Uzito Mkubwa kwa Watoto

uzito mkubwa kwa watoto na kitambi
uzito mkubwa

Uzito mkubwa kwa watoto ni changamoto kubwa sana katika maisha yetu ya sasa. Watoto hawa si tu wanalemewa na uzito mkubwa bali wapo kwenye hatari zaidi ya kuugua magonjwa mengine makubwa.
Uzito mkubwa na kitambi kwa mtoto hauathiri tu uwezo wa mwili bali hata afya ya ubongo. Soma zaidi kujua ni chanzo cha tatizo na namna ya kuwanusuru watoto wasiingie kwenye janga hili linaloitesa dunia.

Nini kinapelekea uzito mkubwa kwa mtoto?

Historia ya wanafamilia, sababu za kisaikolojia, na mtindo wa maisha kiujumla vinachangia uzito mkubwa kwa mtoto. Watoto ambao wazazi wao ni wazito kupita kiasi wanaweza nao kukumbwa na changamoto hii. Lakini sababu kubwa ya uzito mkubwa kwa mtoto ni kula sana chakula kisicho sahihi na kutofanya mazoezi.

Lishe mbovu yenye sukari na wanga nyingi inapelekea uzito mkubwa kwa mtoto. Vyakula vya mtaani(fast food) kama chips, sosage, mndazi na vinywaji vyenye sukari ni kikwazo kikubwa.

Vyakula vya haraka kama mikate, soda, icecream na tambi ni adui mkubwa wa afya ya mtoto. Watoto wengi huongezeka uzito kwasababu wazazi wao hawajui namna gani ya kuandaa chakula salama kisichoongeza uzito haraka. Familia zingine haziwezi kununua matunda, mbogamboga na nyama kwa ajili ya mlo kamili.

Mtoto kutoshugulisha mwili huchangia kuongezeka uzito

Mtoto kutumia muda mwingi amekaa pasipo kujishugulisha ni chanzo kingine cha uzito mkubwa. Katika makundi yote ya watu, kitendo cha kutoshugulisha mwili kitakufanya uongezeke uzito maradufu. Mazoezi yanasaidia kuchoma mafuta yaliyohifadhiwa mwilini.

Matatizo ya kisaikolojia pia yanaweza kumfanya mtoto kuongezeka uzito. Mtoto anayepitia msongo wa mawazo kila kutokana na hali yoyote ile, homoni zake huvurugika na kumfanya kuongezeka uzito zaidi.

Uzito mkubwa kwa mtoto husababisha changamoto kubwa za kiafya
Changamoto hizi ni kama

Kisukari

Kisukari cha ukubwani (type 2 diabetes) ni aina ya kisukari kinachotokana na mwili kushindwa kurekebisha sukari kwenye damu. Kisukari chaweza kupeleke mtoto kupata athari kwenye neva, matatizo ya figo ma kinga kushuka. Watoto na watu wazima wenye uzito mkubwa wapo kwenye hatari zaidi ya kuugua kisukari.

Mogonjwa ya moyo

Kuongezeka kwa sukari na mafuta mabaya kwenye mishipa ya damu hupelekea kuongezeka kwa shinikizo la damu na magonjwa mengine ya moyo. Vyakula vyenye sukari kwa wingi na vyenye mafuta mabaya vinafanya presha ya damu kuwa juu.

Ugonjwa wa Pumu(Asthma)

Pumu ni ugonjwa unaopelekea kuvimba na kututuma kwa njia za hewa. Watoto wenye uzito mkubwa wapo kwenye hatari zaidi ya kuugua na pumu.

Changamoto za usingizi

Watoto wenye uzito mkubwa na kitambi wanapata changamoto za usingizi ikiwemo kukoroma usingizini, na kukosa usingizi mtamu.

Maumivu ya joints

Mtoto wako anaweza pia kupata maumivu ya jonts endapo ana uzito mkubwa.

Lishe kwa watoto wenye uzito mkubwa na kitambi

Kama unataka kumuokoa mtoto wako dhidi ya uzito mkubwa na kitambi, kubadili lishe yatakiwa kuwa kipaumbele chako kikubwa. Wazazi wana mchango mkubwa sana kwneye ulaji wa watoto wao.

Anza kusafisha jiko lako kwa kupunguza matumizi ya vyakula vya wanga na sukari. Badala ya kunywa soda na juisi za matunda mtoto apendelee kutumia juisi ya parachichi na matunda mengine yenye sukari kidogo sana.

Mtoto ale chakula kilichoandaliwa nyumbani kwakuwa utajua nini hasa kipo ndani ya chakula chako. Chakula cha mtaani kinawekwa sukari nyingi na mafuta mengi mabaya yanayomfanya mtoto kongezeka uzito.

Kwa maelezo ya kina kuhusu lishe yenye sukari na wanga kidogo na mafuta mazuri bofya hapa kusoma zaidi.

Mabadiliko ya mtindo wa maisha kuepusha uzito mkubwa kwa mtoto.

Kuna mikakati mingi ambayo wewe kama mzazi unaweza kumwelekeza na kumsimamia mtoto kufuatilia ili apunguze uzito na haitaye kumwepusha na magonjwa mengine makubwa. Hatua hizi ni pamoja na

Mtoto kutenga muda wa kucheza na wenzake.

Baada ya shule mtoto aruhusiwe kwenda kucheza na wenzake. Mzazi usimzuie mtoto kwenda kfanya michezo ya kitoto itamsaidia kuchoma mafuta yanayohifadhiwa mwilini. Mfundishe pia mtoto kushiriki mazoezi kama kuruka kamba, kukimbia na mchakamchaka.

Dhibiti muda wa kutazama TV kwa mtoto

Watoto wanaotazama televisheni muda mwingi na kucheza game kwenye kompyuta wanakuwa na uzito mkubwa zaidi. Mfundishe mtoto wako apende kusoma zaidi vitabu na kufanya mazoezi ya mwili. Yatamsaidia si tu kumkinga na maonjwa bali hata kuimarisha afya ya ubongo.

Hitimisho

Wewe kama mzazi fahamu kwamba una mchango mkubwa sana katika afya ya mtoto wako. Mfundishe njia zilizo salama za kutunza afya yake. Mfundishe namna ya kujiandalia chakula yeye mwenyewe. Mwelekeze hatari ya kula vyakula vyeye sukari kwa wingi .