Makala hii itakupa maelekezo jinsi gani uweze kugundua chanzo cha maumivu ya kichwa yanayokupata. Hii itakusaidia kuamua njia sahihi ya kutibu tatizo lako pasipo kukimbilia kumeza vidonge vya kupunguza maumivu. Vidonge ambavyo vina madhara makubwa kama vikitumika kwa muda mrefu pasipo ushauri wa daktari.
Yafuatavyo ni Mazingira yanayofanya upate Maumivu ya Kichwa
Mwili kupungukiwa na maji
Watu hupata maumivu ya kichwa pale mwili unapopungukiwa na maji. Kama unapata maumivu ya kichwa baada ya kutapika sana, kutokwa na jasho jingi au mafua ya muda mrefu ni wazi kwamba unahitaji kunywa maji mengi ili kuondoa tatizo lako.
Kama ni mtu wa mazoezi sana na huna tabia ya kunywa maji ya kutosha mwili utapungukiwa na maji na ni lazima kichwa kitauma. Kwenye majira ya joto sana hupelekea mwili kutoa jasho jingi na kuishiwa maji. Kumbuka kwamba mwili unahitaji maji ya kutosha ili kuendesha shuguli za ndani.
Mwanga wa simu, computer na vifaa mbalimbali
Kuangalia TV kwa muda mrefu ama matumizi makubwa aya simu yanafanya misuli ya macho kukaza na hatimaye kupelekea macho kuuma. Vitu vingine vinavyopelekea kukaza kwa misuli ya macho ni kama kutazama kitu kimoja ama upande mmoja kwa mda mrefu.
Kwa muda mrefu mfano unapoendesha gari na kusoma. Kukaa kwenye mazingira yenye mwanga mkali sana ama mwanga hafifu, mwili kuwa mchovu na ukavu wa macho.
Badili uelekeo wa macho
Kutatua changamoto hii ya kukaza kwa misuli ya macho. Hakikisha badili uelekeo wa mahali unapoangalia kila baada ya dakika 20. Kama kuna kazi inakutaka utumie muda mwingi kuifatilia kwa macho basi hakikisha unabalansi na shughuli zingine ambazo zinahitaji pia matumizi ya macho.
Hakikisha pia kifaa chako kama simu, computer ama televisheni kipo mbali kuanzia cm 30 . Simu unapotumia iweke katika usawa wa chini kidogo na level ya macho. Kama tatizo ni kubwa ongea na dactari wako wa macho akushauri aina ya miwani ya kutumia ili kujikinga na miale ya mwanga.
Vichocheo vya mwili (hormones)
Kupungua kwa uzalishaji wa homoni ya estrogen huchangia mabadiliko ya utoaji wa kemikali kwenye ubongo zinazochangia maumivu ya kichwa. Inatokea zaidi kwa wanawake wanapokuwa kwenye kipindi cha hedhi.
Wanawake waliokoma hedhi ama wanaokaribia kukoma hedhi hupata pia maumivu ya kichwa kwa estrogen hupungua kwa kiasi kikubwa.
Uzazi wa mpango wa kisasa
Matumizi ya njia ya za kisasa kuzuia mimba na tiba ya homoni za kutegenezwa maabara (hormone replacement therapy) huchangia kuongezeka ama kupungua kwa baadhi ya homoni na kisha kupata maumivu ya kichwa.
Kwa wajawazito homoni ya estrogen huongezeka na kupelekea maumivu ya kichwa. Baadhi ya wanawake maumivu haya huisha ndani ya kipindi kifupi. Wengi hupata maumivu haya kwenye miezi ya kwanza ya mimba. Baada ya kujifungua kiwango cha estrogen hushuka tena.
Ukaaji wa mwili ni chanzo cha maumivu ya kichwa
Ukaaji na ulalaji mbovu unapelekea mgandamizo mkubwa eneo la juu nyuma ya mwili na kwenye mabega na hivo kupelekea maumivu ya kichwa. Maumivu unayoyapata baada ya kulala ama kukaa au kusimama kwa muda flani ni matokeo ya mwili kutobalansi.
Kutoshugulisha mwili inapelekea maumivu ya kichwa
Mazoezi ya mwili ikiwemo kukimbia, kuendesha baiskeli, au squats husaidia mwili kutoa kemikali ambazo ni pain killer mfano endorfins.
Watu wasiofanya mazoezi na wanaotumia muda mwingi wamekaa pasipo kushughulisha miili ni wahanga wa kuumwa kichwa. Hakikisha unaweka ratiba walau mara 3 kwa week kufanya mzoezi.
Matumizi ya dawa
Baadhi ya dawa ya kupunguza maumivu zikitumika kwa muda mrefu naweza kuleta maumivu ya kichwa. Matumizi ya dawa ambazo zipo kwenye kundi la nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs) husababisha tatizo kuwa baya zaidi.
Msongo wa mawazo ni chanzo cha maumivu ya kichwa
Msongo wa mawazo hupelekea misuli yako kukaza na hivo kubadili namna ubongo unavotoa kemikali hadi kupelekea maumivu ya kichwa. Kama wewe ni muhanga wa stress unaweza kusoma vzuri kuhusu namna sahihi za kudeal na msongo wa mawazo hapa.
Kelele
Kukaa kwenye mazingira yenye kelele nyingi kwa muda mrefu hisababisha kuumwa kichwa .
Ni muda gani unatakiwa kumwona daktari.
Endapo utapata dalili zifuatazo hakikisha unamwona dactari haraka
- maumivu ya muda mrefu pasipo kupata nafuu
- maumivu ya kichwa yanayoambatana na homa
- kupungua kwa uwezo wa kuona na shingo kuwa ngumu
- kushindwa kutembea na tatizo kwenye kuongea na
- kukosa nguvu ama kutetemeka kwa eneo moja la mwili
Njia gani utumie ili kupunguza maumivu ya kichwa kabla ya kumwona Daktari.
- Tumia kipande cha barafu kwenye mfuko weka kwenye eneo la mbele la kichwa.
- Kunywa maji ya kutosha walau glass 8 kwa siku
- Fanya mazoezi madogo ya kutembea hasa kutembea peku kwenye mchanga wa bahari
- Kaa mbali na eneo lenye kelele na mwanga mkubwa, tafuta eneo lililotulia
Kumbuka ni muhimu kumwona daktari endapo dalili za kuumwa kichwa zitendelea zaidi pamoja na kwamba umetumia njia za kupunguza maumivu haya.
5.Tumia mafuta ya Lavender kutibu maumivu, msongo wa mawazo na kuleta usingizi mzuri.
Kama wewe ni mmoja ya mamilioni ya watu wanaoteseka na maumivu ya kichwa kila siku, mafuta ya lavender yanaweza kuwa mkombozi wako. Ni moja ya mafuta adimu ya asili kutibu maumivu ya kichwa.
Matumizi: Chukua kiwango kidogo cha mafuta kwenye kidole chako, kisha sugua eneo ya nyuma ya shingo na eneo la nyuma ya masikio yako. Fanya hivo kabla ya kulala na asubuhi baada ya kuoga. Chukua pia mafuta kiasi vuta hewa yake na matone mengine dondosha kwenye mto wa kulalia.
Tumia mafuta haya kila siku kwa wiki mbili. Utaanza kupata matokeo mapema ndani ya siku moja tu ukianza kutumia. Huna tena haja ya kumeza vidonge vyenye madhara. Unaweza kuagiza mafuta kutoka kwetu.