Kupoteza uwezo wa kunusa na kutambua ladha

kukosa uwezo wa kunusa ni dalili ya corona
virusi vya corona

Je kupoteza uwezo wa kunusa na ladha ni dalili ya corona?

Ugonjwa awa COVID-19, ni ugonjwa wa mfumo wa hewa unaosababishwa na kirusi kipya, ugonjwa huu unaweza kuwa na dalili nyingi sana ikiwemo dalili ya kupoteza uwezo wa kunusa na lutambua ladha. Na dalili hizi zinaweza kutofautiana kwa kila mtu.

Ukiacha dalili za kushindwa kupumua, kikohozi, kubanwa kifua na kichwa kuuma, corona yaweza kuwa na dalili zingine. Dalili ya kupoteza uwezo wa kunusa na kutambua ladha ya kitu ni mojawapo.

Kwenye makala tutaangazia zaidi kuhusu dalili hii ya kupoteza uwezo wa kunusa na kutambua ladha na muda gani inachukua kwa dalili kuisha.

Je kupoteza uwezo wa kunusa na kuonja ni dalili ya awali ya corona?

Kwanza kabisa yabidi ufahamu kwamba athari kwenye mfumo wa neva za utambuzi wa ladha na harufu ndiko hupelekea ushindwe kutambua harufu na ladha fulani. Ni mara chache sana hutokea kwa virusi wa mafua ya kawaida kuathiri neva hizi.

Dalili hii ya kupoteza uwezo wa kunusa na kuatmbua ladha huwapata wagonjwa wa corona katika hatua za awali tu. Inawezekana kabisa ukawa na dalili hii pasipo kuwa na dalili zingine kali kama mafua.

Ni kwa namna gani COVID-19 inapelekea kupoteza uwezo wa kunusa na kutambua ladha.

Kuna nadharia kadhaa zinazoelezea changamoto hii. Nadharia hii inasema hivi: virusi vinavyosababisha COVID-19 vinapoingia kwenye njia ya hewa, vina tabia ya kujishikiza kwenye seli zenye aina ya proteion ya ACE2. Na protini hii kulingana na tafiti inapatikana zaidi kwenye seli za kwenye pua na mdomo.

Seli hizi zikivamiwa na kirusi zinaharibiwa, na zikishaharibiwa maana yake kazi ya kutambua harufu na ladha haitafanyika.

Jinsi ya kujaribu kama umepoteza uwezo wa kunusa na kutambua ladha

Kunusa: Tafuta kitu chenye harufu kali sana mfano mafuta, au spray au kitunguu saumu. Unaweza pia kutumia powder ya mtoto kunusa kuona kama uko sawa.

Kuonja ladha: Tafuta chakula chochote chenye ladha kali. Mfano chakula kama machunywa, tangawizi, kahawa au chumvi kisha uonje.

Endapo utagundua kwamba unapata changamoto ya kutambua harufu ya kitu hicho ama ladha yake, ujue tayari una changamoto inayohitaji matibabu.

Kama dalili hizi zimekuja ghafla, inaweza kuwa ni dalili ua corona. Muhimu ufike hospitali mapema upate vipimo uanze tiba haraka.

Inachukua muda gani uwezo wa kuonja na kunusa kurudia

Endapo umeathrika na corona, yaweza kuchukua muda mrefu zaidi kwa uwezo wako wa kunusa na kutambua ladha kurejea. Ukilinganisha na mgonjwa wa mafua ambapo dalili hizi huisha mapema na uwezi wake kurejea.

Ripoti kutoka taasisi ya kudhibiti magonjwa ya Marekeni(CDC) inasema kwamba, kwa wastani inaweza kuchukua siku mpaka 8 kwa mgonjwa kurejea hali ya kawaida.

Dalili gani zingine mbaya za kutazama?

Pamoja na kupoteza uwezo wa kunusa na kutambua ladha, kuna dalili zingine nyingi zinazoashiria una corona. Dalili hizi ni kama

  • homa kali
  • kikohozi kikavu na kukosa pumzi
  • kuhisi uchovu sana
  • maumivu ya kichwa
  • kukosa uwezo wa kunusa na ladha
  • koo kukauka
  • pua kuwasha na kuziba
  • kichefuchefu na kutapika na
  • kuharisha

Kama una dalili za mwanzo za corona kama tulivoainisha hapo juu, chukua hatua hizi

  1. Tulia nyumbani muda wote, labda tu ukiwa unaenda hospitali ndipo utoke.
  2. Mjulishe daktari kuhusu maendeleo ya ugonjwa wako, na pia kama upo kwenye makundi hatarishi
  3. Jitenge na watu wengine: hata ndugu zako wa nyumbani unatakiwa kukaa nao mbali ili usiwaambukizie. Tumia chumba che peke yako na choo chako.
  4. Vaa barakoa ama kitambaa cha kuziba mdomo na pua endapo itakulazimu kutembetembea na kuongea na watu.
  5. Pumzika na unywe maji ya kutosha, unaweza pia kumeza dawa za maumivu na kikohozi kutuliza hali yako
  6. Fuatilia kwa makini dalili zako, kama zitakuwa mbaya unahitaji kupata msaada wa daktari.

Changamoto zingine zinazopelekea upoteze uwezo wa kunusa na kutambua ladha?

Pamoja na COVID-19, kuna changamoto nyingi zinaweza kupelekea upoteze uwezo wa kunusa na kuonja, changamoto hizi ni kama

  • uvutaji wa sigara
  • maambukizi ya mafua na sinusitis
  • aleji
  • kuota vinyama kwenye pua
  • majeraha kwenye kichwa
  • magonjwa ya ubongo
  • matumizi ya baadhi ya dawa za presha na antibiotics
  • mabadiliko ya homoni kutokana na tatizo kwenye tezi ya shingoni (thyroid)
  • upasuaji kwenye mdomo, koo na pua
  • tiba ya mionzi kwa ajili ya saratani kwenye kichwa au koo
  • vimbe kwenye kichwa na shingoni
  • kuishi mazingira yenye baadhi ya kemikali

Hitimisho

Kupoteza uwezo wa kunusa na kutambua harufu yaweza kujiokeza kwa mgojwa wa corona. Dalili hii hujitoeza mapema sana ukishapata maambukizi na yaweza kuchukua wiki kadhaa kuisha.

Ijapokuwa dalili za corona huanza taratibu, zinaweza kupelekea hali mbaya sana. Nenda hospitali mapema endapo utapata dalili za kukosa pumzi, maumivu makali ya kikfua au kushindwa kutambua vitu.

Soma kuhusu: Namna ya kujikinga na kumuhudumia mgonjwa wa corona

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *