Vyakula vya kuepuka kwa mjamzito

Jambo kubwa sana kwa mjamzito huwa ni kuafahamu vyakula gani na vinywaji hawatakiwi kula na kunywa ili kulinda afya ya mtoto aliye tumboni.

Habari njema ni kwamba kuna kundi kubwa sana la vyakula unaloweza kula kuliko vyakula ambavyo hutakiwi kuvitumia. Hakikisha unakuwa mwangalifu sana wakati huu wa ujauzito maana siyo kila kitu ni cha kupeleka tumboni. Baadhi ya vyakula watakiwa kupunguza kula na vingine usile au kunywa kabisa ni kama

Samaki wenye kiwango kikubwa cha mercury

Mercury ni madini sumu ambayo yakiingia mwilini yanabadili vinasaba na kuharibu kinga na mifumo ya mwili. Madini haya huzalishwa zaidi viwandani. Samaki wengi tunaokula wanapatikana kwenye maziwa na bahari ambapo taka nyingi za viwandani humwagwa.

Kutokana na hali hiyo samaki wakubwa wanaopatikana baharini au kwenye maziwa wana kiwango kikubwa cha madini ya mercury, kwasababu samaki hawa wanakula samaki wadogo wengi. Kwahivo ni vizuri kuepuka kula samaki wakubwa wa baharini na hata ziwani unapokuwa mjamzito na wakati wa kunyonyesha.

Nyama Isiyopikwa vizuri na Kuiva

Kula nyama isiyoiva vizuri kunakuweka kwenye hatari ya kupata bakteria na vimelea wengine wabaya ikiwemo E.coli na Salmonella.
Bakteria wanaweza kusababisha ukajifungua mtoto njiti au magonjwa ya ubongo kwa mtoto atakayezaliwae. Mwanamke mjamzito hatakiwi kula nyama mtaani labda awe amehakikisha kwamba nyama husika imechomwa ama kupikwa vizuri na kuiva.

Caffeine

Caffeine inapatikana sana kwenye vinywaji (energy drinks) na kwenye kahawa. Kwa mjamzito inashauriwa kupunguza ama kuacha kabisa kutumia vyakula na vinywaji vyenye caffeine kwa wingi. Mjamzito anapotumia caffeine hufyonzwa mpaka kwenye kondo la nyuma ambapo chakula na hewa hupita kwenda kwa mtoto.

Caffeine huathiri ukuaji wa mtoto na kuongeza hatari ya kujifungua mtoto akiwa na uzito mdogo sana chini ya kilo 2.5. Caffeine inapatikana zaidi kwenye chai ya rangi, energy drinks, soda na chocolate.

Matunda na Mboga Zisizooshwa Vizuri

Ngozi ya matunda na mbogamboga ina vimelea wengi wabaya pamoja na bakteria hatari kama E.coli, Salmonella,na Toxoplasama. Vimelea hawa ni hatari kwa afya ya mtoo kwani wanaweza kulepekea hata upofu, na athari kwenye ubongo.

Nunua apple cider vinegar kuoshea matunda. changanya nusu kikombe cha vinegar kwa maji lita moja kisha osha matunda na mboga zako vizuri kabla ya kuhifadhi kwenye friji.

Pombe

Inashauriwa uacha kabisa kutumia pombe hata kwa kuonja tu kama tayari unajua una ujauzito kwani inaongeza hatari ya mimba kuharibika na kuzaa mtoto njiti. Hata kiwango kidogo tu cha pombe kinaweza kuwa na athari kwenye ubongo wa mtoto.

Kunywa pombe kwa mjamzito pia kunaweza kusababisha mtoto kuzaliwa kuwa na uso wa tofauti na matatizo ya moyo.

Vyakula vilivyosindikwa (Processed junk foods)

Katika muda mzuri zaidi wa kubadili lishe yako na kuachana na lishe mbovu, ni muda huu ukiwa mjamzito. Maana ni muda pekee ambapo una sababu ya msingi ya kubadili lishe na kujifunza kupika ukiwa nyumbani kwako.

Achana na vyakula vya mtaani kama chips, mishkaki, baga, sosage na mayai ya kisasa yanaharibu tu shepu yako na pia kumkosesha mtoto virutubisho muhimu.

Vyakula vingi vilivyosindikwa vina upungufu wa virutubisho na pia vina sukari nyingi sana itakayokuongezea uzito kupita kiasi. Uzito mkubwa sana kwa mjamzito unakuweka kwenye hatari ya kupata shinikizo la damu na kisha kifafa cha mimba.
anza leo kwenda sokoni, fanya shopping kisha pika na ule chakula cha vyumbani kwako unachopendelea.

Bofya kusoma kuhusu: Namna ya kulala kwa mjamzito