Je kuna Tatizo Kuwa na Korodani ndogo?

mfano wa Korodani ndogo
mfano wa korodani

Nini kinasababisha uwe na korodani/pumbu ndogo

Ukubwa wa korodani unatofautiana kati ya mtu na mtu, kwahivo watakiwa kujua kwamba kutofautiana kwa maumbile siyo tatizo. Kuwa na korodani ndogo kwa kwa wanaume wengi inaweza isiwe na athari yoyote katika uzazi. Hapa chini kuna maelezo ya mazingira yanayopelekea kuwa na pumbu ndogo

Hypogonadism

Hypogonadism ni hali ya mwili kutozalisha homoni ya kutosha ya testosterone. Kwa ufahamu tu ni kwamba homoni hii ndio inahusika na ukuaji wa maumbile ya uzazi kwa mwanaume ikiwemo ukubwa wa uume, korodani, uzalishaji wa mbegu na hata matamanio ya tendo la ndoa.

Hypogonadism inaweza kusababishwa na korodani kutopokea taarifa kutoka kwenye ubongo ili kuzalisha homoni ya kutosha ya testosterone na mbegu. Hali hii unaweza kuzaliwa nayo ama ikasababishwa na

  • maambukizi kwenye via vya uzazi
  • kujikunja kwa mirija ya kwenye korodani(testicular torsion) na
  • matumizi ya dawa bila ushauri wa daktari

Varicocele

Changamoto ingine inayosababisha uwe na mapumbu madogo inaitwa varicocele. Varicocele ni kitendo cha kuvimba kwa mishipa midogo ya damu kwenye mfuko wa korodani. Kuvimba kwa mishipa hii kunafanya korodani kutopokea damu ya kutosha na hivo kupungua ukubwa wake.

Undescended testes

Hili ni tatizo linalojitokeza mtoto akiwa mdogo sana kwa korodani zake kutoshuka chini kama inavotakiwa. Tatizo hili linaweza kutibika hospitali kwa upasuaji.

Lini unatakiwa kumwona Daktari

Ni muhimu kuzungumza na daktari iwapo unajiona korodani zako hazipo sawa. Daktari atakuchunguza na kuona kama kuna tatizo lolote la kiafya lililopelekea pumbu zako ziwe ndogo. Usisikilize watu wa kijiweni maana watakupotosha sana. Kuongea na daktari itakupa amani ya moyo na majibu ya uhakika juu ya tatizo lako.

Tiba ya Hospitali kwa korodani ndogo

Matibabu ya Ugumba

Kama tatizo lako la kuwa na korodani ndogo limepelekea ushindwe kumpa mwanamke mimba, daktari atakupatia dawa za kutibu changamoto yako.

Dawa ya clomiphene ya kumeza ambayo hutumika sana kwa wanawake kupevusha mayai, inaweza pia kutumiwa na wanaume wagumba kuchochea uzalishaji wa mbegu.

Sindano pia za homoni (gonatrophins)zinaweza kutumika kama ikitokea una upungufu wa mbegu za kiume.

Matibabu ya varicocele

Kama nilivyosema hapo mwanzo varicocele ni kuvimba kwa mishipa ya damu ya kwenye korodani hata kupunguza ukubwa wa pumbu na uzalishaji wa mbegu. Upasuaji ndio tiba sahihi kwa changmoto hii. Upasuaji utasaidia kuchochea tena uwezo wa korodani kuzalisha mbegu.

Je tiba Asili za kutibu korodani ndogo? na kuongeza korodani?

Kiujumla hakuna njia salama ya kuongeza ukubwa wa pumbu. Kuwa makini na matangazo ya dawa mbalimbali unayoona mtandaoni maana kuna bidhaa nyingi sana za tiba kwa wanaume ambazo hata hazijathibitishwa na mamlaka za afya.

Matumizi ya dawa ambazo hajijathibitishwa ni hatari kwani unaweza kuathiri figo na ini pia.

Ni upi ukubwa sahihi wa korodani unaotakiwa?

Ukubwa wa kawaida wa korodani ni cm 4x3x2. Wanawaume wengi wana korodani mbili, ni jambo la kawaida pia korodani moja kuwa kubwa kuliko ingine. Korodani hizi huhifadhiwa kwenye mfuko maalumu unaoitwa scrotum yaani ile ngozi ya nje.

Je Ukubwa wa korodani ni ishu?

Kwa kiasi kikubwa maumbile ya korodani zako siyo ishu sana kwenye uwezo wa kumpa mimba mwanamke.
Jina la kitabibu kuelezea upungufu wa homoni ya kiume (testosterone) ni kuwa na homoni nyingi za kike kwa mwanume ni hypogonadism.

Dalili za upungufu wa homoni ya kiume ni pamoja na

Ni lini korodani zinaanza kukua na kustop ukuaji wake?
Mtoto anapozaliwa husubiri mpaka miaka 8 kwa korodani zake kuanza kukua kwa kasi na kufikia mwisho wa ukuaji wakati wa balehe. Ni katika wati huu wa belehe ambapo unaanza kuona nywele sehemu za siri na kwapani maarufu kama mavuzi.

Je Korodani zinaweza kunywea ndani?
Kadiri mwanaume anvozeeka uzalishaji wa homoni ya kiume(testosterone) unapungua kutokana na korodani pia kupungua ukubwa wake.Kitaalamu hutiwa testicular atrophy. Mabadiliko huwa ya taratibu sana kiasi kwmaba ni ngumu kwako kugundua.

Homoni ya Testosterone na Uwezo wa Tendo la ndoa

Upungufu wa testosterone hufanya hata hamu ya tendo la ndoa kupungua sana na misuli yako kupungua pia. Hili ni kawaida kabisa kadiri unavozeeka.
Baadhi ya changamoto za kiafya ambazo zinaweza kupelekea kupungua uzalishaji wa testosterone na ukubwa wa pumbu ni pamoja na

  • magonjwa ya zinaa kama kisonono na kaswende
  • kuugua TB na magonjwa mengine yanayosababishwa na virusi
  • Ajali kwenye korodani

Mazingira mengine yanayoweza kupelekea kwa korodani kunywea ndani ni pamoja na mabadiliko ya joto na kuoga maji ya baridi. Mapumbu hurudi ndani ili kutoathiri mbegu. Hii ni kawaida kabisa na isikupe hofu, ni moja ya taratibu za mwili kujilinda.

Jinsi ya Kulinda Afya ya Korodani zako

Hakikisha unajifanyia tathmini wewe mwenyewe kuhusu afya ya pumbu zako kwa kutizama kama kuna vimbe zozote au hali yoyote isyo ya kawaida. Unaweza kujifanyia upembuzi huu wakati unaelekea kuoga au baada ya kuoga.

Shika pumbu moja moja jaribu kuizungusha kidogo kama gololi kuona kama kuna mabadiliko yoyote ya ukubwa , shape na ugumu wake. Kama ukijisikia maumivu yoyote ama uvimbe wakati unapapasa pumbu zako muone daktari mapema kwa uchunguzi.

Maumivu haya au uvimbe inaweza kuashiria mambukizi kwenye pumbu ama saratani. Weka ratiba uonane na urologist. Urologist ni daktari bingwa wa magonjwa ya wanaume na mkojo. Usisubiri kabisa muda mrefu bila kumwona daktari.

Tumia tiba hii ya mimea kupitia vidonge vya zinc na vig power kuongeza mbegu

Ni tiba asili zilizotengenezwa wa mimea, zikawekwa kwenye mfumo wa vidonge na kuthibitishwa na mamlaka ili kutibu changamoto za kiume kama upungufu wa mbegu, shahawa nyepesi, kuwahi kufika kileleni na uume kutosimama vizuri kwenye tendo.

Huhitaji kujaribu dawa zisizo na uhakika, tayari tumeshafanya utafiti wa kina na kujiridhisha kwamba dawa hizi mbili, zikitumika kwa pamoja zinaleta matokeo ndani ya mwezi mmoja.

Baada ya kutumia Vig power na zinc tegemea haya

  • Shahawa kuwa nzito, , na mbegu kuongezeka na kufikia kiwango cha zaidi ya milioni 50 kwa mililita
  • Uwezo wa kufanya tendo kuongezeka na utaweza kurudia mpaka mara tatu bila kuchoka
  • Hamu ya tendo kuimarisha na kukufanya ufurahie tendo la ndoa
  • Misuli ya uume kuimarisha na kukufanya uwe imara wakati wote wa tendo

Ghrama ni Tsh 150,000/= dozi ya mwezi mmoja.

Tunapatikana magomeni Dar, Chati na daktari kwa whatsapp no. 0678626254 kuanza tiba

Bofya kusoma makala inayofuata kuhusu: Kiwango cha mbegu kinachotosha kumpa mwanamke mimba