Fangasi Ukeni Kwa Mjamzito

fangasi ukeni kwa mjamzito
fangas ukeni

Wakati wa ujauzito wanawake wengi hupata hofu juu ya kushika maambukizi yoyote kwani yanaweza kuathiri ukuaji wa mtoto tumboni. Fangasi ukeni kwa mjamzito ni moja ya maambukizi kwenye uke yanawatokea sana wajawazito. Kutokana na mabadiliko ya homoni na mazingira ya ukeni, wengi wanaugua zaidi fangasi.

Nini kinasababisha Mjamzito kuugua fangasi?

Fangasi ukeni huletekezwa na kimelea wanaoitwa Candida. Fangasi aina ya candida wanapatikana katika maeneo mengi ya mwili ikiwemo ukeni , kwenye ngozi na mkunduni.

Katika hali ya kawaida ya mwili hawana madhara kabisa mpaka pale kinga yako itakaposhuka au mazingira ya eneo husika kubadilika ndipo utaanza kuugua.

Wajawazito wanaugua sana fangasi kutokana na mabadiliko ya homoni kutokana na mimba. Wakati wa ujauzito, kinga ya mwili hubadilika, homoni kama estrogen na progesterone kuongezeka zaidi.Vyote hivi vinachangia kwa fangasi ukeni kukua kupita kiasi na kuleta madhara

Dalili kubwa za fangasi ukeni kwa mjamzito ni

Je kuna madhara yoyote ya fangasi kwa mtoto aliye tumboni?

Kwa kiasi kikubwa hakuna madhara kwa mtoto kutokana na mjamzito kuugua fangasi. Japo inaweza kutokea kama mama hajapona fangasi wakati wa kujifungua akamuambukiza mtoto.

Unawezaje kujikinga usiugue fangasi za ukeni?

  • Fanya usafi vizuri wa uke wako mara kwa mara
  • Epuka matumizi ya sabuni au manukato ukeni
  • Vaa chupi za pamba ili kupitisha hewa
  • Punguza matumizi ya vyakula vya sukari kwani vinapunguza kinga na kukufanya uugue fangasi kiurahisi.

Vipimo vya fangasi za ukeni kwa mjamzito

Hospitali daktari atakuuliza kuhusu dalili unazopata baada ya hapo atachukua sampuli kidogo ya uchafu unaopata na kuupeleka maabara kwa ajili ya vipimo.

Daktari pia anaweza kuotesha uchafu wako (culture) ili kubaini aina ya fangasi wa candida wanaokusumbua.

Matibabu ya Hospitali ya Fangasi Ukeni kwa Mjamzito

Kwa kiasi kikubwa fangasi za ukeni hutibika kiurahisi sana kupitia dawa za kupaka au za kuingiza ukeni(antifungal cream & suppository)

Dawa zitakupa nafuu ndani ya siku saba. Kwa mjamzito hakikisha kwanza unamwona daktari kabla ya kuanza kutumia dawa. Daktari atakupima na kukupa uhakika kama kweli una fangasi ama una maambukizi mengine.

Huduma ya kwanza kwa fangasi za ukeni

1.Maziwa mtindi

Mziwa mtindi ni tiba nzuri ya nyumbani kwa ajili ya
tatizo la fangasi ukeni. Maziwa mtindi yana bakteria wazuri
wanaoitwa Lactobacillus acidophilus. Bakteria hawa ni muhimu katika kuimarisha kinga ya mwili kwenye uke wako, watakusaidia kuzuia ukuaji wa fangasi ukeni.

Chovya kiasi kidogo cha maziwa weka ukeni kila siku. Hakikisha pia unakunywa glasi tatu za mtindi wa asili kila siku. Maziwa yako yasiongezewe sukari wala kemikali yoyote mbaya.

2.Mafuta ya nazi

Kutibu fangasi za ukeni hakikisha unanunua mafuta asili ya nazi-virgin, cold pressed. Mafuta ambayo hayajaongezewa kemikali zozote. Na pia yaliyokamuliwa pasipo kupitishwa kwenye moto mkali.
Pakaa kiasi kidogo cha mafuta ukeni mara mbili kwa siku asubuhi na jioni pia.

3.Apple cider vinegar

Hii ni moja ya tiba asili maarufu sana kwa ajili ya fangasi za ukeni. Vinegar ya apple ikitumika vizuri inasaidia kuimarisha ukuaji wa bakteria wazuri kwenye uke wako.

Sasa ili kupata faida zake vizuri hakikisha unanua vinegar ya apple yenye sifa hizi( organic, unfiltered with the mother). Baada ya hapo chukua vinegar ujazo wa robo kikombe cha chai changanya na maji lita moja osha uke wako mara 2 kwa siku.

Muhimu.

Kwa mjamzito dawa za hospitali za kumeza ili kutibu fangasi hazitakufaa kwani zinaweza kupelekea mimba kuharibika na matatizo kwa mtoto endapo atazaliwa. Dawa za kupaka ukeni ni salama zaidi kwa mjamzito endapo umejaribu hizi tiba asili bila mafanikio.

Ukiwa na maswali wasiliana nasi kupitia whatsapp namba 0678626254.

Bofya kusoma kuhusu: Tendo la ndoa baada ya kujifungua na changamoto zake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *