Vidonge vya Misoprostol vimekuwa vikitumika hasa pamoja na dawa zingine kwenye kutoa mimba. Lakini lengo kuu la dawa hii ni kuzuia maumivu ya tumbo pale unapotumia dawa kama asprin na ubuprofen. Hasa kama upo kwenye hatari ya kuugua vidonda vya tumbo au una historia ya kuugua vidonda vya tumbo.
Misoprostol inasaidia kupunguza changamoto kubwa hasa kutokwa damu kwenye vidonda. Dawa hii inalinda ukuta wa tumbo kwa kupunguza kiwango cha asidi kinachomwagwa kwenye ukuta wa tumbo.
Jinsi ya kutumia vidonge vya misoprostol.
Unapoenda kunua dawa famasi inaambatana na karatasi ya maelekezo. Soma vizuri karatasi hiyo kabla ya kuanza kumeza. Endapo una maswali hakikisha unauuliza daktari, nesi au mfamasia anayekuhudumia.
Dozi ya dawa itategemea na aina ya tatizo linalokusumbua. Kama unatumia dawa ili kuzuia vidonda vya tumbo, meza kwa mdomo mara nne kwa siku baada ya kula na uanpoelekea kulala ili kupunguza kuharisha. Au umeze kama daktari aivyoshauri. Kumbuka kumeza dawa kila siku muda ule ule.
Endapo unatumia misoprostol kwa ajili ya leba, mtoa huduma ataweka kidonge kwenye uke.
Epuka kutumia dawa za kupunguza asidi zenye madini ya magnesum wakati unameza misoprostol, kwasababu zinafanya uharishe kupita kiasi. Kama unahitaji dawa ya kupunguza asidi(antacid), zungumza na daktari kwanza au mfamasia akusaidie kuchagua dawa itakayokufaa.
Matokeo/Side effects ya Vidonge vya Misoprostol
Kichefuchefu na maumivu ya tumbo yanaweza kukupata wakati wa tiba. Kama dalili zitakuwa mbaya zaidi ni vizuri kurudi hospitali na kumweleza daktari. Kumbuka daktari anakwandikia utumie misoprostol kwasababu amejiridhisha kwamba faida za dawa ni kubwa kuliko madhara utakayopata.
Wagonjwa wengi wanaotumia dawa hii hawapati matokeo mabaya.
Kuharisha ni dalili kubwa pale unapotuma misoprostol na inatokea hasa wiki mbili baada ya kuanza kumeza dawa na kuisha baada ya wiki moja. Hakikisha unakunywa maji ya kutosha ili kupunguza hatari ya kuishiwa maji mwilini.
Usisite kumuona daktari
Muone daktari mapema endapo utapata dalili hizi mbaya zinazoonesha umepungukiwa sana na maji na madini kwa kuharisha. Dalili hizi ni kuishiwa nguvu, kupungua mkojo, mood kubadilika misuli kulegea na mapigo ya moyo kupungua.
Mjulishe daktari kama unapata dalili zingine za matatizo ya homoni hasa hedhi nzito kupita kiasi, aleji inayoleta muwasho na rashes hasa wenye ngozi ya uso,koo na ulimi.
Makala hii haiongelei madhara yote unayoweza kuyatapata. Kuna umuhimu wa kumjulisha daktari dalili/matokeo yoyote yasiyo mazuri utakayopata baada ya kutumia misoprostol.
Tahadhari unapotumia vidonge vya misoprostol.
Kabla ya kumeza misoprostol, mjulishe daktari au mfamasia anayekuhudumia endapo una aleji yoyote. Dawa hii inaweza kuwa na viambata vinavyoleta aleji kwa mtumiaji.
Mjulishe daktari historia ya magonjwa yoyote uliyonayo hasa magonjwa ya tumbo.
Matumizi ya pombe kila siku pamoja na tumbaku/sigara yanaweza kuongeza hatari ya kutokwa damu kwa vidonda tumboni. Punguza pombe na sigara wakati unaendelea na tiba.
Tegemea Kupata bleed nzito
Kama unameza misoprostol ili kutoa mimba endapo daktari ameidhinisha hilo kwasababu ya madhara ya ujauzito wako, unaweza kupata dalili za kutokwa mabonge ya damu. Ni muhimu kutembelea hospitali na kupata uangalizi wa karibu kipindi hichi. Mjulishe daktari kama utapata maambukizi ya bakteria baada ya kutoa mimba.
Dawa hii haitakiwi kutumika wakati wa ujauzito ili kuzuia vidonda vya tumbo. Kwasababu ni lazima itaathiri mtoto tumboni. Kama upo kwenye dozi ya misoprostol na hutaki kushika mimba mapema, tumia uzazi wa mpango.