Chanzo Cha Ukavu Ukeni

ukavu ukeni
mfano wa uke

Nini kinasababisha ukavu ukeni? Uke umeumbwa kwa mashavu yenye kuta zenye tishu laini sana. Na kufunikwa na majimaji yenye utelezi ili kusaidia mbegu za kiume kuogelea vizuri na kurutubisha yai wakati wa tendo la ndoa.

Uteute huu pia ni kilainishi cha uke kupunguza msuguano wakati wa tendo la ndoa.

Kadiri mwanamke anavozeeka mabadiliko ya uzalishaji wa vichocheo ama homoni vinapelekea kuta za uke kusinyaa na kuwa dhaifu. Kuta zikisinyaa maana yake seli zinazozalisha uteute zinapungua na hivo kupelekea ukavu ukeni.

Mabadiliko ya homoni ndio sababu kubwa inayokufanya uwe na uke mkavu.

Nini Madhara ya Ukavu Ukeni?

Kukauka kwa uke wako kunaweza kusababisha madhara kama

Nini Kinapelekea Ukavu ukeni?

Kupungua kwa homoni ya estrogen ndipo chanzo kikubwa cha ukavu ukeni. Wanawake wote hupungua uzalishaji wa estrogen kadiri wanavozeeka na kukaribia kukoma hedhi yaani menopause.

Menopause siyo chanzo pekee kwani kuna vitu vingine vinavyopelekea uwe na uke mkavu. Mambo mengine yanayopunguza uzalishaji wa estrogen ni pamoja na

 • kunyonyesha
 • kuvuta sigara
 • kuzaa
 • upasuaji kuondoa mifuko ya mayai(ovary)
 • stress kupita kiasi
 • maozezi makali sana
 • sonona
 • magonjwa ya kinga na
 • baadhi ya tiba kama chemotherapy na radiotherapy

Lini Unatakiwa Kumwona Daktari?

Ni mara chache sana ukavu wa uke iwe ni kiashiria cha tatizo kubwa la kiafya. Muhimu ni kutafuta ufumbuzi wa daktari endapo tatizo lako limechukua muda mrefu . Endapo usipotibia mapema ukavu wa uke unaweza kusababisha kumeguka kwa kuta za uke.

Matibabu ya Tatizo la Ukavu Ukeni

Kuna aina nyingi za tiba ambazo waweza kuzipata famasi ya karibu yako ili kulainisha uke. Tiba hizi zinakuwa kwenye mfumo wa jelly mfano KY jelly ni maarufu sana.

Hakikisha unatumia vilainishi vya maji siyo vya mafuta. Vilainihsi hivi visiwe na manukato wala kemikali hatarishi.

Kamwe usitumie mate kama kilainishi wakati wa tendo la ndoa kwani unaweza kupata maambukizi ya bakteria. Usitumie mafuta ya kujipaka kama kilainishi kwani utaharibu kuta za uke.

Nawezaje Kuzuia tatizo hili kujitokeza mara kwa mara

 • kunywa maji ya kutosha kila siku
 • usitumie sabuni wa marashi ukeni
 • ongea na mwenzi wako kuhusu tatizo ili akuvumilie wakati unatafuta tiba.

Tumia Vidonge Asili vya Evecare kurejesha uteute mzuri.

evecare

Evacare ni tiba asili iliyo kwenye mfumo wa vidonge. Ni dawa zinazozalishwa nchini India kutibu changamoto za wanawake kama ukevu ukeni, upungufu wa ute, hedhi kuvurugika na maumivu makali kwenye hedhi. Dozi moja ina vidonge 30, unatumua kwa week mbili. Kulingana na ukubwa wa tatizo lako tunaweza kushauri utumie zaidi ya dozi moja.

Vidonge vimetengenezwa kitaalamu kupitia muunganiko wa mimea na kuhifadhiwa vizuri ili kutunza uasili wa dawa pasipo kuwekwa kemikali.

Gharama ni Tsh 75,000/=
Tuandikie whatsapp no: 0678626254 kuanza Tiba.

Bofya kusoma makala inayofuata: Aina za harufu ukeni

7 replies on “Chanzo Cha Ukavu Ukeni”

Samahani, kama tatizo la ukavu ukeni limetokea, je kuna uwezekano wa kushika mimba?

Me na hilo taizo na nikiwa nasex natumia mafuta au mate japo nasex kila baad ya miez kazaa kutokana mume wangu yupo mbali je naweza pata madhara

Leave a Reply

Your email address will not be published.