Ukuaji wa mimba hatua kwa hatua kila mwezi

mimba
ukuaji wa mtoto tumboni

Ndani ya masaa 24 baada ya urutubishaji kufanyika, yai ambalo baadae ndipo itakuwa mtoto, huanza kugawanyika kwa kasi sana na kuwa seli nyingi za mwili. Kufikia wiki nane, jina la mtoto kitaalamu litabadilika kutoka kuitwa embryo mpaka fetus. Kuna wiki karibu 40 kutoka kushika mimba mpaka kujifungua kwa mimba ya kawaida. Wiki hizi hugawanywa katika mihula mitatu (trimesters). Leo utajifunza ukuaji wa mtoto katika kila mwezi mpaka pale mwanamke anapojifungua.

Mimba inaanza kuhesabika lini?

Mimba huanza kuhesabiwa siku ya kwanza ya hedhi yako ya mwisho. Kipindi hiki huitwa gestational age au menstrual age. Ni kipindi cha karibu wiki mbili kuelekea kwneye siku ya hatari uliposhika mimba. Pengine hii yaweza kukushangaza kidogo. Lakini siku ya kwanza ya hedhi yako ya mwisho ni muhimu sana katika kujua umri wa mimba yako. Muhudumu wa hospitali atakuuliza siku hii ili afanye makadirio ya umri wa mimba yako.

Mimba inafanyikaje?

Kila mwezi mwili wako unapitia mzunguko wa hedhi. Na katika mzunguko huu kuna siku za hatari za kushika mimba haraka. Mzunguko huu wa hedhi unaanza pale unapovunja ungo na kukoma kwenye miaka ya 40’s au 50’s.

Utolewaji wa yai lililokomaa unaanza hivi. Moja kundi la mayai machanga (oocytes) yaliyohifadhiwa kwenye mifuko midogo inayoitwa follicles huanza kukua. Kwenye kundi hili kubwa la mayai, yai moja pekee ndilo litapevuka na kuwa tayari kutolewa.

Ovulation

Mfumo wa yai uliopevuka vizuri unafunguka na kutoa yai kwenye kiwanda chako cha mayai cha ovary. Kitendo hiki huitwa ovulation. Ovulation inafanyika kama wiki mbili hivi kabla hujaanza hedhi yako. Ni kipindi kilicho katikati ya mzunguko wako.

Bada ya mfuko wa yai kufunguka na kutoa yai lililokomaa, kovu linalobaki huitwa corpus luteum. Kovu hili huanza kuzalisha vichocheo ama homoni za estrogen na progesterone. Kazi ya homoni ya progesterone ni kuandaa ukuta wa kizazi ili ubebe kiumbe. Endapo mimba haitaingia basi ukuta huu utabomoka ndipo utapata hedhi.

Kikawaida urutubishaji unafanyika wiki mbili baada ya hedhi yako ya mwisho. Mbegu ya kiume ikishapenya kwenye yai, kuna mabadiliko yanatokea haraka kwenye ukuta wa yai ili kuzuia mbegu ingine isiingie.

Jinsia ya mtoto wako huwa inategemea na aina ya mbegu iliyorutubisha yai. Mwanamke anabeba vinasaba vyenye XX na mwanaume XY kwenye mbegu. Kama mbegu ya kiume yenye X ikatutkana na yai la mwanamke, basi mtoto wa kike atafanyika. Na kama mbegu ya Y ikikutana na yai la mwanamke, mtoto wa kiume atafanyika.

Lini nitajua kama tayari nina mimba?

Pale tu mimba inapotungwa, homoni ya human chorionic gonadotrophin(hCG) huanza kuzalishwa na kupatikana kwenye damu na mkojo. Homoni hii huzalishwa na seli ambazo zinafanya kondo la nyuma(mrija wa chakula kwa mtoto). Pamoja na kwamba homoni hii huanza kuzalishwa mapema, inachukua walau wiki tatu kuweza kuonekana kwenye mkojo. Subiri wiki moja ipite baada ya kukosa hedhi ndipo upime mkojo.

Lini natakiwa kuanza clinic

Muhimu pale tu unapopima na kujua una mimba, kwenda hospitali. Ukifika hospitali ama kituo cha afya, muhudumu atakuuliza kama kuna virutubishi vyovyote unatumia. Virutubishi hivi hasa ni vitamini ya folic acid. Ni muhimu upate walau kiwango cha mcg 400 za folic acid kila siku wakati wote wa ujauzito. Hii itasaidia ukuaji mzuri wa ubongo na uti wa mgongo kwa mtoto.

Hatua za ukuaji wa mimba mwezi kwa mwezi.

Muhula wa kwanza (First trimester)

Muhula wa kwanza wa ujauzito unaanza siku ya kushika mimba mpaka wiki 12 za mwanzo. Katika kipindi hiki mtoto atabadilika kutoka kwenye grupu la seli mpaka kuwa kiumbe chenye shape kama za mtoto.

Mimba ya mwezi wa kwanza (wiki 1 mpaka 4)

Kadiri yai lililorutubishwa linavokua, puto lenye maji ndani yake litaanza kuumbika. Puto hili huitwa amniotic sac na maji ya ndani yake huitwa amniotic fluid. Kazi ya puto hili ni kumkinga mtoto dhidi ya ajali yoyote na kusaidia ukuaji wa mtoto.

Katika kipindi hichi, kondo la nyuma(placenta) pia huanza kujitokeza. Kondo la nyuma ni kiungo chenye umbo la duara, kazi yake ni kupitisha chakula na hewa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, na kurudisha taka kutoka kwa mtoto kwenda kwa mama.

Ndani ya wiki chache za mwanzo kichwa kitaanza kufanyika, uso na vidoti vyeusi kwenye macho. Mdomo na koo pia vitaanza kuumbwa. Moyo pia utaanza kuonekana ukidunda mara 65 kwa dakika katika wiki ya 4 ya mwezi wa kwanza. Mwishoni mwa mwezi wa kwanza mtoto wako atakuwa na urefu wa inch 0.25.

Mwezi wa pili (wiki ya 5 mpaka 8)

Uso wa mtoto wako utaendelea kuonekana zaidi. Masikio pia yataanza kuumbika kwenye pande za kichwa. miguu, mikono na macho pia huendelea kuumbwa.

Neural tube ambayo baadaye inaenda kuumba ubongo, uti wa mgongo na mfumo wa neva, inakuwa tayari imefanyika. Pia mifupa huanza kuundwa.

Katika mwezi huu kichwa cha mtoto kinakuwa kikubwa kuliko maeneo mengine ya mwili. Mpaka kufikia wiki ya 6 ya ujauzito, mapigo ya moyo ya mtoto yanaweza kutambulika kwa utrasound. Baada ya wiki ya 8 kiumbe hiki huitwa fetus, kutoka kwenye kuitwa embryo.
Mpaka kufikia mwisho wa mwezi wa pili tayari mtoto wako atakuwa na urefu wa inch moja na uzito wa gramu 0.9.

Mwezi wa tatu (week ya 9 maka ya 12)

Kufikia mwezi wa tatu, miko, vidole na kichwa tayari vimeumbwa kikamilifu. Kipindi hichi mtoto ataanza kidogo mazoezi kama kukunja na kukunjua vidole na mdomo pia. Kucha na masikio ya nje yanaaanza kuumbwa. Viungo vya uzazi vitaanza kuumbwa katika mwezi huu wa tatu lakini bado itakuwa ngumu kujua jinsia kwa utrasound.

Mpaka mwishoni mwa mwezi wa tatu, mtoto atakuwa amekamika kabisa kuumbwa. Viungo vyote na na miguu na mikono vtaendelea tu kukua. Pia mfumo wa usafirishaji na wa mkojo unaanza kufanya kazi. Ini pia la mtoto litaanz akuzalisha nyongo.

Kwasababu viungo vyote vya mtoto viakuwa vimeumbwa, uwezekano wa mimba kutoka unapungua sana baada ya mwezi wa tatu.

Muhula wa pili(Second trimester)

Muhula wa pili wa ujauzito inaamnika kwamba ni kipindi kizuri zaidi. Kufikia kipindi hichi zile dalili mbaya za kutapika, kichefuchefu (morning sickness), zinakuwa zimepungua sana au kusiha kabisa. Mtoto ataendelea kukua zaidi sura yake na pia utaanza kuhisi mtoto anacheza. Katika muhula wa pili ndipo unaweza kutambua jinsia ya mtoto wako kwa utrasound.

Mwezi wa 4 (wiki ya 13 mpaka 16)

Mapigo ya moyo ya mtoto yataanza kutambulika kupitia kipimo maalumu cha doppler. Vidole vya mikono na miguu tayari vimeumbwa. Macho, kope, nyusi na nywele za kichwa zimefanyika. Meno na mifupa inazidi kuimarika. Mtoto ataanza pia kunyonya dole gumba, kujinyoosha na kupiga miayo. Pia mfuko wa usafirishaji taarifa unaanza kufanya kazi. Viungo vya uzazi tayari vimeumbwa na daktari anaweza kuviona kupitia utrasound.

Kufikia mwishoni mwa mwezi wa 4, mtoto wako anakuwa na urefu wa inch 6 na uzito wa gramu 113.

Mwezi wa 5 (wiki ya 17 mpaka 20)

Kufikia mwezi huu utaanza kuhisi mtoto anacheza tumboni. Hapa mtoto anaanza kuimarisha misuli na hivo anaifanyia mazoezi.

Nywele zinaanza kukua kichwani kwa mtoto. Mabega ya mtoto wako pamoja na mgondo zinafunikwa na nywele laini zinaitwa lunago. Nywele hizi zinamlinda mtoto, na mara nyingi zinapotea unapokaribia kujifungua.

Ngozi ya mtoto inafunikwa na utando mweupe unaoitwa vernix caseosa. Utando huu unamlinda mtoto dhidi ya kuathriwa na kimiminika cha amniotic. Utando huu huisha kabla mtoto hajazaliwa.

Kufikia mwisho wa mwezi wa tano mtoto wako anakuwa na urefu wa karibu inch 10 na uzito wa karibu nusu kilo.

Mwezi wa 6 (wiki ya 21 mpaka 24)

Kama unaweza kutazama ndnao ya kizazi chako, basi utaona mtoto akiwa na ngozi nyekundu na mishipa ya damu ikionekana. Vidole vya mikono na miguu vinaonekana. Katika hatua hii mtoto ataanza kufumbua macho na kusikia muziki wa nje ukipigwa.

Kama mtoto atazaliwa kabla ya wakati wake, mtoto ataweza kuishi baada uangalizi mkubwa wa madaktari. Kufikia mwishoni mwa mwezi wa 6, mtoto wako atakuwa na urefu wa inch 12 na uzito wa kilo moja.

Mwezi wa 7 (wiki ya 25 mpaka 28)

Mtoto ataendelea kukua na kutengeneza hifadhi ya mafuta mwilini. Katika hatua hii uwezo wa mtoto kusikia unakuwa umekamilika. Mtoto ataaanza kubadili mkao kuelekeza kichwa kwenye mlango wa kizazi. Pia majimaji (amnitic fluid) yataanza kupungua.

Kama mtoto atazaliwa njiti kipindi hichi, anaweza kuishi. Mwishoni mwa mwezi wa saba, mtoto wako atakuwa na urefu wa inch 14 na uzito wa kilo 1 mpaka mbili.

Muhula wa tatu (Third trimester)

Hichi ni kipindi cha mwisho cha ujauzito wako. Pengine utaanza na kuhesabu siku zilizobaki kuelekea kujifungua. Kila wiki kwenye kipindi hichi ni maandalizi ya mtoto kutoka nje na kuona dunia. Muhula huu wa tatu mtoto ataongezeka uzito kwa kasi na hifadhi ya mafuta yatakayomsaidia baada ya kuzaliwa.

Kumbuka, ijapokuwa jamii yetu inajua miezi ya mimba ni 9, lakini unaweza kujifungua pia kwa miezi 10. Mimba ya kawaida iliyokamilika ni wiki 40 , ambapo itachukua mpaka miezi 10. Ni kawaida pia ukapitiliza wiki moja ama mbili kwenye muda uliotarajia kujifungua. Kama utavuka wiki nyingi zaidi na bado hujapata uchungu, mtoa huduma atakuchoma sindano ya uchungu ili ujifungue. Hakikisha unazungumza na daktari namna ulivyopanga kujifungua.

Mwezi wa 8(wiki ya 29 mpaka 32)

Mtoto ataendelea kukomaa na kuongezeka hifadhi ya mafuta. Utagundua mtoto ataanza kucheza zaidi. Ubongo wa mtoto unakuwa kwa kasi sana. Viungo vingi vya ndani zinakuwa zimekamilka, japo mapafu yanakuwa bado kukamilika.

Mwezi wa 9 (wiki ya 33 mpaka 36)

Kufikia kipindi hichi, mtoto wako anazidi kukua na kukomaa. Mapafu yanakaribua kukamilika. Mwili utaanza kuwasiliana ili aweze kufumba na kufumbua macho, kuzungusha kichwa kushika na kuhisi mwanga, kushika kitu na sauti.

Mtoto hapa anakuwa na urefu wa inch 17 mpaka 19 na uzito wa kilo 2 na nusu mapak tatu.

Mwezi wa kumi (wiki ya 37 mpaka 40)

Katika mwezi huu mwa mwisho unaweza kwenda leba muda wowote. Utagundua kwamba mtoto atacheza taratibu sana kutokana na nafasi ndogo. Kipindi hichi pia mtoto ataanza kusogeza kichwa zaidi kwenye mlango wa kizazi. Utajisi ovyo sana kipindi hichi mtoto anapojiandaa kutoka.

Mtoto wako tayari anaweza kutoka kuiona dunia kwa mara ya kwanza. Hapa mtoto atakuwa na urefu wa icnh 18 au 20 na uzito wa kilo 3 mpaka 3 na nusu.

Soma kuhusu: Kujifungua kwa Upasuaji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *