Fangasi inaweza kuathiri eneo lolote la mwili wako. Fangasi wanaoitwa onychomycosis au tinea unguium, nia aina ya fangasi wanaoathiri sana kucha za vidole vya miguu na dole gumba la mguuni. Maambukizi ya fangasi huanza taratibu na kusambaa, kwahivo mabadiliko yoyote ya mwonekano wa kucha zako siyo jambo la kupuuza kabisa.
Kwanini unaugua fangasi za kucha
Kila eneo la mwili lina kiwango fulani cha fangasi, iwe kwenye kucha, ngozi, mdomoni na ukeni, mkunduni na kwenye uume. Unaanza kuugua fangasi pale vimelea hawa wanapomea kupita kiasi. Vimelea wa fangasi wakua zaidi kwenye mazingira ya unyevunyevu na joto.
Vimelea wa fangasi waliopo ndani ya mwili wako wanaweza kukuletea athari pale mazingira ya mwili yanapovurugika. Pia endapo utagusana na mtu mwenye maambukizi unaweza kuugua fangasi.
Endapo unapenda kwenye saluni kusafisha kucha zako, hakikisha unamkumbusha muhudumu kutakasa kwanza vifaa vyake. Hii itasaidia kupunguza hatari ya wewe kupata maambukizi ya fangasi kutoka kwa mtu mwingine.
Nani yupo kwenye hatari zaidi ya kuugua fangasi za kucha?
Kuna sababu nyingi zinazopelekea uugue fangasi za kucha. Tiba ya tatizo itategemea na chanzo cha tatizo lako. Upo kwenye hatari zaidi ya kuata fangasi za kucha kama upo kwenye makundu haya
- unaugua kisukari
- una umri zaidi ya miaka 65
- wanapenda kuvaa kucha bandia
- unapenda kuogoelea kwenye swimming pool za watu wengi
- una jeraha kwenye kucha
- kucha zako zina unyevunyevu kila mara
- kinga yako ya mwili imeshuka
- kuvaa viatu vya kufunika muda muda mwingi
wanaume wanaugua zaidi kuliko wanawake
Maambukizi ya kucha ni tatizo linalojitokeza zaidi kwa wanaume kuliko wanawake. Na pia inatokea zaidi kwa watu wazima kuliko watoto. Kama una ndugu wa familia wanaougia sana tatizo hili, wewe pia upo hatarini kupata fangasi za kucha.
Wazee wapo kwenye hatari zaidi ya kuugua fangasi za kucha, kwasababu ya kupungua kwa kasi ya usafirishaji ndani ya mwili. Pia kucha zinarefuka taratibu sana kadri umri unavosogea.
Dalili za fangasi kwenye kucha
Fangasi kwenye kucha moja inaweza kuathiri pia kucha ya kwenye kidole kingine na pia hata kidole chenyewe. Dalili kubwa ni pamoja na
- kupinda kwa kucha
- harufu mbaya kutoka kwenye kucha
- kucha kuwa ngumu sana na nene
Nitajuaje kama tayari naugua fangasi ya kucha?
Kwasababu kucha zako zinaweza kuathiriwa na magonjwa mengine, njia sahihi ya kujua kama ni fangasi ni kwa kumuona daktari. Daktari atachukua sampuli ya kucha iliyoathiria na kuipeleka maabara kwa ajili ya uchunguzi.
Matibabu ya fangasi za kucha
Siyo salama kujinunulia dawa na kutumia pasipo kumuona daktari. Daktari anaweza kupendekeza dawa mbalimbali za kumeza ili kupambana na fangasi kama
- itraconazole
- fluconazole na
- griseofulvin
Pia daktri anaweza kupendekeza utumie na dawa za kupaka kupambana na fangasi. Dawa hizi za kupaka utatumia kwenye kucha kama vile unavyopakaa rangi.
Dondoo za kukusaidia usiugue fangasi za kucha
Endapo utabadili baadhi ya vitu kwenye mtindo wako wa maisha, itakusaidia kuzuia usipate maambukizi ya fangasi kwenye kucha. Usafi wa kucha kwa kuzikata mapema ni muhimu. Pia jitahidi kujikinga na majeraha kwenye ngozi ya kucha. Endapo utakaa kwenye eneo la maji maji kwa muda mrefu hakikisha unavaa gloves za plastic kuzuia vidole kulowana.
Mambo mengine ya kufanya ni pamoja na
- kuosha mikono yako baada ya kushika kucha iliyoathirika
- kausha vidole vizuri baada ya kuoga hasa katikati ya vidole vya miguu
- pata huduma za manicure na pedicure kutoka kwenye saluni ya kuaminika
- epuka kutembea peku kwenye maeneo ya watu wengi
- punguza matumizi ya kucha za bandia na rangi za kupaka kucha
Tiba asili kwa tatizo la fangasi za kucha
Kumbuka pamoja na tiba hizi asili za numbani, ni muhimu sana kumuona daktari kwa ajili ya vipimo na ushauri wa kina. Hizi ni baadhi ya tiba unazoweza kutumia ukiwa nyumbani kabla ya kwenda hospitali
Mafuta ya tea tree: yana viambata vya kupamaban ana fangasi pamoja na vimelea wabaya. Matumizi yake ni kwa kupakaa mafuta haya kwenye kucha mara mbili kwa siku kwa kutumia pamba.
Apple cider vinegar. Matumizi: chukua vijiko vitani vya apple vinegar, changanya na maji nusu lita, kisha chivya mguu ulioathirika kwa dakika 20 kila siku.
Kitunguu saumu: Unaweza kutibu fangasi ya kucha kwa kutumia kitunguu saumu kwa kuponda kitunguu chako na kupakaa eneo la kucha, kisha subiri wa dakika 30 ndipo jisafishe.
Rekebisha lishe yako kwa kupunguza kwa kiasi kikubwa vyakula vya sukari na kula zaidi vyakula vyenye mafuta mazuri kama nazi, mafuta ya olive, protini, maziwa mtindi. Pia vyakula vyenye madini chuma kwa wingi kama mboga za kijani ilichokolea, beetroot,parachichi, maharage na maini.
Tumia Propolis Kutibu Fangasi Yako
Ni vidonge asili viliyotengenezwa kupitia bidhaa adimu ya propolis ili kutibu mambukizi sugu ya fangasi mwilini. Dozi moja inatumika kwa wiki mbili, unameza kila siku vidonge viwili asubuhi na jioni. Huhitaji kufanya utafiti ni dawa ipi nzuri, tayari tumeshafanya hivo kwa zaidi ya miaka mitano sasa na kukuletea dawa hii iliyothibitishwa.
Baada ya kutumia propolis tegemea haya ndani ya wiki mbili
- Fangasi yako kupona kabisa
- Dalili zote mbaya mbaya muwasho na maumivu kuisha
- Kinga ya mwili kuimarika na fangasi kutojirudia
Gharama ni Tsh 90,000/=, Tupo Magomeni Dar. Chati nasi kwa whatsapp no- 0678626254 kuanza tiba
Hitimisho
Kwa baadhi ya watu, fangasi za kwenye kucha inaweza kuwa tatizo gumu kutibu, na dozi ya kwanza inaweza isifanye kazi. Yawezekana kabisa kwa maambukizi ya fangasi kurejea tena baada ya kupona. Endapo tatizo litakuwa kubwa sana, linaweza kusababisha madhara ya moja kwa moja kwenye kucha yako na kuhitaji kuondolewa kwa upasuaji mdogo.
Ni muhimu sana kumuona daktari kama una fangasi za kucha na pia unaugua kisukari. Watu wenye kisukari wako kwenye hatari ya tatizo la fangasi ya kucha kuchelewa kupona. Nenda hospitali onana na daktari kama unaugua kisukari na unahisi tayari una fangasi kwenye kucha.