Jinsi ya Kubana Misuli ya Uke Uliolegea

kubana misuli ya uke kupitia mazoezi
mabadiliko ya uke

Ni shauku ya kila mwanamke kutaka kufahamu namna gani wanaweza kubana misuli ya uke uliolegea ili wafurahie tendo la ndoa na kuwafurahisha wenzi wao.

Kuna vitu vikubwa viwili vinavyofanya uke wako kulegea. Umri na kuzaa. Kufanya tendo la ndoa mara kwa mara siyo sababu ya uke wako kulegea.

Wanawake waliojifungua kwa njia ya uke zaidi ya mara moja misuli yao ya uke inalegea sana. Na pia kadiri umri wako unavoenda unafanya misuli ya uke kulegea taratibu hata kama hukuwahi kuzaa.

Umri Mkubwa

Unapofika miaka ya 40 utaanza kuona utofauti kwenye misuli ya uke wako. Hii ni kutokana na kupungua kwa uzalishaji wa homoni ya estrogen. Kupungua kwa homoni ya estrogen kunafanya tishu za uke wako kusinyaa, kukauka na kutovutika. Hiki itakuwa ni kiashiria kwamba sasa unakaribia kukoma hedhi.

Kuzaa

Ni jambo la kawaida kabisa kwa uke kulegea baada ya kuzaa,kwasababu misuli ya uke inatanuka sana ili kuruhusu mtoto kuzaliwa.
Baada ya kuzaa utagundua kwamba uke wako siyo wa kawaida kama ulivozoea.

Hii ni kawaida na isikupe hofu kabisa. Uke wako utaanza kurejea katika hali yake ya kawaida siku chache baada ya kujifungua, japo hautarudi kama mwanzo.

Uke Kulegea Baada ya Kukoma Hedhi

Kukoma hedhi ama menopause huleta mabadiliko makubwa kwenye mwonekano wa uke wako. Kiwnago cha homoni ya estrogen kinapungua sana, kuingiliwa na mwanaume itakuwa changamoto maana itaambatana na maumivu makali. Katika hatua hii mashavu ya uke yatasinyaa sana kuliko ulivokuwa binti. Tumia vilainishi vinavyoruhusiwa ili ufurahie tendo la ndoa.

Kama hutapendezwa na kutanuka kwa uke wako usihofu, kuna baadhi ya Mazoezi unaweza kufanya ili kubana misuli ya uke wako baada ya kujifungua.

Jinsi ya Kubana Misuli ya Uke Uliolegea

Mazoezi ya nyonga ni moja ya mazoezi mazuri zaidi katika kukaza misuli ya uke wako. Mazoezi haya yanalenga kuimarisha misuli ya kibofu cha mkojo, mkundu, utumbo mdogo na kizazi pia.

Misuli ya uke inapolegea utaanza kuona dalili kama

  • mkojo kutoka pasipo ridhaa yako
  • kujisikia haja ndogo kila mara
  • kupata maumivu eneo la nyonga
  • kujamba ukeni wakati wa tendo na
  • kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa

Pamoja na kwamba mazoezi haya ya nyonga yatakusaidia kukaza misuli ya uke, siyo tiba kwa changamoto kubwa kama fistula, ambapo mwanamke anatokwa na haja ndogo na kubwa bila kujizuia. Fistula inatibika bure na wahitaji kufanyiwa upasuaji mdogo tu hospitali.

Mazoezi ya Kubana Misuli ya Uke ni pamoja na

Zoezi la Kegel kubana misuli ya uke

Muda mzuri wa kufanya zoezi hili ni pale unapoenda haja ndogo. Wakati wa kukojoa ndipo unaweza kutumia misuli inayotakiwa. Kama utafanikiwa kubana misuli sahihi wakati unakojoa na ukagundua mabadiliko kwenye speed ya mkojo basi hapo umepatia zoezi.

Wakati unakojoa bana misuli ya ndani ya uke ili kuzuia mkojo usitoke. Bana mkojo wa sekunde 10 kisha uachie kwa sekunde kadhaa bana tena. Mwanzo utakuwa mgumu lakini usikate tamaa endelea kufanya mpaka upatie zoezi. Usifanye kila muda unapoenda kukojoa ila jitahidi ufanye mara 4 kwa siku.

Njia ingine ya kufanya zoezi la kegel

Kama utashindwa kufanya zoezi wakati wa kukojoa basi unaweza kujaribu njia ingine kwa kuingiza kidole ukeni mpaka ndani na ujaribu kubana misuli ya uke uone kama kidole kinabanwa. Fanya zoezi hili awamu 5 kila unapokojoa au unapoingiza kidole. Na ufanye mara tano mpaka 10 kwa siku.

Kama ilivo kwa mazoezi mengine, unavofanya zaidi kila siku unapata uzoefu na ndivyo unazopatia zaidi.

Pelvic Tilt Exercise ili Kubana Misuli ya Uke

Kukaza misuli ya uke wako kupitia zoezi hili fanya haya

  1. simama wima na makalio yako yaegemee ukuta.
  2. vuta tumbo kwa ndani. Unapofanya hivi mgongo wako utanyooka kuelekea kwenye ukuta
  3. bana tumbo lako kwa muda wa sekunde 4 kisha jiachie
  4. fanya hivi mara 10 na awamu tano kwa siku nzima.

Hitimisho Kuhusu Kukaza Uke

Fahamu tu kwamba maumbile yanatofautiana kwa kila mwanamke . Kwahivo usijilinganishe na rafiki yako nawe ukataka kuwa kama yeye. Kama ukiona mabadiliko kwenye uke wako yanayokufanya usifurahie tendo la ndoa, nenda hospitali onana na daktari atakupa ushauri wa kina.

Hutakiwi kuvumilia maumivu wakati unafanya tendo eti ili tu umridhishe mme wako hapana. Matatizo mengi yanafanya uke kuwa mkavu yanaweza kutibika. Kama una mashaka na uke wako muone daktari mapema kupata suluhisho.

Wasiliana nasi kupitia whatsapp namba 0678626254.

Bofya kusoma makala inayofuata kuhusu aina za harufu ukeni, fahamu kama harufu yako ni salama au siyo salama.