati wa tendo ili kusaidia msuli kufunga.

Tezi Dume

Maambukizi ya bakteria kwenye tezi dume yanaweza kupekelea tezi kuvimba kupita kiasi. Tezi ikiathiriwa yaweza kupelekea uchafu mweupe utakaovuja kwenye njia ya mkojo. Dalili zingine za shida kwenye tezi dume ni pamoja na

 • kushindwa kukojoa vizuri
 • maumivu wakati wa kukojoa
 • maumivu ya tumbo la chini, mkundu na chini ya mgongo
 • homa
 • mkojo wenye harufu kali
 • maumivu wakati wa kukojoa
 • uume kutosimama na kushindwa kabisa kufanya tendo na
 • kukosa hamu ya tendo

Hitimisho kwa tatizo la Kukojoa Usaha

Kama utaona chembechembe nyeupe kwenye mkojo, inaweza kuwa ni maji ya via vya uzazi, shida kwenye njia ya mkojo, figo na hata maambukizi. Kama utapata dalili mbaya zaidi, utahitaji kumwona daktari haraka kupata vipimo na tiba

Bofya kusoma makala zinazofuata kuhusu

Kwa nini unapata Kaswende sugu na

Dalili za Kisonono