Antibiotics: Matumizi Sahihi pamoja na madhara

antibiotics
antibiotics

Antibiotics ni dawa zinazotumika kutibu maambukizi ta bakteria. Kwa jina lingine tunaita antibacterials. Zinatibu maambukizi kwa kuua au kupunguza bakteria wabaya mwilini.

Antibiotic ya kwanza kabisa ilizalishwa rasmi na kuanza kutumika mwaka 1936. Kabla ya hapo aslimia 30 ya vifo vyote vilisababishwa na maambukizi ya bakteria. Kupitia antibiotics maisha mengi sana yameshaokolewa. Kwasasa antibiotics ni dawa zenye nguvu sana kuzuia kusambaa kwa maambukizi na kutibu.

Aina za Antibiotics

Kuna aina nyingi za antibiotics. Baadhi ya antibiotics hufanya kazi vizuri kwa aina fulani ya maambukizi ya bakteria.

Antibiotics zinakuja katika mifumo mingi, ikiwemo

 • Vidonge
 • Kimiminika
 • Cream na
 • Mafuta

Baadhi ya antibiotics zinapatikana hospitali baada ya kuandikiwa na daktari, na zingine unaweza kunua pharmacy ukatumia.

Antibiotics zinavyopambana na bakteria wabaya

Antibiotics zinapambana na baada aidha kwa kuua au kupunguza kasi ya ukuaji wa bakteria. Zinafanya hivi kwa

 • Kushambulia ukuta wa bakteria
 • Kuingilia na kuzuia uzalishaji wa bakteria na
 • Kuzuia uzalishaji wa protin kwenye bakteria

Inachukua muda gani antibiotics kuleta matokeo?

Antibiotics zinaanza kufanya kazi mapema tu baada ya kutumia. Japo unaweza usijisikie nafuu kwa haraka mpaka baada ya siku tatu. Unafuu baada ya kutumia antibiotics pia unatofautiana kwa kila aina. Na pia inategemeana na aina ya maambukizi uliyonao.

Dozi nyingi za antibiotics nyingi zinatakiwa kutumika kwa siku 7 mpaka 14. Daktari wako atapendekeza ukubwa wa dozi na aina ya antibiotics kulingana na mambukizi uliyonayo.

Japo kwa nyakati fulani hutapata mafuu mapema kwa siku kadhaa, ni muhimu kumaliza dozi yote kama ulivyaelekezwa na daktari. Kumaliza dozi kunasaidia kuepusha usugu wa mwili kwenye dawa. Usiache kutumia dawa haraka bila kumpa taarifa daktari anayekuhudumia.

Nini maana ya usugu wa dawa- antibiotics?

Antibiotics ni dawa zenye nguvu sana na zinafanya kazi vizuri kutibu changamoto husika ya kiafya. Japo kwa sasa baadhi ya antibiotics zimepungua makali yake kutokana na bakteria kuwa sugu.

Usugu wa dawa (antibiotics resistence) inatokea pale aina fulani ya antibiotic inaposhindwa kupambana na bakteria, kitu ambacho hapo awali hakikuwepo. Kila mwaka watu zaidi ya milioni mbili wanaathiriwa na bakteria sugu, wasiosikia antibiotics, na hivo kupelekea vifo zaidi ya 23,000.

Pale unapotumia antibiotic bakteria dhaifu wanakufa. Bakteria wanaobaki wanakuwa sugu dhidi ya dawa. Bakteria hawa kwa kiasi kikubwa wanakuwa na sifa za tofauti na za kipekee ukilinganisha na wengine.

Matumizi mabaya ya antibiotics

Sababu kubwa ya bakteria kuwa sugu kwenye antibiotic ni matumizi makubwa kupita kiasi au matumizi yasiyo sahihi. Karibu asilimia 30 ya matumizi ya antibiotics siyo ya lazima kabisa. Hii ni kwasababu antibiotics zinapatikana kwa wingi famasi. Watu wengi hawana kawaida ya kufanya vipimo. Wakiumwa wanakimbilia kumeza tu dawa.

Hatua za kufuata kuepusha usugu wa dawa

Tumia antibiotics kwa ajili ya maambukizi ya bakteria tu. Usitumie antibiotics kwa changamoto zinazosababishwa na virusi kama mafua,koo kuwasha na kikohozi.

Tumia antibiotics kama ulivyoelekezwa na daktari: Matumizi ya dozi tofauti, kuvusha dozi au kutumia kwa muda mrefu zaidi inaleta usugu wa dawa. Hata kama utajisikia vizuri baada ya siku chache, usiache kumeza dawa ulizopatiwa.

Tumia antibiotics sahihi. Matumizi ya aina isiyo sahihi ya antibiotics inaweza kusababisha usugu. Usitumie dozi ya dawa alizoandikiwa mtu mwingine. Na pia usitumie dawa zilizobaki hapo awali.

Antibiotics zinatumika kutibu magonjwa gani?

Antibiotics zinatumika kutibu magonjwa yanayosababishwa na bakteria. Wakati fulani ni vigumu kugundua kama aina yako ya maambukizi imesababishwa na bakteria au virusi kwasababu dalili zinaweza kufanana.

Daktari ataweza kufanya upembuzi zaidi wa dalili unazopata na kulinganisha na majibu ya maabara kujua aina ya maambukizi. Kwa nyakati fulani daktari anaweza kuagiza ufanyiwe kipimo cha mkojo ama damu kujua aina ya maambukizi uliyonayo.

Baadhi ya maambukizi yanayosababishwa ana bakteria ni pamoja na

 • UTI
 • Sinus na maambukizi kwenye masikio
 • Maambukizi kwenye koo

Antibiotics hazitibu maambukizi ya virusi au fangasi kwahivo haziwezi kutibu magonjwa kama fangasi kwenye ngozi, ukeni au miguuni au minyoo. Changamoto hizi zinatibiwa kupitia aina ingine ya dawa zinazoitwa antifungal.

Madhara madogo(side effects) ya kutumia antibiotics

Aina nyingi za antibiotics zina matokeo yanyofanana. madhara yaliyozoeleza zadii ni pamoja na

 • Kuharisha
 • Kichefuchefu
 • Kutapika na
 • Maumivu ya misuli

Badhi ya matokeo yanaweza kupunguzwa kwa kutumia antibiotic baada ya kula. Japo kuna aina zingine za dawa yatakiwa kutumia kwenye tumbo tupu kabla ya kula. Hakikisha unamuuliza daktari au mfamasia namna ya kutumia dawa.

Muone daktari endapo utapata dalili hizi

Soma zaidi kuhusu: Fangasi Mdomoni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *