Dalili za Mimba Lakni Kipimo Negative

kipimo cha mimba(UPT)-Dalili za mimba
kipimo cha mimba

Waweza kujiuliza kwanini unapata dalili za mimba kama zote lakini kipimo kinaonesha negative. Kila mwanamke ana matamanio siku moja ya kushika mimba na kuzaa mtoto.

Lakini pia inatokea sana kwa wanawake mimba kuingia pasipo kupanga. Na tunafahamu kukosa hedhi kwa mwanamke ni jambo la kushtusha sana na hapo kunakuwa na shauku ya kutaka kupima kujihakikishia kama mimba ipo kweli.

Utapata mawazo gani pale unahisi dalili zote za mimba kama uchovu, kukosa hedhi,matiti kuuma, kutapika na zingine lakini ukipima mimba hakuna?

Tutazame mabadiliko ya homoni/vichocheo wakati wa mzunguko wa hedhi

Week moja kabla ya kupata hedhi kiwango cha homoni ya progesterone huanza kupanda na kiwnago cha homoni ya estrogen huanza kupungua.

Hali hii huchochea mwili kupata dalili za kuelekea hedhi kama matiti kuwa laini, mood kubadilika, mwili kukosa nguvu, tumbo kujaa gesi, wasiwasi na hali ya kutamani vitu flani flani.

Hedhi inapochelewa kutoka dalili hizi huongezeka zaidi. Hali hii inaweza kukuchanganya sana kwasababu vile unavojisikia hedhi inapochelewa ndivyo anavojisikia mwanamke mwenye mimba, dalili ni zile zile.

Hali huchanganya zaidi kwa mwanamke anayetafuta mimba kwa muda mrefu bila mafanikio.

Nini cha kufanya kuepuka mawazo

Swali muhimu la kujiuliza: Je ni lini muda sahihi wa kupima mimba baada ya kuanza kuona dalili za mimba na kuvusha hedhi?
Nashauri mwanamke asubiri walau week moja ama mbili zaidi baada ya kukosa hedhi ndipo ufanye kipimo cha mimba.

Kwasababu 30% ya mimba ambazo hutungwa zinaharibika katika kipindi kifupi na kutolewa nje kama hedhi. Hii yaweza kutokea katika kipindi cha week moja tu baada ya mimba kutungwa. Kitaalamu tunaitwa chemical preganancy.

Hii ndio hali inatokea umepima mimba ipo lakini baada ya week moja unashangaa hedhi imeanza kutoka.

Swali lingine unaweza kujiuliza vipi kama umesubiri week moja imepita hedhi haijatoka na dalili za mimba bado zipo na umepima hakuna mimba, nini inaweza kuwa shida? tazama sababu zingine hapa chini

1.Stress

Stress tunaiweka katika makundi mawili (physical stress) na emotionally stress.

Physical stress: Fikria swala la kufanya mazoezi kupita kiasi mfano wakimbiaji wa mbio ndefu(marathon), na emotionally stress ni msongo wa mawazo mfano umefiwa ghafla, unahofu dhidi ya ugonjwa labda corona, ama umeachwa na mpenzi nk.

Sababu hizi zinaeweza kupelekea mabadiliko ya vichocheo/homoni na hivo hedhi kusogea mbele.

2.Matumizi ya dawa

Baadhi ya dawa zina mchango mkubwa katika kururuga mzunguko wa hedhi yako. Dawa nyingi zikiwa zile za kundi la stereoids. Tiba asili pia na mafuta tiba(essential oils) zinaweza kuvuruga mzunguko.

Kama unatumia uzazi wa mpango pia mfano sindano, kitanzi au vidonge hiyo ni sababu kubwa kwako kuvurugika hedhi. Dawa za kisukari na za goita pia huchangia mzunguko kuvurugika.

3.Kipindi cha kukaribia kukoma hedhi

Kikawaida wanawake wengi hukoma hedhi wakiwa ana miaka 46 mpaka 50. Lakini swala la kuvurugika mzunguko huanza mapema kwenye miaka 40 hivi. Unaweza kuvusha miezi kadhaa usipate hedhi ama ukapata hedhi kidogo. Mood yaweza kubadilika matiti kuwa laini na mwili kuwa mchovu kama vile una mimba.

Ukiona dalili hizi na umri wako ni mkubwa basi tambua unakaribia kukoma hedhi. Usipate hofu kwavile ni jambo la kawaida kabisa kwa mwanamke unaweza kubofya hapa, kusoma makala yake kwa kina, ili kufahamu cha kufanya unapokoma hedhi.

Ukiwa na maswali wasiliana nasi kupitia whatsapp namba 0678626254.

Bofya kusoma kuhusu: Dalili za awali za mimba changa

10 replies on “Dalili za Mimba Lakni Kipimo Negative”

Nimelewa lakn mim naumwa kichwa kiuno nyonga mwli unakosa nguv sina ham yakula inaweza ikawa ni dalili?

baada ya Sikh 12 hedhi yangu ya mwez uliopita nilianza kupata dalili zote za mimba lakini Leo nimeingia tena na damu inatoka nyepesi sio kama yazamni maana zamani nilikua napata ya mabonge je tatizo nn? naomba nisaidie

Mtu akiwa na dalili zote za mimba kama kuumwa na kichwa,kiuno na chini ya tumbo na sijaona hethi kwa mwezi 1 na nusu nikipima kwa njia ya mkojo inaleta negative tatizo ni ipi

Mmi nimetoa kipandikiz mwaka jana mwez wa kumi nilivyotoatu nikachoma sindano ya uzaz wa mpango hedhi nikaja ipata mwez wa kwaza mwaka huu 2023 toka mwez huo cjapata tena hedhi na sion dalil ya mimba nifanyaje msaada

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *