Kondomu ya kike ni kifaa kilichotengenzwa kwa mpira laini. Kifaa hiki hukwekwa ukeni na kujishikiza kwenye kuta za uke. Kazi yake ni kukusanya manii na mbegu za kiume ili mwanamke asipate mimba isiyotarajiwa.
Kondomu ya kike inakuwa na ringi ndogo mbili moja inakuwa juu kwenye mdomo wa kondomu na ingine inakuwa chini ndani ya kondomu.
Jinsi ya kutumia Kondomu Ya Kike
Matumizi ya kondomu ya kike hayatofautiani sana na namna ya kutumia tampon au pedi za kuingiza ukeni. Fanya haya ili utumie kwa usahihi kondomu yako
- Tumia kondomu kila mara unapohitaji kukutana na mwanaume
- ifungue taratibu na hakikisha kucha zako zimefupi ili usikate kondomu na kuleta matobo
- Weka kondomu ndani ya uke kabla uume haujaingia wakati wa tendo
- Weka kilainishi mwishoni kwa kondomu yako
- Tafuta mkao mzuri ili kondomu iingie vizuri ukeni, mfano unaweza kulala kitandani, kuchuchumaa, au kusimama kwa mguu mmoja na mwingine ukiuweka kwenye kiti.
- Kwa kutumia vidole vyako ingiza ringi ndogo ile ya chini ya kondomu, isukume ndani ya uke mpaka mwisho wa vidole vyako.
- Wakati wa tendo mwanaume ahakikishe uume unaingia kwenye kondomu wakati wote wa tendo.
- Baada ya tendo shika vizuri ringi ya juu kwa mikono yako miwili kisha vuta taratibu ili usimwage mbegu.
Je Kondomu ya kike ni salama na ina uwezo kiasi gani?
Kondomu za kike zinafanya kazi vizuri kama ilivyo kwa kondomu za kiume. Kama tu zikitumika kwa usahihi zina ufanisi wa asilimia 95. Kwa maana hiyo ni kwamba kati ya wanawake 100 wanaotumia kondomu za kike ni watano tu ndio wanaweza kushika mimba.
Kumbuka kwamba kondomu ya kike haizuii moja kwa moja usipate magonjwa ya zinaa kama kaswende na kisonono, bali inapunguza tu hatari. Kwa kiasi kikubwa kondomu hizi zitakusaidia kuzuia usipate mimba ambayo hukuipangilia kuipata.
Faida ya kondomu za kike ukilinganisha na kondomu ya kiume
- Unaweza kuiweka ukeni hata masaa 8 kabla ya tendo ili isikutoe mchezoni pale ambapo unajiandaa kufanya tendo.
- Wanawake wanaweza kuamua wenyewe kujikinga hata kama mwanaume anagoma kuvaa kondomu ya kiume.
- Kondomu hii hubakia ukeni hata kama uume utalegea baada ya kumwaga mbegu.
- Huhitaji kuondoa kondomu yako haraka baada ya tendo, unaweza kusubiri ukafurahia kufika kileleni kwa muda ndipo utoe kondomu.
Ubaya wa kondomu za kike Ukilinganisha na Kondomu za kiume
- yaweza kuhama kwenye uke wakati wa tendo
- inaweza kuleta muwasho kwa mwanamke au mwanaume pia
- inapunguza msisimko wakati wa tendo , na kufanya mwanaume kuchelewa sana kumwaga mbegu
- zinaweza kuleta sauti ama kelele wakati wa tendo, tumia vilainishi vilivyoidhinishwa kupunguza mlio
- gharama yake ni kubwa kuliko kondomu za kike lakini pia size yake ni moja tu kwa wote