Kitanzi na Fungus Ukeni

Nini Maana ya Kitanzi?

fungus ukeni
kitanzi

Kitanzi kwa lugha ya kitaalamu intrauterine device(IUD) ni njia ya kisasa kupanga uzazi kwa muda mrefu. Ni kifaa kidogo chenye umbo la herufi T, ambacho huchomekwa kwenye kizazi kupitia njia ya uke. Vitanzi hutengenezwa kwa plastic ama madini ya copper. Leo tutaona jinsi kitanzi kinavoweza kuleta fungus ukeni.

Aina za kitanzi

Kuna aina mbili za kitanzi. Kitanzi cha copper na kitanzi cha homoni (hormonal IUD). Kitanzi cha homoni kinaweza kukukinga usishike mimba kwa miaka mitatu mpaka mitano. Wakati kitanzi cha copper kinaweza kukukinga usishike mimba mpaka miaka kumi au zaidi.

Kuna Faida nyingi sana za kutumia kitanzi. Kwanza ni simple ukiweka umeweka, siyo kama vidonge kila siku ukumbuke kumeza.

Kumbuka kwamba ukihitaji kuzaa wala hakuna changamoto, unaenda tu kwa esi au daktari hospital anakitoa. Na baada ya miezi ama week kadhaa unashika mimba.

Hatua za kuweka kitanzi

Kwanza daktari au nesi anayekuhudumia anatakiwa kuweka kitanzi ndani kabisa ya kizazi. Kabla kitanzi kuweka kinakuwa kimenyooka na chenye kamba zinazonin’ginia mwishono.

Zifuatazo ni hatua ambazo muhudumu anazifuata wakati wa kukuwekea kitanzi

  1. Utapimwa kizazi chako kama kinafaa kutumia kitanzi, kisha muhudumu anapaka dawa ya kuua vimelea kwenye uke, na kisha atapitisha kitanzi kwenye mlango wa kizazi mpaka kwenye kizazi
  2. Daktari akishajiridhisha kwamba kitanzi kimegusa mwisho wa kizazi, atakitanua ili kitengeneze umbo la T. Hapo unaweza kupata maumivu kwa mbali
  3. Baada ya hapo daktari atakata zile kamba zibaki fupi. Kamba kidogo zitabaki kunin’ginia kwenye eneo la mlango wa kizazi.

Nini kinatokea baada ya kuwekewa kitanzi?

Baada ya kitanzi kuwekwa mahali pake, utapata maumivu kwa mbali na kisha utakuwa sawa. Kumbuka zoezi linachukua dakika chache tu, wala huhitaji kulazwa.

Unaweza kupata matone kidogo ya damu siku kadhaa mbele baada ya kuwekewa kitanzi. Daktari atakwambia lini urudi tena kliniki ili kukuchunguza endapo kuna mabadiliko zaidi.

Namna Kitanzi Kinafanya Kazi

Kitanzi kinafanya kazi kwa kufanya ute wa ukeni kuwa mzito sana, na hivo kuzuia mbegu kurutibisha yai. Yani ute huu unakuwa kama neti inavozuia mbu.

Pia kitanzi kinafanya ukuta wa kizazi uwe mwembamba sana, kiasi kwamba kiumbe hakiwezi kujshikiza pale. Na pia kitanzi kinafanya mayai pia yasipevuke.

Je kitanzi kinaweza kupelekea uugue fungus ukeni?

Kwa mtu ambaye anaugua fungus mara kwa mara kabla hajaanza kutumia kitanzi, na pia kama uliugua magonjwa mengine ya zinaa, itakuwa rahisi sana kuugua ukianza kitanzi.

Kwa wanawake wengine ambao hawaugui mara kwa mara ni ngumu kupata fungus hata baada ya kuweka kitanzi. Ni baadhi tu ya wanawake hupata fungus na hii ni kwasababu kitanzi huwa kinabadili mazingira ya uke.

Dalili mbaya zinazoashiria kuna maambukizi ukeni

Endapo unapata dalili hizi, hakikisha unamwona daktari mapema.

Makundi yasiyotakiwa kutumia Kitanzi

Japo kitanzi ni njia ya kisasa kupanga uzazi, haifai kwa kila mwanamke. Hutakiwi kutumia kitanzi endapo

  • una magonjwa ya zinaa ambayo hayajatibiwa
  • mgonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi na kizazi kwa ujumla
  • una matatizo kwenye kizazi chako kiasi inakuwa ngumu kwa daktari kukipachika mfano kizazi kuinama
  • mgonjwa ini
  • una mimba

Je vipi kama sitashika mimba mapema?

inatokea kwa wanawake wachache kupata madhara ya kitanzi, hasa kuvurugika kwa mazingira ya kizazi na hivo mimba haiingii. Kwa grupu hili la wanawake tunawashauri kutumia hizi tiba asili ili kusafisha kizazi na kusaidia mayai kupevuka.

Bofya hapa kuanza tiba ya uzazi.

Asilimia 90 ya wanawake tuliowapa dawa hizi walishika mimba ndani ya miezi miwili. Huwezi kujua pengine na wewe ukawa mmoja wa mashuhuda wetu.

Nawezaje kujizuia nisipate fungus ukeni nikiwa natumia kitanzi?

Kitanzi kwa kiasi kikubwa hupelekea maambukizi hasa kwenye week chache za mwanzoni tu. Lakini pia muhimu utambue kitanzi siyo njia ya kukuzuia usipate magonjwa ya zinaa. Njia nzuri ya kujizuia usipate magonjwa ya zinaa ni kutumia condom kwa kila tendo.

Pia unaweza kuzuia kupata maambukizi kwa kuacha kuosha uke mpaka ndani. Uke wako una bakteria wazuri na unajisafisha wenyewe. Kuosha uke mpaka ndani kunavuruga mazingira ya uke na kuongeza hataru ya kupata fungus.

Hakikisha unamwona daktari mapema endapo umegundua kuna viashiria vya maambukizi. Ukipata tiba mapema chansi ya kupona ni kubwa zaidi.

Bofya kusoma kuhusu Aina za Uchafu Ukeni