Kifafa cha Mimba

kifafa cha mimba
mimba

Nini Maana ya kifafa Cha Mimba?

Kifafa cha mimba kitaalamu eclampsia ni matokeo ya kuongezeka zaidi kwa presha ya damu kwa mjamzito. Ni tatizo linalotokea mara chache sana ambapo presha kubwa ya damu kwa mjamzito inapelekea kupata na kifafa.

Kifafa ni matokeo ya mabadiliko yasiyo ya kawaida ya shuguli za ubongo yanayopelekea kupatwa na dalili za mwili kukosa nguvu, kutokwa na povu, kutetemeka na kupoteza fahamu.

Dalili Za Kifafa Cha Mimba

Kwasababu shinikizo kubwa na damu kwa mjamzito (preeclampsia) ndio chanzo kikubwa cha kifafa cha mimba. Mjamzito anaweza kuwa na dalili za changamoto zote mbili, yaani akawa na dalili za kuongezeka zaidi kwa presha ya damu, kuvimba miguu na mikono na na dalili kuu za kifafa cha mimba yaani kuanguka na kupoteza fahamu mara kwa mara.

Dalili zingine ni kama

  • kuongezea uzito kupita kiasi
  • kutapika na kichefuchefu upita kiasi
  • kutoa mkojo kwa shida
  • maumivu makali ya kichwa
  • kuvimba uso na vidole na
  • maumivu ya tumbo hasa upande wa juu kulia

Nini Kinasababisha Kifafa Cha Mimba?

Kifafa cha mimba hutokea hasa baada ya mgonjwa kuwa na shinikizo kubwa sana la damu. Inaweza kutokea wakati wa ujauzito au mara chache sana baada ya kujifungua. Presha inapokuwa kubwa sana huathiri ufanya kazi wa ubongo na kupelekea kifafa.

Kundi gani lipo Kwenye hatari Zaidi ya Kupata Kifafa cha mimba?
Kama una tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu, kuvimba uso, miguu na mikono kitalamu huitwa preeclampsia. Hii inaweza kupelekea ukapata kifafa cha mimba yani eclampsia.

Mazingira mengine hatarishi mi pamoja na

  • kupanda kwa presha ya damu wakati wa ujauzito
  • kubeba mimba katika umri zaidi ya miaka 40 au chini ya miaka 20
  • mimba ya mapacha wawili au zaidi
  • ujauzito wa mara ya kwnza
  • kuwa na historia ya kuugua kisukari kwa muda mrefu na
  • magonjwa ya figo

Madhara ya Kifafa Cha Mimba Kwa Mtoto

Kifafa cha mimba na kupanda kwa presha ya damu kwa mjamzito huathiri kondo la nyuma. Huu ni mrija unaomuunganisha mama na mtoto. Ni mahali ambapo chakula na hewa inapita kwenda kwa mtoto.

Mzunguko wa damu unaweza kupungua na hivo kiumbe kukosa virutubisho muhimu. Hii itasababisha mtoto kuzaliwa njiti na kupatwa na matatizo ya kiafya.

Kifafa Cha Mimba Kinagundulikaje Hospitali?

Endapo una historia ya kuugua presha, dakari anaweza kupendekeza vipimo kujua ukubwa wa tatizo lako. Kama hujawahi kuugua presha ataagiza vipimo pia kujua kwanini unapata kifafa. Vipimo hivi ni

Kipimo cha damu: Vipimo hivi ni kwa ajili ya kujua kiwango cha seli nyekundu za damu zilizopo na kipimo cha kugundua namna gani damu yako ina uwezo wa kuganda. Kipimo cha damu pia kitatumika kujua hali ya figo na ini lako kama vinafanya kazi vizuri.

Creatinine Test: Creatinine ni taka inayozalishwa na misuli yako. Kazi ya figo ni kuchuja creatinine kwenye damu, kama chujio la figo limeathirika manake creatinine itabaki kwenye damu. Kiwango kikubwa cha creatinine kwenye damu kinaweza kuashiria una preeclampsia.

Kipimo cha Mkojo: Daktari anaweza pia kupendekeza kipimo cha mkojo kuona kiwango cha protini.

Nini Tiba Ya Kifafa Cha Mimba

Tiba kuu ya kifafa cha mimba ni wewe kujifungua. Daktari atafatilia mwenendo wa dalili unazopata na pia kuona ukuaji wa mtoto na kisha atapendekeza lini yafaa mtoto azaliwe kwa kuongezewa uchungu au ufanyiwe upasuaji.

Je Kuna Madhara ya Muda Mrefu Ya Kifafa Cha Mimba?

Baada ya kujifungua dalili za kifafa cha mimba zitaisha ndani ya wiki chache. Kwa maana hiyo kama umeugua kuna uwezekano mkubwa pia kwa siku za mbele ukishika ujauzito utapata tena kifafa cha mimba. Ama ukaungua presha kwa miaka ijayo. Ni muhimu kuendelea na checkup baada ya kujifungua kujua mwenendo wa presha yako.

Kama tatizo ni kubwa mfano la kukatika kwa kondo la nyuma, daktari anaweza kupendekeza ufannyiwe upasuaji wa haraka ili kumuokoa mtoto. Mama anaweza kupata matatizo zaidi kama kiharusi na hatari ya kifo.

Muhimu sana mama apate tiba ya tatizo lake la presha kupanda wakati wa ujauzito. Hudhuria clinic kama ulivoshauriwa bila kukosa kupata vipimo na ufuatiliaji wa kiwango cha presha yako vizuri.

Bofya kusoma makala inayofuata kuhusu: Kujifungua kwa upasuaji+maandalizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *