Chuchu ni eneo la matiti ambalo linakuwa na msisimko sana ambalo laweza kuuma kwa sababu mbalimbali. Nguo za kubana, vipele na pia maambukizi ya bacteria au fangasi yanaweza kufanya ngozi kututumka na hivo kuleta maumivu ya chuchu.
Kwa wanawake wengi chuchu zao huvimba hasa wakati wa hedhi, mimba na kipindi cha kunyonyesha.
Wanawake wengi pia hupata hofu pale wakijiskia maumivu ya chuchu na kuhisi kwamba pengine wameanza kupata saratani ya matiti.
Sababu za Maumivu ya Matiti
1.Nguo isiyokaa vizuri
Uvaaji wa bra au shati ambalo halijakaza vizuri hupelekea msuguano na chuchu kila mara, pengine wakati wa kutembea ama kukimbia. Msuguano huu husababisha chuchu kuvimba na hata kutoa damu. Kuepuka tatizo hili hakikisha unavaa topu na sidiria zinazokutosha vizuri, isiwe kubwa kuliko na isiwe ndogo sana.
2.Matatizo ya ngozi
Magonjwa ya ngozi kama pumu ya ngozi ama fangasi ya ngozi ni chanzo cha kuvimba kwa na maumivu ya chuchu; onana na daktari kama una ugonjwa wowote wa ngozi upate tiba mapema.
3.Hedhi
Kuvimba na maumivu ya chuchu inaweza kuwa ni kiashiria cha hedhi kukaribia. Hedhi inapokarbia homoni ya estrogeni huzalishwa kwa wingi na kupelekea chuchu kuvimba na kuuma. Maumivu haya huisha baada ya hedhi kupita.
4.Mimba
Wakati wa mimba kunatokea mabadiliko makubwa ya vichocheo/homoni na hivo kufanya matiti kuwa laini, kuvimba na kuuma. Chuchu huanza kutoa maji maji kama maziwa kadiri unavokaribia kujifungua. Kama maumivu ni makali sana, ongea na daktari wako akupatie vidonge salama vya kupunguza maumivu.
5.Kunyonyesha
Chuchu huuma pale mtoto anapovuta titi wakati wa kunyonya. Maumivu haya yanaweza kuwa kama umechomwa sindano kwa mbali ila yataisha ndani ya muda mfupi.
Jinsi ya Kupunguza Maumivu ya Chuchu wakati unanyonyesha
- Kabla hujanyonyesha binya titi upate maziwa kidogo kisha yapake eneo la chuchu.
- Unaweza kupaka mafuta salama kwa mtoto kwenye eneo la titi, ongea na daktari kupata pendezo la mafuta ya kutumia.
- Hakikisha chuchu zako zinakauka kila unapomaliza kunyonyesha na ubadili sponge ya kunyonya matiti mara kwa mara.
- Vaa sidiria nzuri ya pamba kwa ajili ya kunyonyesha, hakikisha inakutosha vizuri na haisuguani na chuchu zako.
- Jaribu njia na mikao mbalimbali ya kunyonyesha mpaka upate mkao unaokufaa na usiokuumiza.
Sababu zingine na Maumivu ya Matiti yako ni pamoja na
Maambukizi
Mambukizi yaweza kuwa chanzo cha maumivu yako ya chuchu. Mfano maambukizi ya kwenye mrija wa maziwa kitaalamu mastitis ambayo husababishwa na bacteria kukua na kuathiri mshipa wa maziwa ulioziba ni chanzo kikubwa cha maumivu kwa wanawake wengi wanaonyonyesha. Hakikisha unatumia dozi nzima utakayoandikiwa na daktari kutibu changamoto hii.
Saratani ya matiti
Unaweza kuwa na saratrani ya matiti kama maumivu yako ya chuchu yanaambatana na dalili zingine za
- chuchu kutengeneza shimo baada ya kubinya
- kutokwa na majimaji yasiyo maziwa
- kuvimba chini ya kwapa
- chuchu kuwa nyekundu na kutengeneza magamba
Ukiona dalili hizi nenda hospitali haraka daktari akufanyie vipimo kujua kama una saratani ili uanze tiba mapema.
Tumia breast care tea kutibu changamoto za matiti yako
Kazi na faida za breast care tea
- Kutibu chuchu na matiti yanayouma na kuvimba mara kwa mara
- Kuimarisha mzunguko wa damu kwenye matiti na kuondoa damu iliyoganda(damu kudanda kwenye mishipa ndio chanzo kikubwa cha uvimbe kwenye matiti)
- Kukukinga dhidi ya changamoto za matiti kama saratani
- Kuzuia kujitokeza kwa saratani baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye matiti na
- Kuongeza kinga ya mwili