Wanawake wengi wanashuhudia hali ya hedhi kuganda katika mzunguko wao. Damu inayoganda hutokanana tishu za ukuta wa mimba zilizobomoka na kutolewa nje. Makala hii itakueleza kwanini unapata shida hii, madhara yake, na namna tutakavokusaidia kupona tatizo lako.
Je ni kawaida Damu ya hedhi kuganda?
Kama mabonge ya damu ya hedhi ni madongo kama matunda ya strawberries na yanatoka hasa mwanzoni mwa hedhi hapo huna cha kuhofia. Kama mabonge unayopata ni makubwa kama limau na yanatoka muda wote wa hedhi, hapo kuna shida mahali na unahitaji kumwona daktari.
Unapaswa kumwona daktari pia kama unapata hedhi nyingi kiasi ya kubadilisha pedi mbili ndani ya masaa mawili.
Nini kinatokea mpaka unapata hedhi?
Wanawake wengi walio kwenye umri wa kushika mimba, yaani miaka 15 mpaka 40 wanapata hedhi kila baada ya siku 28 mpaka 35 za mzunguko. Ukuta wa mji wa mimba ambao hubomoka kwa kitaalamu huitwa endometrium.
Ukuta huu wa endometrium hukua kwa kasi kuelekea yai kupevuka, kutokana na ongezeko la homoni ya estrogen. Kukua kwa ukuta maandalizi ya kizazi kubeba kiumbe endapo mama anashika mimba katika mwezi husika.
Kama mimba haitafanyika homoni zingine za mwili hutolewa ili ukuta ubomoke na kutolewa nje kwa njia ya uke. Uchafu na damu inayotolewa ndio hedhi au wengi huita period.
Kinachopelekea damu kuganda
Kusaidia kuta za mfuko wa mimba zivunjwevunjwe na kutolewa vizuri, mwili huzalisha kemikali yaani anticougulants kuzuia damu kuganda na hivo kuruhusu uchafu kutoka vizuri.
Mwili unapozidiwa na damu kuwa nyingi kuliko uwezo wa kuzalisha anticougulants, inapelekea baada ya damu kuganda na kutoka yakiwa mabonge.
Hedhi nzito ya Mabonge
Mabonge haya ya damu hufanyika zaidi endapo unatokwa na damu nyingi kuliko kawaida(heavy bleed). Kwa wanawake wenye hedhi salama, wanapata mabonge ya damu mwanzoni tu mwa hedhi na huchukua muda mfupi kuisha.\
Kwa wanawake wenye hedhi isiyo salama, mabonge ya damu yanaweza kuchukua siku myingi zaidi kutoka na yakiambatana na maumivu makali.
Changamoto za kiafya zinazopelekea kutokwa na mabonge ya hedhi.
Baadhi ya magonjwa ya kizazi yanaweza kusababisha utokwe na damu nyingi yenye mabonge. Changamoto hizi ni kama
Kuziba kwa ukuta wa mimba(uterine obstruction) changamoto yoyote inayopelekea kuziba kwa ukuta wa mimba unatengezeza presha kubwa kwenye ukuta huu wa mimba na hivo kukufanya utokwe na mabonge ya damu ya hedhi.
Kuziba kwa ukuta wa kizazi kunaweza kusababishwa na
- vimbe kwenye kizazi
- kutanuka kwa kizazi na
- vimbe za saratani kwenye kizazi
Mabadiliko ya homoni na Hedhi Kuganda
Kukua na kubomoka kwa ukuta wa kizazi kunategemea hasa mabadiliko ya homoni. Homoni ni kama vichocheo vinavyoamrisha mwili kufanya kazi fulani katika wakati fulani. Ni homoni zinakufanya wakati gani upate hedhi, wakati gani hedhi ikome na wakati gani mayai yapevuke.
ikitokea kuvurugika kwa homoni na shughuli za mwili zinavurugika. Baadhi ya mambo yanayopelekea homoni kuvurugika ni pamoja na
- kukaribia kukoma hedhi
- kukoma hedhi
- stress
- kuongezeka uzito au kupungua ghafla
Dalili kubwa ya kukuonesha kwamba homoni zako zimevurugika ni pale hedhi yako inapovurugika, yaani kukosa hedhi, kupata hedhi ya muda mrefu zaidi au hedhi yenye maumivu makali sana.
Mimba kuharibika na kutoa mimba
Tafiti zinasema kwamba nusu ya mimba zote hutoka kabla ya muda wa kujifungua na pia mmoja kati wa wanawake wawili ameshawahi kutoa mimba katika maisha yake.
Mimba inapotoka hupelekea kupata bleed nzito sana iliyoganda hasa kama mimba ilikuwa bado changa.
Je Kuna Matatizo hedhi kuganda?
Muhimu kumwona daktari kama unapata damu ya kuganda mara kwa mara. Moja ya matokeo mabaya ya kutokwa na damu nyingi ni kupungukiwa damu. Upungufu wa damu unatokea pale mwili unapokuwa na upungufu wa madini chuma.
Dalili za kupungukiwa damu ni pamoja na
- mwili kuchoka sana na kizunguzungu
- ngozi ya mwili kubadilika
- kukata pumzi mara kwa mara na
- maumivu ya kifua
Matibabu ya Hedhi kuganda
Kutibu hedhi kuganda, ni muhimu kwanza kutibu shida ya hedhi nyingi kupita kiasi. Kwa kulingana na chanzo cha tatizo lako daktari atachagua tiba inayokufaa
Dawa za homoni
Daktari anaweza kuamua kukupa dawa za uzazi wa mpango za kurekebisha homoni ili kupunguza kukua kwa ukuta wa kizazi kupita kiasi. Dawa hizi pia zinaweza kusaidia kupunguza ukuaji wa vimbe yaani fibroids.
Kwa wanawake wasiotaka kutumia dawa za homoni, wanaweza kupatiwa dawa za kuzuia damu kuganda.
Tiba ya upasuaji
Wakati mwingine upasuaji ndio njia pekee inayoweza kukusaidia kwa tatizo lako la hedhi nyingi na nzito. Upasuaji unaweza kulenga kutanua mlango wa kizazi ili damu itoke vizuri.
Kwa wanawake wenye uvimbe yaani fibroids, upasuaji unaweza kufanyika kuondoa vimbe hizi endapo dawa hajifanya kazi. Kumbuka upasuaji wa kuondoa fibroids unategemea na ukubwa wa vimbe zako.
Kama uvimbe ni mkubwa sana, utahitaji kufanyiwa upasuaji mkubwa kupitia njia ya tumbo. Utakatwa kidogo tumboni na uvimbe utatolewa kupitia hapo.
Upasuaji mdogo kuondoa vimbe
Kama vimbe ni ndogo utafanyiwa upasuaji wa laparascopy, yaani matundu madogo yanatobolewa kupitia eneo la tumbo, kisha vifaa vya kamera na vya kukata uvimbe kuingizwa kupita matobo yale. Badaa ya upasuaji utazibwa matobo haya.
Baadhi ya wanawake wanawaweza kuamua kizazi kuondolewa kabisa(hysterectomy). Ongea na daktari kwanza kujua faida na hasara za kila aina ya upasuaji.
Je kuna njia zozote za kupunguza dalili mbaya za hedhi nzito?
Kutokwa na hedhi nzito kunaweza kauthiri sana maisha yako. Ukiacha maumivu ya kiuno na mgongo, unaweza kushindwa pia kufanya kazi zako vizuri. Dondo hizi zitakusaidia kupunguza dalili mbaya
- Kutumia dawa za kupunguza maumivu ambazo zinapatikana famasi
- Badilisha pedi kila baada ya masaa mawili. Unaweza pia kuvaa pedi mbili kwa wakati mmoja ili kuzia damu kuvuja kwenye nguo zako.
- Weka taulo au kipande cha nguo juu ya kitanda kabla ya kulala kuzuia damu kuchafua mashuka yako.
- Vaa nguo nyeusi ili zisioneshe matoke ya damu endapo damu itavuja na kuchafua nguo yako ya nje
- Muda wote unapoenda ofsini au matembezini beba kanga na pedi ya ziada.
- Kila mahali unapoenda hakikisha unajua mahali pa karibu pa kujisitiri endapo utahitaji kwenda chooni kubadili pedi
- Kunywa maji ya kutosha, kula zaidi vyakula vyenye madini chua kwa wingi kama maini, mboga za kijani nanyama.
- Usitumie vitu kama kahawa, chocolate,soda na vingine vya sukari nyingi wakati wa hedhi.
Tumia Vidonge asili vya Evecare kurekebisha hedhi yako
Evecare ni dawa asili na imetengenezwa nchini India kupitia mimea ua Ashoka, Asaparagus na lodh tree. Kwa miaka zaidi ya mitano ambayo tumekuwa tukihudumia wagonjwa wetu wa matatizo ya hedhi na homoni, tumepokea shuhuda lukuki.
Dawa itakusaidia kurekebisha homoni ili uanze kupata hedhi vizuri. Evecare inakuwa na vidonge 30, unameza vidonge viwili kila siku kwa muda wa wiki mbili.
Baada ya kutumia Evecare tegemea kupata matokeo haya:-
- Hedhi kutoka vizuri na nyepesi ya kawida
- Maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi kuisha kabisa
- Homoni kubalansi
- Mzunguko wa hedhi kurekebika na kuanza kupata kila mwezi
- Kizazi kuimarika sana hata kuongeza chansi ya kushika mimba kama wewe ni muhanga wa kukosa mimba kwa muda mrefu.
Bei ya Evecare ni Tsh 75,000/= Tunapatikana Dar, Magomeni.
angalizo
Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge fake vya evecare, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb