Kiwango Sahihi cha Mbegu za Kiume Kutungisha Mimba

mbegu za kiume
mbegu za kiume

Wingi wa mbegu za kiume ni jambo la muhimu sana katika kumpa ujauzito mwanamke. Endapo una kiwango kidogo na huwezi kumpa mwanamke mimba basi ujue kuna shida mahali inayotakiwa kutibiwa mapema.

Kiwango cha kawaida cha mbegu za kiume kinatakiwa kuwa milioni 15 mpaka milioni 200 kwa milliliter ya shahawa. Kiwango chochote chini ya milioni 15 kinatambulika kwamba ni pungufu na ni ngumu kumpa mwanamke mimba.

Kufahamu uwezo na wingi wa mbegu zako ni muhimu uende hospitali au mabaara ya karibu kisha utapiga punyeto na kuweka mbegu kwenye kifaa, na muhudumu atafanya vipimo na kutoa ripoti yako.

Jinsi ya Kutafsiri Uwezo Wa Mbegu Zako

Kipimo cha mbegu(semen analysis) kinapima mambo yafuatayo kuhusu mbegu

 • kiwango cha mbegu zako
 • shepu ya mbegu na
 • uwezo wa mbegu kuogoelea (sperm motility)

Baada ya vipimo zungumza na daktari akupe ufafanuzi wa kina kuhusu uwezo wa mbegu zako kwa kulingana na ripoti ya vipimo.

Kwanini Kiwango Cha Mbegu za Kiume Ni Swala La Muhimu?

Unapoongelea swala la kumpa mwanamke mimba, uwezo wa mbegu zako kama mwanaume ni jambo la muhimu sana. Pamoja na kwamba inahitajika mbegu moja tu kurutubisha yai, mbegu nyingi za kiume zinapokuwa na afya njema basi chansi ya mwanamke kushika mimba inaongezeka zaidi.

Hata kama bado huna mpango wa kumpa mwanamke mimba, uwezo na ubora wa mbegu zako ni kipimo cha utimamu wa afya yako pia. Utafiti mmoja uligundua kwamba wanaume wenye mbegu kidogo wana uwezekano mkubwa wa kuwa na mafuta mengi mwilini na presha kubwa ya damu ukilinganisha na wanaume wenye mbegu nyingi.

Kwa kutazama sababu hapo juu, kama daktari atagundua una mbegu kidogo, itakuwa ni muhimu sana daktari apime pia kiwango cha homoni ya testosterone, afatilie mtindo wa maisha na afya yako kwa ujumla kujua chanzo cha tatizo lako.

Kiwango cha Mbegu Kivoathiri Uwezo wa Kutungisha Mimba

Chansi ya kumpa mwanamke mimba inapungua kadiri idadi ya mbegu inavopungua. Hii ni sababu mojawapo kubwa kwanini wanawake wengi hawashiki mimba.

Sababu zingine kwa upande wa mwanamke ni pamoja na

Kushindwa kushika mimba pia yaweza kusababishwa na wapenzi kutokutana mara kwa mara. Ni kawaida kwa wapenzi wenye afya nzuri kabisa kuchukua mpaka miezi sita ama mwaka kushika mimba, hilo ni kawaida.

Kama una umri zaidi ya miaka 35 na mmekekuwa mkitafuta mimba bila mafanikio zaidi ya mwaka mmoja muhimu muende hospitali mkafanyiwe vipimo kwa wote wawili.

Nini Kinasababisha upungufu wa mbegu kwa mwanaume?

Vihatarishi vinavyopekelea kupungukiwa mbegu za kiume vipo vingi. Hapa chini tumeelezea sababu kuuu

1.Magonjwa ya uzazi na upasuaji kwenye viungo vya uzazi

Ajali ama ugonjwa unaopelekea ufanyiwe upasuaji ni kihatarishi cha kupngua kwa uzazlishaji wa mbegu. Baada ya upasuaji mirija midogo kwenye korodani yaweza kuathiriwa na hivo mbegu zikazalishwa kidogo.

2.Tiba ya saratani

Tiba hizi ikiwemo mionzi na chemotherapy huathiri mbegu: mionzi huua mbegu moja kwa moja.

3.Kuvimba kwa mirija midogo ya damu kwenye korodani

Kitaalamu tatizo huitwa varicocele. Mirija hii inapovimba inapunguza mzunguko wa damu kuelekea kwenye tishu za kuzalisha mbegu.

4.Maambukizi ya magonjwa ya zinaa

Endapo mgonjwa hakupata tiba vizuri ama aliyechelewa kupata tiba , inaweza kupelekea kuziba kwa mirija ya damu kwenye via vya uzazi.

5.Mazingira

Hali ya joto sana inaathiri na kuua mbegu. Hii ndiomaana wakati wa joto utaona mapumbu yakininginia nje kuepka joto kali la mwili. Hivo vitu chochote chenye joto sana siyo salaa kuwekwa karibu na viungo vya uzazi, mfano kompyuta mpakato, simu nk.

Mazingira mengine hatarishiri ni eneo lenye mionzi hasa kwenye viwanda.

6.Mtindo wa maisha

Aina fulani ya maisha ina mchango mkubwa kwenye ubora na wingi wa mbegu zako. Matumizi ya pombe, sigara na madawa ya kulevya hupunguza uzalishaji wa mbegu. Kufanya kazi masaa mengi ukiwa umekaa, uzito mkubwa, msongo wa mawazo pia hupelekea kupungua uzalishaji wa mbegu.

Vipi kuhusu kupiga punyeto, je inapunguza mbegu?

Tafiti zinasema kwamba hata kama ukimwaga mbegu kila siku aidha kwa kupiga punyeto ama kukutana na mwanamke bado mbegu zitawepo za kutosha. Madhara ya punyeto ni kushindwa kumridhisha mwanamke na kwa kushindwa kurudia tendo na pia kuwhai kufika kileleni.

Je Kuna Tiba ya Kuongeza Mbegu za Kiume?

Habari njema ni kwamba tiba inapatikana hospitali na kwenye tiba asili pia, ili kuboresha idadi na uwezo wa mbegu zako. Kwa kulingana na chanzo cha tatizo, daktari anaweza kupendekeza tiba hizi

Kufanyiwa upasuaji: hii ni kama mishipa midogo ya damu kwenye korodani imevimba(varicocele)
Antibioitcs: kama kuna maambukizi ya bakteria yanyosababisha mbegu kufa na
Dawa za kuchochea uzalishaji wa mbegu pamoja na ushauri kama una tatizo la kuwahi kumwaga na kutosimamisha uume.

Ushauri wa Kufuata ili Kuboresha Mbegu zako

 1. Punguza uzito na kitambi: uzito mkubwa na kitambi yaweza kusababisha kupungua kwa uzalishaji wa mbegu. Rekebisha mtindo wa maisha ili upunguze uzito kuwa normal
 2. Tumia virutubisho vya Vitamin na Zinc. Ongea na daktari akujulishe una upungufu wa madini na vitamini gani. Daktari anaweza kupendekeza ule zaidi vyakula aina gani kukusaidia.
 3. Punguza matumizi ya pombe na sigara
 4. Vaa boksa za cotton zinakinga pumbu dhidi ya joto kali ambalo huua mbegu.

Tumia tiba hii ya mimea kupitia vidonge vya Confido na Zinc kuongeza mbegu.

tiba ya kuongeza mbegu

Ni tiba asili zilizotengenezwa wa mimea, zikawekwa kwenye mfumo wa vidonge na kuthibitishwa na mamlaka ili kutibu changamoto za kiume kama upungufu wa mbegu, shahawa nyepesi, kuwahi kufika kileleni na uume kutosimama vizuri kwenye tendo.

Huhitaji kujaribu dawa zisizo na uhakika, tayari tumeshafanya utafiti wa kina na kujiridhisha kwamba dawa hizi mbili, zikitumika kwa pamoja zinaleta matokeo ndani ya mwezi mmoja.

Baada ya kutumia Confido na zinc tegemea haya

 • Mbegu kuongezeka na kufikia kiwango cha zaidi ya milioni 50 kwa mililita
 • Uwezo wa kufanya tendo kuongezeka na utaweza kurudia mpaka mara tatu bila kuchoka
 • Hamu ya tendo kuimarisha na kukufanya ufurahie tendo la ndoa
 • Misuli ya uume kuimarisha na kukufanya uwe imara wakati wote wa tendo

Gharama ni Tsh 150,000/= dozi ya mwezi mmoja.

Tunapatikana magomeni Dar, Chati na daktari kwa whatsapp no. 0678626254 kuanza tiba

Bofya makala inayofuata kuhusu Shahawa nyepesi na suluhisho lake

2 replies on “Kiwango Sahihi cha Mbegu za Kiume Kutungisha Mimba”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *