Hedhi nyepesi sana na inatoka kidogo

hedhi nyepesi
damu ya hedhi

Napata hedhi nyepesi sana je ni kawaida?

Kwa mwanamke ni muhimu sana kuielewa hedhi yako vizuri. Ni muhimu kujua kipi ni sahihi na dallili ipi siyo sawa kwenye hedhi yako. Hedhi ni matokeo ya kubomoka kwa ukuta wa mimba pale mimba isipotungwa. Kulingana na changamoto za kiafya unaweza kupata hedhi nyepesi sana au nzito kupita kiasi.

Wanawake wengi hupata hedhi yao karibu kila baada ya siku 21 mpaka 35. Hedhi inaweza kutoka kwa siku tatu mpaka saba. Japo hedhi inaweza kutofautiana mwonekano na wingi kulingana na mzingira fulani, mfano ukiwa na mimba huwezi kupata hedhi kwa sababu ukuta unaotakiwa kubomoka tayari umeshikilia mtoto.

Dalili ya kwamba unapata hedhi nyepesi sana kuliko kawaida

Hedhi nyepesi inaweza kuwa tatizo endapo

  • unapata hedhi siku chache, chini ya siku mbili
  • unapata matone tu ya damu
  • umevusha mzunguko bila kuona hedhi
  • unapata hedhi ya kujirudia mara mbili au zaidi ndani ya mzunguko wako

Kumbuka unaweza kupata hedhi nyepesi na isiwe kiashiria cha tatizo lolote. Pengine umebadili mazingira tu. Hakikisha unamweleza daktari jambo hili. Daktari atakusaidia kucheki chanzo cha tatizo lako.

Nini kinasababisha upate hedhi nyepesi

Hedhi au bleed nyepesi inachangiwa na vitu vingi ikiwemo

Umri

Hedhi yako inaweza kutoka vizuri sana ukiwa bado ni binti yaani chini ya miaka 40. Pale unapokaribia kukoma hedhi (menopause) hedhi itaanza kuvurugika na kutoka kidogo kidogo. Nyakati hizi utashuhudia hedhi nyepesi sana na wakati mwingine kuvusha hata miezi mitatu bila kuona hedhi.

Lishe na uzito huchangia hedhi nyepesi

Uzito wako na lishe vina mchango mkubwa sana katika mwenendo wa hedhi yako. Ukiwa na na uzito mkubwa sana unaweza kupata hedhi nzito na inayochukua siku nyingi. Unapokuwa na uzito mdogo sana kuliko kawaida utapata hedhi nyepesi sana kwasababu homoni zako hazifanyi kazi ipasavyo. Lishe yenye kiwango kikubwa cha sukari na wanga pia huvuruga homoni zako.

Ujauzito.

Ukiwa mjamzito hedhi inakoma kwanza mpaka pale utakapojifungua. Lakini unaweza kutokwa na matone ya damu na ukafikiri ni hedhi kumbe siyo. Matone haya hutoka hasa ndani ya siku 12 baada ya yai kurutubishwa, na husababishwa na kitendo cha kiumbe kujishikiza kwenye ukuta wa kizazi.

Jifunza zaidi kuhusu dalili za mimba changa kwa kubofya hapa.

Kunyonyesha

Baada ya kujifungua utaanza kunyonyesha. Hedhi haitarudi kwenye mpangilio wake haraka badala yake utaanza kuona matone matone ya damu. Homoni za maziwa huzuia yai kupevuka, na hivo kupelekea kuchukua miezi kadhaa mpaka hedhi kurudi kawaida.

Kumbuka hili, unaweza kushika mimba hata kama unanyonyesha. Hata kama hedhi yako bado haijarudi kwasababu ni lazima yai litapevuka na kutolewa kabla ya hedhi yako ya kwanza. Kama ulikutana na mwanaume bila kinga na unapata hedhi nyepesi au matone ya damu basi muhimu kufanya kipimo cha mimba.

Uzazi wa mpango unachangia hedhi nyepesi

Njia za uzazi wa mpango zinazobadilisha mpangilio wa homoni zinaweza kusababisha upate hedhi nyepesi. Baadhi ya njia hizi huzuia mayai kupevuka. Njia hizi ni kama

Kama mayai hayapevuki na kutolewa, ukuta wa mimba hauwezi kujengeka na hivo hakuna ukuta utakaobomoka ili damu ya hedhi itoke. Unaweza kuendelea kukosa hedhi au kuvusha mzunguko bila kuona hedhi hata kama umeshaacha kutumia uzazi wa mpango.

Stress zinaweza kupelekea hedhi nyepesi

Unapokuwa na stress aidha stress ya kihisia au stress ya mwili inapelekea ubongo kubadili mpangilio wa homoni. Unaweza kuvusha mzunguko bila kuona hedhi au kupata hedhii nyepesi. Baada ya muda mwili ukiwa hauna stress hedhi yako itarudi kawaida.

Kufanya mazoezi kupita kiasi

Wanawake wanaofanya mazoezi mara kwa mara au mazoezi magumu, huona mabadiliko kwenye mpangilio wao wa hedhi.

Ugonjwa wa polycystic ovary syndrome(PCOS)

Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (ovary) hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke. Uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndio unaojulikana kama ovarian cyst.

Wakati fulani mifuko midogo hujitengeneza juu ya yai lililokomaa, kimfuko hichi hupotea pale yai linapotolewa kwenye hedhi. Pale inapotokea yai limekomaa na halijatolewa basi kimfuko hichi hujifunga na kuwa na maji ndani yake. Kimfuko hichi tunakiita ovarian cyst na vinapokuwa vingi tunaviita polycystic.

Kwahiyo Polycystic ovarian syndrome ni mkusanyiko wa dalili zinazoambatana na uwepo wa vimbe hizi ndogo ndogo(cysts) kwenye mifuko ya mayai ya mwanamke.

Uvimbe huu unaweza kumtokea mwanamke wa umri wowote ingawa mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito yaani menopause.

Vipimo na Tiba kwa Tatizo la PCOS

Kujua kama una ugonjwa huu wa PCOS, daktari atakufanyia utrasound. Kamaa tayari una PCOS daktari anaweza kupendekeza upunguze kwanza uzito wako na kumeza dawa za uzazi wa mpango kurekebisha homoni zako.

Daktari anaweza kukupatia dawa ya metformin ambayo hutumika zaidi na watu wenye kisukari. Zitakusaidia kurekebisha homoni ya insulini kwenye damu na hivo kukusaidia mayai yaweze kupevuka.

Lini unatakiwa kumwona Daktari?

Muone daktari endapo

  • umekosa hedhi tatu mfululizo na hauna mimba
  • unafikiri umeshika mimba na huna uhakika
  • hedhi yako inavurugika
  • unapata bleed katikati ya mzunguko
  • unapata maumivu makali wakati wa hedhi
  • muone pia daktari aendapo unapata dalili zingine ambazo hatujaziandika hapa

Matibabu kwa changamoto ya hedhi nyepesi

Matibabu ya tatizo la hedhi nyepesi na kidogo yatategemea na chanzo cha tatizo lako. Daktari atakuuliza baadhi ya maswali na kukufanyia vipimo na kukuanzishia dawa kulingana na alichogundua.

Kwa kiasi kikubwa unaweza kutibu shida hii kwa kurekebisha mtindo wa maisha yako na dawa unazotumia. Matumizi ya uzazi wa mpango wa kisasa ni chanzo kikubwa cha tatizo. Ongea na mtoa huduma akupe ufafanuzi juu ya njia za uzazi wa mpango ambazo hazibadilishi mpangilio wa homoni zako.

Tumia Vidonge asili vya Evecare

Evecare ni dawa asili na imetengenezwa nchini India kupitia mimea ua Ashoka, Asaparagus na lodh tree. Kwa miaka zaidi ya mitano ambayo tumekuwa tukihudumia wagonjwa wetu wa matatizo ya hedhi na homoni, tumepokea shuhuda lukuki.

Dawa itakusaidia kurekebisha homoni ili uanze kupata hedhi vizuri. Evecare inakuwa na vidonge 30, unameza vidonge viwili kila siku kwa muda wa wiki mbili.

Baada ya kutumia Evecare tegemea kupata matokeo haya

  • Hedhi kuanza kutoka vizuri na ya kutosha
  • Maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi kuisha kabisa
  • Homoni kubalansi
  • Mzunguko wa hedhi kurekebika na kuanza kupata kila mwezi
  • Kizazi kuimarika sana hata kuongeza chansi ya kushika mimba kama wewe ni muhanga wa kukosa mimba kwa muda mrefu.

Bei ya Evecare ni Tsh 75,000/= Tunapatikana Dar, Magomeni.

tahadhari

Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge fake vya evecare, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb

Chati na daktari kwa whatsapp no. 0678626254 kuanza tiba

Soma zaidi njia mbalimbali za uzazi wa mpango kwa kubofya hapa.