Presha ya Macho, Maelezo, Vipimo na Tiba

Presha ya macho ni nini?

Eneo la mbele la macho yenye limejaa majimaji. Pale majimaji haya yasipomgwa vizuri nje ya macho yako katika mfumo wa machozi, presha inapanda kwenye macho. Presha hii huitwa kitaalamu ocular hypertension ama presha ya macho.

Presha ya macho inaweza kupelekea kukatika kwa mawasiliano kati ya jicho na ubongo na kusababisha upofu. Ndio maana kuna umuhimu wa kufanya vipimo vya macho kila mara, kugundua tatizo mapema na kulitibu.

Makala hii itaandika kwa kina chanzo cha tatizo la presha ya macho na namna linavyotibiwa.

Nini maana ya presha ya macho?

Presha ya macho ni pale shinikizo la ndani ya jicho linapokuwa kubwa zaidi pasipo kutokea majeraha yoyote. Jicho moja ama yote yanaweza kuathiriwa na tatizo hili.

Mgonjwa anatambulika kama ana presha ya jicho endapo

  • presha ya jicho inazidi kiwango cha 21 mmHg na
  • hakuna dalili za majeraha kwenye jicho wala kupungua uwezo wa kuona

Nini kinapelekea presha ya macho?

Eneo la mbele la jicho limejaa majimaji yanayoitwa aqueous humor. Kazi ya majimaji haya ni kuleta unyevunyevu kwenye tishu laini za jicho na kuweka sawa shepu ya jicho.

Kwasababu jicho linazalisha majimaji haya muda wote, yatakiwa mengine yamwagwe nje kama machozi. Endapo majimaji haya hayatolewi ipasavyo, yataanza kujikusanya na kujaa. Hii inaongeza mgandamizo ndani ya jicho na kupelekea presha ya jicho.

Mazingira hatarishi yanayopelekea presha ya Jicho

Kila mtu anaweza kukutwa na tatizo la presha ya jicho. Japo makundi haya hapa chini wapo kwenye hatari zaidi ya kuugua tatizo

  • wenye presha ya kupanda ya damu na kisukari
  • Kama familia yako ina historia ya kuugua upofu ama presha ya macho
  • wenye umri zaidi ya miaka 40
  • uliwahi kufanyiwa upasuaji wa macho ama majeraha kwenye macho
  • matumizi ya muda mrefu ya dawa za kupunguza mpambano ndani ya mwili (steroid medications)
  • watu wenye matatizo ya macho kama kushindwa kuona mbali.

Je presha ya macho huonesha dalili?

Presha ya macho haina dalili zozote. Kutokana na hili, inawezekana kabisa ukawa unaugua na hujui kama una tatizo. Hii ndio sababu kwanini unatakiwa kufanya vipimo vya macho mara kwa mara.

Vipimo kugundua presha ya Jicho

Daktari atatuma kipimo cha haraka kupima presha ya jicho, kipimo hiki huitwa tanometry.

Pamoja na kipimo cha tanometry, daktari ata kucheki kuona kama kuna dalili za kukatika mawasiliano kati ya jicho na ubongo (glaucoma). Vipimo hivi vinatazama neva za fahamu zinapelekea taarifa kwenye ubongo.

Tiba ya presha ya macho

Presha ya jicho hutibiwa kupitia dawa za matone ambazo zitasaidia, majimaji yaliyozidi yatolewe ama kupunguza kiwango kinachozalishwa cha majimaji ya jicho.

Daktari atakujulisha kuendelea kurudi hospitali katika wiki kadhaa zijazo ili kuona kama dawa inafanya kazi.

Lakini pia kwasababu presha ya jicho inaweza kusababisha kukatika kwa neva, ni muhimu kuendelea kupima macho kwa kipindi cha miaka mwili.

Upasuaji kwa presha ya macho

Kwa baadhi ya wagonjwa, tatizo la presha ya macho linaweza lisiishe kwa dawa pekee. Kwa hali hii upasuaji unaweza kuhitajika ili kupunguza presha ya ndani.Lengo la upasuaji ni kutengeneza tundu la kusaidia majimaji yaliyozidi yalotewe.

Kama umependezwa na huduma yetu na unahitaji kutuchangia chochote ili tuendelee kutoa zaidi elimu hii, Wasiliana nasi kupitia whatsapp namba 0678626254.

Soma zaidi kuhusu: Mtoto wa jicho

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *