Dawa ya Artovastin kupunguza cholesterol

dawa ya artovastin
artovastin

Dawa ya Artovastin ni moja ya dawa zinazotolewa hospitali kupunguza mafuta mabaya kwenye mwili yaani cholesterol. Pamoja na dawa hii, daktari anaweza kukushauri kurekebisha lishe yako na mtindo wa maisha ili uweze kupona mapema.

Artovastin ipo miongoni kwa kundi la dawa zinazoitwa ‘statins’. Zinafanya kazi kwa kupunguza mafuta yanayozalishwa na ini.

Kitendo cha kupunguza mafuta mabaya na kuongeza mafuta mazuri mwilini kunapunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na stroke. Pamoja na dawa, ni muhimu pia kurekebisha mtindo wa maisha, mfano kuweka ratiba ya kufanya mazoezi walau mara tatu wa wiki.

Jinsi ya kutumia dawa ya artovastin

Hakikisha unasoma karatasi ya maelekezo inayopatikana kwa mtoa huduma za dawa, kabla hujaanza kumeza artovastin. Kama una maswali yoyote, muulize daktari akupe ufafanuzi. Meza dawa aidha kabla au baada ya kula, kila siku kama daktari alivyokwelekeza.

Dozi yako itategemea na ukubwa wa tatizo lako na historia ya ugonjwa, umri na pia kama kuna dawa zingine unatumia. Hakikisha tu unamweleza daktari au mudumu duka la dawa, endapo una dawa zingine unatumia au tiba asili.

Muhimu kuzingatia wakati wa dozi

Epuka kutumia zabibu wakati unatumia artovastin, labda tu kama daktari amelekeza vingine. Zabibu zinaweza kuongeza kiwango cha dawa kinachofonzwa kwenye damu na kuleta shida zaidi.

Kama kuna dawa zingine unameza za kupunguza cholesterol, meza artovastin saa moja kabla au masaa manne baada ya kumeza artovastin.

Meza dawa muda ule ule kila siku ili kupata matokeo mazuri. Kumbuka kumeza muda sawa kila siku na endelea kumeza dawa mpaka umalize, hata kama umeanza kujisikia vizuri. Wagonjwa wengi wenye cholesterol huwa kwenye hali nzuri na wanaendelea na shughuli zao.

Ni muhimu sana kuendelea kufatilia ushauri wa daktari kwenye lishe na mazoezi. Inaweza kuchukua mpaka wiki nne kupata matokeo mazuri zaidi ya dawa hii.

Matokeo hasi na madhara ya kutumia dawa ya artovastin

Fahamu tu kwamba daktari amekupa dawa hii baada ya kujiridhisha kwamba dawa itakusaidia. Daktari amepima madhara ya dawa ni madogo kwako kuliko faida utakayopata. Watu wengi wanaotumia dawa hii hawapati madhara yoyote.

Watu wachache sana wanaotumia artovastin wanaweza kupata chagamoto ya kumbukumbu na kushindwa kufanya maamuzi. Pia dawa inaweza kupelekea kisukari. Endapo dalili hizi zitajitokeza, muone daktari haraka.

Dawa yaweza kuleta matatizo ya misuli kwa watu wachache sana. Mjulishe daktari endapo utapata dalili zisizo za kawaida kama mumivu ya misuli, misuli kuchoka, dalili za ahari kwenye figo kama mabadiliko ya kiwango cha mkojo.

Dawa pia inaweza kusababisha matatizo kwnenye ini kwa baadhi ya watu. Kama ukiona dalili za kuathirika ini mfano macho na ngozi kuwa ya njano, mkojo mweusi zaidi, maumivu makali pembeni ya tumbo na kutapika mfululizo, muone daktari.

Pia dawa yaweza kuleta aleji kwa mtumiaji. muhimu upate ushauri wa daktari mapema, endapo utaona dalili za aleji kama kuvimba ulimi, uso au koo, kushindwa kupumua vizuri, kuota vipele na kujikuna baada ya kumeza dawa.

Tahadhari wakati wa kutumia artovastin

Kabla ya kuanza kutumia artovastin, mjulishe daktari au mfamasia kaa una aleji yoyote. Dawa ahii ina viambata hai ambayo vyaweza kupelekea mpambano ndani ya mwili.

Mjulishe pia daktari kama una historia ya kuugua magonjwa ya figo, ini na kama unatumia pombe.

Kabla ya kufanyiwa upasuaji, mjulishe daktari endapo upo kwenye matumizi ya artovastin.

Punguza matumizi ya pombe. Kunywa pombe kila siku, kunaongeza hatari ya kuugua magonjwa ya ini hasa ukiwa kwenye dozi ya artovastin.

Soma hapa kuhusu vyakula vya kupunguza cholesterol