Vyakula na Mazoezi ya Kuongeza makalio

makalio

Unahitaji kuongeza makalio?

Tofauti na waengi wanavodhani kwamba makalio makubwa ni mpaka uzaliwe nayo. Ukweli ni kwamba unaweza kutengeneza makalio yakawa makubwa kwa njia salama bila hata kutumia vidonge wala kufanyiwa upsuaji. Baadhi tu ya vyakula na mazoezi nitakayokwelekeza leo ukifatilia utaweza kutimiza ndoto yako kama mwanamke.

Naamini umeshasikia misemo mingi ikimpamba mwanamke mwenye tako kama huu “mwanamke tako sura hata mbuzi anayo“. Amini sasa hata wewe unaweza kutengeneza tako lako vizuri ukaweza kuwaringia kabisa wengine.

Vyakula Vya Kutumia mara Nyingi Kuongeza Makalio

Mayai

Mayai ya kuku au ya kanga yana virutubisho vingi sana kama madini ya selenium, vitamin B12, riboflavin na phosphorus ambayo kwa pamoja inasaidia kuongeza protini ya kutosha mwilini. Protini inasaidia kujengeza misuli na nyamanyama za kutosha kwenye eneo la makali yako. Pia viambata vya leucine na amino acid kwenye mayai vinasaidia kujenga tishu na pia kuzuia hali ya misuli kupungua.

Vyakula jamii ya Kunde

Vyakula hivi ni pamoja na maharage na karanga vina kiwango kikubwa cha protini ambacho kitasaidia kuimarisha ukuaji wa misuli.

Maparachichi

Matunda ya parachichi yana kiwango kikubwa cha mafuta mazuri, protini , vitamin C, vitamin b6 na magneisium.
Maparachichi pia yana kiwango kikubwa cha viondoa sumu mwilini yani antioxidants. Tafiti zinasema kwamba viondoa sumu hivi vinapunguza kuharibika kwa misuli na hivo kuacha makalio yako yakiwa bado yamejengeka.

Maziwa

Baada ya kufanya mazoezi ni vizuri sana upate kikombe cha maziwa , kwani ni muhimu katika ndoto yako ya kuwa na tako kubwa.Tafiti zinasema kwamba kunywa maziwa baada ya mazoezi kunaimarisha kujengengeka na kuimarika kwa misuli ya makalio.

Mbegu za maboga

Mbegu za maboga ni chakula kizuri kutafuna chenye virutbishi vingi muhimu kwa afya yako. Sasa pengine ulikuwa hujui kwamba ndoto yako ya kuwa na makalio makubwa yaweza kutimizwa wa kula zaidi mbegu hizi. Leo nakupa siri hakikisha hukosi mbegu hizi nyumbani kwako. Nunua osha zikaange anza kula kila siku utanishukuru.

Nyama ya Kuku

Bila shaka umekuwa ukila nyama ya kuku mara chache sana kw akutojua siri iliyoko ndani. Kuku ana protini nyingi sana, kiwango kidogo cha nyama ya kuku kwenye kiganja cha mkono ni sawa na gramy 24 za protini. Sasa kama unataka kuwa na makalio makubwa anza kula nyama ya kuku walau kila siku upate vipande viwili tu. Baada ya miezi miwili utakuja kunishukuru.

Muhimu kufahamu: Lishe nzuri ni muhimu sana kufanikisha ndoto yako ya kuwa na makalio makubwa. Lakini watakiwa kufahamu kwamba lazima ufanye na mazoezi ya viungo. Muunganiko wa mazoezi na lishe itakupa matokeo makubwa sana katika muda mfupi.

Mazoezi ya kuongeza makalio

kuongeza makalio
makalio

Hapa chini ni mazoezi unayotaiwa kufanya kuongeza makalio yako yawe makubwa.

Sumo Squats

sumo squats kuongeza makalio
sumo squats

Namna ya kufanya:Ukiwa umesimama wima panua miguu yako kidogo, huku vidole vya kiguu vikiwa vimenyooka mbele, kunja miguu yako kama vile unachuchumaa. Kaa hivo bila kutikisika kwa muda wa sekunde 30 kisha simama tena. Rudia zoezi hili seti 25 mpaka 30 asubuhi na jioni ukiwa hujala kitu chochote. Tazama picha hapo juu namna ya kufanya zoezi hili.

Donkey Kick

donkey kick

Namna ya kufanya: shika chini kwa mikono yako miwili huku kuono ukiwa umebinua kidogo kama vile unatambaa, huku kichwa kichwa chako kikiwa kimeangalia mbele.Sasa nyanyua mguu wako wa kushoto kama vile unampiga teke mtu aliyeko nyuma yako. Fanya hili zoezi kwa kurudi mara 15 kwa kila mguu.

Dead Lifts

dead lift

Namna ya kufanya: Kwa kutumia kifaa chao chenye uzito wa wastani(dumbells). Ukiwa umesimama inama taratibu kwa mbele na kurudi juu, hakikisha mikono yako haigusi mwili unapojipinda. Jaribu walau seti 20 kila siku. Tazama picha hapa juu namna ya kufanya.

Bofya kusoma hatua za kuondoa michirizi na mikunjokunjo kwenye ngozi