Dawa ya anusol kutibu bawasili

dawa ya anusol
vidonge vya anusol

Dawa ya anusol hutumika kupunguza maumivu makali na muwasho kutokana na bawasili. Bawasili ni tatizo la kuota kinyama sehemu ya haja kubwa. Inaweza kuwa kwa nje ama bawasili ya ndani. Dawa ya anusol ya kuingiza mkunduni ina viambata vya zinc oxide, starch na cocoa butter kusaidia kupunguza muwasho wakati wa kujisaidia.

Jinsi ya kutumia anusol ya kuingiza mkunduni

Muhimu kumsikiliza daktari au mfamasia wakati anakwelekeza matumizi ya dawa. Kabla ya kuanza dozi, safisha eneo la haja kunwa kwa maji ya ukaushe kwa taulo au kitambaa safi na laini.

Fungua dawa kutoka kwenye pakiti yake, lala kwa ubavu wa kushoto na ukujne mguu wa kulia. Taratibu ingiza kidonge ndani ya tundu la haja kubwa kwa kutumia kidole chako. Usiingize zaidi ya inch moja ndani.

Dozi ya dawa

Dawa hii mara nyingi hutumika mara sita ndani ya siku moja. Au kila baada ya kwenda haja kubwa kama daktari alivyokwelekeza. Dozi yako itategemea na ukubwa wa tatizo na historia yako. Usitumie dawa ya anusol kwa muda mrefu zaidi ya ulivyoelekezwa na daktari.

Kama kidonge ni laini sana kiasi ya kushindwa kupush kwenda ndani, Weka kwenye friji kabla ya kukifungua kwa nusu saa ndipo uingize.

Matokeo/ ya dawa ya anusol

Kwa kiasi kikubwa dawa hii haileti matokeo mabaya mwilini. Endapo umetumia dawa kwa zaidi ya wiki na hujaona matokeo yoyote muone daktari.

Kama daktari ameelekeza upatiwe dawa hii, fahamu tu kwamba amejirisha dawa itakupa faida nyingi zaidi kuliko madhara yake. Wagonjwa wengi wa bawasili wanapotumia anusol hawapati madhara yoyote.

Endapo una aleji yoyote, mweleze daktari kabla hujaanzishiwa tiba. Dalili kama kizunguzungu, vipele, muwasho au kuvimba uso na koo inaonesha una aleji na dawa.

Jarida hili linaweza lisitoe maelezo ya dalili zote. Hivo kama utajisikia dalili zingine mbaya zaidi ya hizi tulizoandika muone daktari mapema.

Angalizo

Usitumie dawa ya anusol kama bawasili yako imefikia hatua ya kutoa damu na kuvimba sana eneo la haja kubwa.

Kama hujapata nafuu ndani ya siku saba, na kama damu inaendelea kutoka na maumivu ni makali sana, rudi hospitali haraka.

Dawa isitumike kabisa kwa watoto chini ya umri wa miaka 12. Na kwa wajawazito dawa itumike tu pakiwa na ulazima.

Dawa inaweza kukudhuru endapo utaimeza. Kama mtu amemeza dawa kwa bahati mbaya, apelekwe hospitali haraka.

Ushauri kwa mgonjwa wa bawasili

Kama unataka kuwahi kupona mapema, na tatizo lisjirudie, zingatia ushauri huu hapa chini

  1. Kula mbogamboga za majani, na nafaka zisizokobolewa. Matumizi ya vyakula vya nyuzinyuzi kwa wingi husaidia kuongeza ukubwa wa kinyesi na hivo kurahisha utolewaji wake. Kama mwanzo hukutumia vyakula vya nyuzinyuzi basi anza kuongeza taratibu kwenye mlo wako mpaka pale tumbo litakapozoea.
  2. Tumia machungwa kwa wingi, machungwa yana kiungo kinachoitwa flavonoids, kiungo hiki ni muhimu katika ustawi wa mishipa ya damu ya veins, mishipa hii ndio huathirika na kuletekeza bawasiri.
  3. Kunywa maji ya kutosha kila siku, tumia kiu na rangi ya mkojo kama kiashiria cha kiasi gani cha maji unatakiwa kunywa. Kama mkojo ni wa rangi ya njano inayokolea basi ni kiashiria kwamba mwili hauna maji ya kutosha na unatakiwa kunywa.
  4. Hakikisha unapata virutubisho kwa ajili ya kusawazisha bacteria wazuri ndani ya mfumo wa chakula, vyenye ubora wa hali ya juu usimeze kila kirutubisho. Kama huna chanzo kizuri cha kupata virutubisho hivi tunashauri fika ofsini kwetu kupata usaidizi.
  5. Usitumie nguvu kubwa kujikamua kutoa haja, tumia misuli ya tumbo kutoa haja taratibu.
  6. Unapotoa haja basi hakikisha unachuchumaa kama miili yetu ilivoumbwa. Watu wanaotumia njia hii mara chache sana huugua bawasili, lakini matumizi ya vyoo vya kukaa ni moja ya kihatarishi cha kupata bawasili.
  7. Usitumie nguvu kubwa kujifuta kwa toilet paper ama wipes zingine baada ya kwenda haja, hii hufanya ngozi kulanika na kuvimba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *