Harufu ya Shombo la Samaki Ukeni

harufu ya shombo la samaki ukeni
Mwanamke

Kama umegundua unatokwa na harufu ya shombo la samaki ukeni, inaweza kuwa imesababishwa na jasho, maambukizi ya bakteria na au likawa tatizo la kurithi.

Harufu ya uke inabadilika katika siku zote za mzunguko wako wa hedhi. Kama una wasiwasi kuhusu harufu ya uke na rangi ya uchafu unaotoka, tafadhali muone daktari mapema. Hasa kama uchafu huu unaambatana na dalili za muwasho, kuunguza ukeni na uke kuwa mwekundu sana.

Daktari atakufanyia vipimo na kukupa dawa za kukufaa.

Chanzo cha Harufu ya shombo la Samaki Ukeni

1.Vaginitis

Vaginitis ni kuvimba na kututumka kwa uke kutokana na maambukizi ya bakteria au fangasi. Vaginitis pia yaweza kusababishwa na magonjwa ya zinaa kama trichomoniasis. Kutokwa na harufu ya shombo la samaki ni ni dalili kubwa ya mambukizi haya.

2.Ukuaji wa Bakteria wabaya kupita kiasi(Bacterial Vaginosis)

Sababu kubwa inayopelekea kuvurugika kwa mazingira ya uke ni kufanya ngono na wanaume tofautitofauti. Kwanini? kwasababu unahamisha bakteria wa eneo moja na kuwapelekea eneo jingine.

Kuhamisha vimelea, inafanya mazingira ya eneo husika kuvurugika na kinga kushuka. Kwahivo hata kufanya ngono wa mdomo, kunyonya uke na uume vitakufanya uugue.

Wanawake pia wasiofanya ngono mara kwa mara wanaweza kupata tatizo hili kutokana na mabadiliko ya homoni na kusafisha uke kupita kiasi.

3.Maambukizi kwenye njia ya mkojo(UTI)

Maambukizi ya bakteria kwenye njia ya mkojo yanaweza kusababisha kutokwa na harufu ya shombo la samaki ukeni. Dalili zingine za UTI ambazo waweza kupata ni pamoja na muwasho , kuungua na maumivu wakati wa kukojoa.

4.Jasho

Jasho kutokana na kazi mbali mbali kama mazoezi na mabadiliko ya hali ya hewa, inaweza kusababisha utokwe na harufu ya shombo la samaki kwenye uke.

Vipimo Kwa Tatizo la Harufu ya Shombo la Samaki Ukeni

Endapo unapata harufu na dalili zisizo za kawaida kwenye uke wako, muone daktari haraka. Daktari atafanya uchunguzi wake kwa kukutazama ukeni kuona kama kumevimba.

Daktari pia anaweza kuchukua sampuli ya uchafu na kupeleka maabara kufanya vipimo zaidi.

Lini Unatakiwa Kumwona Daktari?

Unatakiwa kumwona daktari kama unapata dalili hizi pia

  • muwasho ukeni
  • kuungua ndani ya uke
  • maumivu wakati wa kukojoa
  • maumivu baada ya tendo
  • kutokwa ana uchafu wenye harufu mbaya
  • kuvimba kwa mashavu ya uke na
  • uchafu usio wa kawaida wa kijani, njano au mweupe mzito.

Matibabu

Matibabu ya tatizo lako yanategemea na chanzo chake. Kama ilivoainishwa hapa chini

Matibabu kwa bacterial vaginosis: Daktari atakupa tiba antibiotics kutibu maambukizi ya bakteria. Dawa maarufu zaidi vidonge vya metronidazole(Flagyl) au ya kupaka ukeni mfano clindamycin.

Matibabu kwa fangasi ukeni: Endapo una fangasi daktari anaweza kukupatia dawa za kupaka mfano miconazole au tioconazole. Unaweza pia kununua dawa kwenye famasi ya karibu kutibu maambukizi haya fangasi.

Matibabu ya UTI: UTI hutibiwa kwa antibiotics na pia tiba ya nyumbani. Hakikisha unafuata ushauri wa daktari kabla ya kumeza antibiotics kwani kumeza kiholea kunasababisha usugu wa dawa.
Daktari pia atakushauri kunywa maji ya kutosha na kuepuka kahawa na soda.

Ushauri namna ya kusafisha uke

Epuka kutumia sabuni kuosha uke au manukato yoyote ukeni. Safisha uke kwa kuanzia mbele kurudi nyuma kuepuka kuhamisha bakteria kutoka mkunduni mpaka kweny uke. Safisha uke kwa maji ya uvuguvugu .

Badili nguo za ndani kila unapooga, walau mara mbili au tatu kwa siku. Hakikisha unasafisha vizuri mashavu ya uke baada ya kazi za kutwa nzima kuondoa majasho na uchafu.

Tumia Vidonge vyetu Asili vya UCP-Vinasafisha uke na kurejesha harufu nzuri.

Uterus cleansing pills (UCP) ni dawa yenye vidonge 2 kama vinavyoonekana kwenye picha hapo juu. Vinatumika kwa wiki moja kusafisha uke, kurejesha harufu nzuri na kutibu maambukizi ukeni.

Matumizi ya vidonge ni kwa kuweka kidonge ukeni na kutoa kila baada ya siku tatu, unapumzika masaa 24 unaweka kidonge kingine.

Vidonge vimetengenezwa kitaalamu kupitia muunganiko wa mimea na kuhifadhiwa vizuri ili kutunza uasili wa dawa pasipo kuwekwa kemikali.
Angalizo: Vidonge havifai kutumika kwa mjamzito na bikira.

angalizo

Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge vyenye mfanano na hivi vya UCP, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb.

Gharama ni Tsh 50,000/=
Tuandikie whatsapp no: 0678626254 kuanza Tiba.

Bofya kusoma kuhusu: Mashavu ya uke kuvuta, kuuma na kuvimba wakati wa hedhi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *